Yesu Kristo ni Hazina
Dondoo
Nabii Yakobo wa Kitabu cha Mormoni alirejelea kuhusu kuchukulia kwa urahisi au kutothamini kile ambacho kiko karibu kama “kuangalia kupita alama” [Yakobo 4:14]. …
Tunatakiwa kujilinda dhidi ya tabia hii tusije kumkosa Yesu Kristo katika maisha yetu na kushindwa kutambua baraka nyingi anazotupatia. Tunamuhitaji Yeye. … Kama kimakosa tunafikiria kwamba kuna haja ya kitu fulani zaidi ya kile Yeye anachokitoa, tunakana au kudharau uwezo na nguvu Yeye anazoweza kuwa nazo kwenye maisha yetu. … Yesu Kristo ni hazina yetu.
Mwokozi ametupa njia nyingi za kuweza kwa dhati kufokasi Kwake, ikijumuisha fursa ya kila siku ya kutubu. Wakati mwingine, hatuthamini jinsi gani baraka hii iliyotolewa ilivyo kuu. …
… Baraka za thamani za sakramenti zinapatikana kwetu kila mara tunapohudhuria mkutano wa sakramenti. … Roho Mtakatifu hutubariki kupitia nguvu Yake ya utakaso ili kwamba daima tubakie na msamaha wa dhambi zetu, mwanzo hadi mwisho wa wiki. …
Wakati Roho Mtakatifu anapokuwa pamoja nasi, tutapata msukumo na kuongozwa kufanya na kushika maagano mengine kama yale ya hekaluni. Kwa kufanya hivyo uhusiano wetu na Mungu huwa wa kina. … Ari yetu ya kuhudhuria lazima angalau iwe ya nguvu wakati hekalu likiwa karibu au wakati likiwa mbali.
… Wakati tunapomuamini nabii wa Mungu hapa duniani leo na kutenda kulingana na ushauri wake, tutapata furaha, nasi pia tutaponywa. Hatuhitaji kuangalia mbali zaidi.