Historia ya Kanisa
Robert na Klabu ya Ice Lions


Robert na Klabu ya Ice Lions

Mnamo 2018 Robert Opiyo, Mtakatifu wa Siku za Mwisho alikuwa mshiriki kwenye klabu ya mpira wa kwenye uwanja wa barafu ya Afrika Mashariki na Kati, Kenya Ice Lions. Wachezaji wa mpira wa uwanja wa barafu walikuwa si zaidi ya 30 huko Kenya, na 17 kati yao (15 wanaume na 2 wanawake) walikuwa washiriki rasmi wa timu ya Ice Lions.

Robert alitumia ujuzi aliojifunza akiwa misioni huko Melbourne, Australia, kusaidia kuratibu mafunzo ya timu na kusimamia akaunti za mitandao ya kijamii ya timu.

Timu ya Ice Lions ilifanyia mazoezi kwenye uwanja wenye barafu wa hoteli ambao ulikuwa mbili ya tatu ya uwanja wa kawaida. Mnamo Oktoba 2018, timu ilidhaminiwa kusafiri kwenda Toronto, Kanada, kucheza dhidi ya timu mbili za kikanada.

Kabla ya mchezo wa kwanza huko Toronto, walifanya mazoezi bila ya mlinda mlango. Kwenye usahili huko Toronto, kapteni wa Ice Lions alifafanua: “Hatukuwa na kifaa cha mlinda mlango, na hakuna ambaye angetaka kuwa kwenye hatari hiyo ya kuwa mlinda mlango bila kifaa husika. Hivyo, tulichofanya ilikuwa ni kuweka mwanasesere na tulikuwa tukimweka katikati ya lango na ili kufunga ulitakiwa mpira uguse juu ya tumbo la mwanasesere.”

Robert ana ndoto ya kufikia Olimpiki siku zijazo lakini pia anaridhika kuwa sehemu ya juhudi hizi anzilishi. “Taratibu watu wengi wanasikia kuhusu nia yetu na wanataka kutusaidia kuifikia,” alisema. “Ninashukuru kuwa sehemu ambayo inaweka msingi kwa ajili ya vizazi vya baadae.”