Historia ya Kanisa
Kenya: Mpangilio wa Matukio ya Kanisa


Kenya: Mpangilio wa Matukio ya Kanisa

1960s • Nairobi, KenyaKundi dogo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ambao ni wataalam toka Marekani walikutana kwenye nyumba ya kila mmoja wao.

Juni 8, 1978 • Jijini Salt Lake, Utah, MarekaniUrais wa Kwanza ulitangaza ufunuo kufikisha ukuhani kwa waumini wote wanaume wastahiki.

Oktoba 21, 1979 • KenyaEbisiba na Elizaphan Osaka na watoto wao wakubwa wawili, Margaret na Jairo, walikuwa Wakenya wa kwanza kubatizwa kwenye nchi yao.

Septemba 1980 • NairobiWamisionari wa kwanza wanandoa walifika Kenya.

1985 • KenyaSerikali ya Kenya haikuwa kisheria imelitambua Kanisa, hivyo waumini wa Kanisa wangeweza pekee kukutana kwa siri katika makundi madogo madogo. Patrick Kapsandoy, muumini mwenyeji, aliliwakilisha Kanisa katika majaribio ya kulisajili serikalini.

1986 • Chyulu, KenyaTawi lilianzishwa, na mikutano ilifanyika nyumbani kwa Gideon Kasue.

1983 • ChyuluWamisionari wawili wazawa wa Kenya, kaka Nickson na Benson Kasue, waliitwa kwenda misioni. Nickson alipangiwa kutumikia kwenye Misioni ya Washington D.C, na Benson alitumikia kwenye misioni ya California Los Angeles.

1986–89 • Ngorika, KenyaKwa kutumia fedha zilizotokana na mfungo maalum mnamo Novemba 1985, Kanisa lilichangia dola za kimarekani 300,000 ili kuwasaidia wakenya kujenga mfumo wa maji huko Ngorika.

July 1989 • KenyaKanisa kwa hiari liliwaondoa wamisionari wanandoa kutoka nchini mpaka pale utambuzi rasmi ungeweza kupatikana kutoka serikali ya Kenya. Joseph W. Sitati muumini mwenyeji alisimikwa kuwa mzee kiongozi kwa ajili ya Kanisa huko Kenya.

Picha
Kundi la wanaume wakiwa wamesimama ofisini

Februari 25, 1991 • Kenya

Baada ya miaka 11 ya juhudi za kusajili, ikijumuisha mfungo endelevu wa kila wiki kwa zamu uliokuwa ukifanywa na waumini saba kwenye mwisho wa mwaka mmoja na nusu, serikali ya Kenya ililipatia Kanisa utambuzi rasmi.

Septemba 24, 1991 • NairobiWilaya ya Nairobi Kenya iliundwa, Joseph Sitati akiwa kama rais.

October 24, 1991 • NairobiMzee James E. Faust wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliiweka wakfu Kenya kwa ajili ya kuhubiriwa injili. Zaidi ya waumini wa Kanisa 100 walikusanyika nje ya nyumba ya mkutano ya Nairobi kwa ajili ya hafla ya jioni.

October 1991 • KenyaWamisionari 10 walifika kutoka Afrika ya Magharibi.

February 22, 1992 • NairobiDarasa la mafunzo ya injili kwa vijana lilianza kwenye Tawi la Kibera, likiwa na wanafunzi 16. Mwaka mmoja baadae, kulikuwa na seminari 16 na vyuo 10 kwenye misioni.

Julai 1992 • ChyuluWaumini wa Kanisa, wakiongozwa na Julius Kasue, rais wa Tawi la Chyulu, wanashiriki kwenye kutoa msaada wakati wa baa la njaa kwa kugawa mahindi na maharage kwa waumini wa Kanisa na majirani, vilevile kusaidia kuanzisha programu ya ustawi wa kijamii kupitia kilimo kupitia ardhi, pampu za maji na matanki ya kutunza maji.

Disemba 15, 1992 • KenyaWilaya ya Chyulu Kenya iliundwa, Julius Kauli Kasue akiwa kama rais.

1993• KenyaMmisionari wa kike wa kwanza kutoka Kenya, Tiatilis Mutono alianza misioni yake.

Februari 1993 • KenyaKanisa lilitoa kilogramu 106,600 za chakula kwa ajili ya wakimbizi huko Kenya karibu na mpaka wa Somalia.

Agosti 1994 • NairobiNyumba ya kukusanyika ya kwanza kujengwa Afrika Mashariki ilikuwa chumba cha ibada kwa ajili ya Tawi la Langata.

