Zaka: Kufungua Madirisha ya Mbinguni
Dondoo
Yote tuliyonayo na jinsi tulivyo vinatoka kwa Mungu. Kama wafuasi wa Kristo, tunashiriki kwa hiari na wale wanaotuzunguka.
Pamoja na yote Bwana anayotupatia, ametuomba tumrudishie Yeye na ufalme wake duniani asilimia 10 ya ongezeko letu. Ametuahidi kwamba tunapokuwa waaminifu katika zaka zetu, Yeye “atafungua … madirisha ya mbinguni, na kumwaga … baraka, kwamba hapatakuwa na nafasi ya kutosha kuhifadhi.” [Malaki 3:10]. Ametuahidi kwamba Atatulinda dhidi ya maovu. …
Madirisha ya mbinguni yanafunguka kwa njia nyingi. Baadhi ni za kimwili, lakini nyingi ni za kiroho. Baadhi ni ndogo na rahisi kupuuzwa. Tumaini katika wakati wa Bwana; baraka daima zinakuja. …
… Ulimwengu unazungumza juu ya zaka kulingana na pesa zetu, lakini sheria takatifu ya zaka kimsingi ni suala la imani yetu. Kuwa waaminifu katika zaka zetu ni njia mojawapo tunayoonesha nia yetu ya kumweka Bwana kwanza katika maisha yetu, kupita wasiwasi na maslahi yetu wenyewe. Ninakuahidi kwamba kadiri unavyomtumaini Bwana, baraka za mbinguni zitafuata. …
Nyongeza ya neema ya Bwana inayotolewa kupitia zaka zako za ukarimu imeimarisha akiba ya Kanisa, na kutoa fursa za kuendeleza kazi ya Bwana zaidi ya kitu chochote ambacho tumekipitia. Yote yanajulikana na Bwana, na baada ya muda, tutaona malengo Yake yote matakatifu yakitimizwa.