Historia ya Kanisa
Kenya: Ufupisho


Picha
ramani ya Kenya

Historia ya Kanisa huko

Kenya

Ufupisho

Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1960, Watakatifu wa Siku za Mwisho ambao walikuwa wataalam wa Kimarekani huko Kenya walifanya mikutano ya Kanisa nyumbani kwao. Hii iliendelea kwa takribani miaka 20, kwa Watakatifu mara chache kuwaalika marafiki zao na majirani kwenye mikutano, kushiriki machapisho ya Kanisa na kufundisha injili katika njia za siri na ndogo. Kipindi hicho, wakenya waliokuwa wakiishi nje ya nchi pia walikutana na Watakatifu wa Siku za Mwisho, na wachache walibatizwa.

Mnamo 1979, mwaka mmoja baada ya ufunuo wa kufikisha baraka timilifu za injili ya urejesho kwa watu wa Afrika, Wakenya wengi walianza kuchunguza Kanisa. Wengi ambao waliikumbatia injili ya urejesho walitaka kubatizwa. Hatahivyo, baadhi ya mamlaka za maeneo husika zilikuwa pinzani kuhusu kundi la dini mpya na wasingekubali Kanisa kufanya ibada. Kwa miaka mingi, Watakatifu hawa kwa uvumilivu waliendelea na imani yao kwa siri, walifunga na kusali kwa matumaini kwamba watatambuliwa, na kwa bidii waliwasihi maafisa. Hatimaye, mnamo Februari 1991, Kanisa lilitambuliwa. Kupitia jaribu hili, Watakatifu wa Kenya walipata “utukufu katika mateso na sababu ya “kufurahi wakitazamia tumaini la utukufu wa Mungu” (ona Warumi 5:1–5).

Baada ya kupata utambuzi, Kanisa lilikuwa kwa haraka. Matawi matatu huko eneo la Nairobi mwaka 1991 punde yaliongezeka kuwa mengi, wakati waumini walipowaalika marafiki zao na majirani kujiunga nao, na waongofu wapya walibatizwa kote nchini. Mnamo Septemba 2001, Kigingi cha Nairobi Kenya kiliundwa.

Kupitia huduma yenye uaminifu, Watakatifu Wakenya wamefanya kazi pamoja na majirani kujenga jamii, wakiongeza ufikiaji wa rasilimali na kushriki mwanga wa injili.

Ujenzi wa Hekalu la Nairobi Kenya ulitangazwa wakati wa mkutano mkuu wa Aprili 2017.

Chapisha