Februari 1996 • KenyaKutokana na tuhuma kadhaa zisizo za kweli kuhusu Kanisa, misioni ilipewa saa 48 kuwaondoa wamisonari wote ambao si wazawa kutoka Kenya. Wamisonari thelathini na sita walilazimishwa kuondoka, wakiachwa 14 pekee vilevile wamisionari wanandoa.

Februari 17, 1998 • NairobiKaribu waumini 900 kutoka nchi tano za Afrika walikusanyika kumsikiliza Rais wa Kanisa Gordon B. Hinckley akiongea wakati alipotembelea Nairobi.

Oktoba 1998 • Jijini Salt LakeWatakatifu wa Siku za Mwisho Wakenya walisafiri kwenda Jijini Salt Lake kutafsiri ibada za Hekaluni kwa Kiswahili.

Machi 7, 1999 • KenyaWaumini wa kanisa walifanya mfungo maalum kwa ajili ya urudishwaji wa wamisionari wa kigeni nchini, bila vikwazo. Kwa wakati huo, waliruhusiwa kuingia nchini kwa viza za wageni.

Februari 22, 2000 • NairobiSheri L. Dew wa Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi na Sharon G. Larsen wa Urais Mkuu wa Wasichana walitoa mafunzo kwa viongozi wa wilaya na matawi wa Muungano wa Usaidizi na Wasichana na kwa washauri kwenye ukuhani.

2000 • Jijini Salt LakeKitabu cha Mormoni kilichapishwa katika lugha ya Kiswahili.

Septemba 9, 2001 • NairobiRobert C. Oaks na Steven E. Snow wa Urais wa Eneo la Kusini mwa Afrika waliunda kigingi cha Nairobi Kenya, kutoka kwenye Wilaya ya Nairobi Kenya. Kilikuwa ni kigingi cha kwanza Afrika Mashariki, na Joseph W. Sitati alikuwa rais.

Aprili 3, 2004 • AfricaJoseph Sitati aliitwa kuwa Sabini wa Eneo, wa kwanza kutoka Kenya au Afrika Mashariki. Mnamo 2007, alikuwa rais wa misioni ya Nigeria Calabar. Mnamo 2009, alikubaliwa kama Sabini Mwenye Mamlaka.

2005• KenyaVijana wa kiume na wa kike walianza kutumia programu ya Mfuko Endelevu wa Elimu kuendeleza elimu yao. Kwa miaka mingi, mamia ya Watakatifu wa Siku za Mwisho vijana walishiriki.

Januari 4, 2009 • Jijini Salt LakeTawi la Parleys Creek lilianzishwa kama sehemu ya kigingi cha Salt Lake Sugar House huko Utah, na Amram Musungu kama rais (Mkenya wa kwanza kuimba kwenye kwaya ya Tabernacle). Tawi linahudumia wale ambao wanaongea Kiswahili na wengine wenye lahaja za Kiafrika.

Mei 2010 • KenyaWaumini walikusanyika kwa ajili ya ibada na mafunzo ya viongozi wakitembelewa na viongozi Julie B. Beck Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi na Elaine S. Dalton Rais Mkuu wa Wasichana.

Aprili 24, 2011 • Eldoret, KenyaWilaya ya Eldoret Kenya iliundwa.

Agosti 16, 2014 • KenyaZaidi ya waumini wa Kanisa 400 na marafiki walishiriki kwenye shughuli ya Mikono Saidizi kwenye maeneo ya Mombasa na Chyulu. Shughuli zilijumuisha usafishaji wa mitaa, upandaji wa maua na miti, na usawazishaji wa barabara, ukivutia waandishi wa redio na televisheni za ndani ya nchi.

Oktoba 12, 2014 • Kilungu Hills, KenyaWilaya ya Kilungu Hills Kenya iliundwa.

Oktoba 25, 2015 • Mombasa, KenyaWilaya ya Mombasa Kenya iliundwa, Jarvy Moses Msafiri akiwa kama rais.

Aprili 2, 2017 • Jijini Salt LakeKanisa lilitangaza mpango wa kujenga hekalu huko Nairobi.

Februari 10, 2019 • Kitale, KenyaWilaya ya Kitale Kenya iliundwa, Anthony W. Matende akiwa kama rais. Alice Khisa Juma alikubali wito kutumikia kama rais wa Wilaya wa Muungano wa Usaidizi.

Juni 16, 2019 • Kisumu, KenyaWiaya ya Kisumu Kenya iliundwa, Kennedy A. Okila akiwa kama rais.

Chapisha