Rwanda: Kronolojia,” Historia za Ulimwengu: Rwanda (2020)
“Rwanda: Kronolojia,” Historia za Ulimwengu: Rwanda
Rwanda: Kronolojia
-
Mapema mnamo 1990 • RwandaHabimana Theoneste, ambaye alikuwa amefundishwa na wamisionari huko Lyon, Ufaransa, alirudi Rwanda na kuanza kushiriki injili.
-
Julai 28, 1994 • RwandaKufuatia mauaji ya kimbari ya Rwanda, Kanisa lilituma msaada wa thamani ya $760,000 Dola za Kimarekani kwa Rwanda, ikiwa ni pamoja na chakula, vifaa vya matibabu, nguo, blanketi na vifaa vya usafi.
-
2005 • Kigali, RwandaJohn Jackson, mfanyakazi wa ubalozi wa Marekani, alipanga mikutano ya washiriki wa Kanisa nyumbani kwake. Mikutano ilihamia nyumbani kwa Nelson Samuel miaka kadhaa baadaye.
-
16 Machi 2008 • KigaliTawi la Kigali liliundwa na Eric K. Hyde kama rais wa kwanza wa tawi.
-
16 Agosti 2008 • KigaliIbada ya kwanza ya ubatizo ilifanyika katika Ziwa Muhazi.
-
2009 • KigaliUongozi wa kwanza wa Msingi uliundwa na Agathe Rumanyika kama rais.
-
Machi 2010 • KigaliBrent na Cheri Andrus, wamisionari wa kwanza waliotumwa Rwanda, walifika Kigali.
-
2011 • RwandaKanisa lilifadhili miradi ya kibinadamu kote nchini, ikijumuisha maji safi, usafi wa mazingira, vifaa vya matibabu na mafunzo, huduma ya macho na mafunzo ya uokozi wa watoto wachanga.
-
2011 • KigaliEmmanuel Rukundo aliitwa kuongoza programu ya Kanisa ya kusaidia kupunguza ukosefu wa ajira nchini Rwanda.
-
Mei 2011 • KigaliMadarasa ya kwanza ya chuo yalifanyika huku Godfrey Musaazi akiwa kama mwalimu.
-
Septemba 2011 • KigaliKwa msaada wa waumini wa ndani, Kanisa lilianza kutafsiri nyenzo katika lugha ya Kinyarwanda.
-
Oktoba 2011 • KigaliJackson Ndayambaje akawa mmisionari wa kwanza aliyeitwa kutoka Rwanda. Alihudumu katika Misheni ya Johannesburg ya Afrika Kusini.
-
Novemba 2011 • KigaliIli kutii marufuku ya serikali, waumini waliagizwa wasifanye mikutano katika jumba la mikutano bali wafanye ibada ya familia katika nyumba zao. Mikutano ya kawaida ilianza tena Julai 2012.
-
13 Agosti 2012 • KigaliTawi la Kigali lilifanya Siku ya Mikono Saidizi na kuwaalika wananchi wazee kwenye nyumba ya mikutano, ambapo walipokea miwani za kusomea, mikongojo na viti vya magurudumu.
-
24 Oktoba 2013 • RwandaKanisa lilipokea cheti cha muda cha kufanya kazi nchini Rwanda wakati wakiendelea na maombi ya kutambuliwa kisheria.
-
1 Septemba 2014 • KigaliTawi la Tatu la Kigali liliendesha mradi wa Mikono Saidizi, kuwapa wanajamii miwani 265
-
26 Machi 2017 • KigaliWilaya ya Kigali Rwanda iliundwa ikiwa na matawi matatu huko Kagali na Joshua Owino Opar kama rais wa wilaya. Tawi la nne lilianzishwa Kigali mnamo mwaka 2019.
-
24 Agosti 2018 • KigaliWatakatifu nchini Rwanda walikusanyika kuadhimisha siku ya kila mwaka ya All-Africa Mormon Helping Hands kwa kufanya usafi wa mazingira ya jumuiya yao.
-
Septemba 13–15, 2018 • KigaliMzee Joseph Sitati, Sabini Mkuu mwenye Mamlaka, alitoa hotuba muhimu kuhusu uhuru wa kidini kwa ajili ya Kongamano la tatu la All Africa Religious Liberty Congress nchini Rwanda.