Historia ya Kanisa
Rwanda: Maelezo ya Jumla


“Rwanda: Maelezo ya Jumla,” Historia za Ulimwengu: Rwanda (2020)

“Rwanda: Maelezo ya Jumla,” Historia za Ulimwengu: Rwanda

Picha
ramani ya Rwanda

Historia Fupi ya Kanisa huko

Rwanda

Maelezo ya Jumla

Katika miaka ya 1980 na 1990 rekodi za Kanisa ziliorodhesha hadi waumini saba wa Kanisa wanaoishi Rwanda, lakini Watakatifu wa Siku za Mwisho walikuwa wakiishi bila kuwa na Kanisa nchini humo. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 hali hiyo ilibadilika kwani waumini walianza kukutana mara kwa mara mjini Kigali. Nelson na Sapna Samuel, wamisionari wawili waliorudi kutoka Bangalore, India, waliokuwa wamehamia Rwanda, walifanya mikutano ya awali ya kikundi. Wakati tawi la kwanza lilipoundwa mwaka 2008, wengi wa waumini—ikiwa ni pamoja na Fabien Hatangimbabazi, Yvonne Martin, Jean Marie na Agathe Rumanyika, na Ruth Opar—walikuwa Wanyarwanda ambao walikuwa wamejiunga na Kanisa katika nchi zingine na kurudi katika nchi yao ya asili.

Ingawa serikali ya Rwanda ilisitisha usajili wa makanisa mapya mwaka huo huo, waumini wa Kanisa na viongozi walisonga mbele kwa imani wakijiandaa kwa siku zijazo. Mnamo mwaka 2009 Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliweka wakfu Rwanda kwa ajili ya kuhubiri injili, na mwaka 2010 nchi hiyo ilikubali wamisionari wa kusimamia misaada ya kibinadamu. Katika miaka michache iliyofuata, mipango mingi zaidi ya Kanisa ilianzishwa, tafsiri ya maandiko ya Kanisa kwa Kinyarwanda ilianza, na Jackson Ndayambaje akawa mmisionari wa kwanza aliyeitwa kutoka Rwanda. Kanisa hatimaye lilipata kutambuliwa na serikali mnamo mwaka 2013. Kufikia mwaka 2019 kulikuwa na matawi manne katika Wilaya ya Kigali Rwanda.

Vidokezo

  • Jina Rasmi: Jamhuri ya Rwanda/Repubulika y’u Rwanda/République du Rwanda/Jamhuri ya Rwanda

  • Mji mkuu: Kigali

  • Jiji Kubwa: Kigali

  • Lugha Rasmi: Kingereza, Kinyarwanda, Kifaransa na Kiswahili

  • Eneo la nchi: 26,338 km2 (10,169 mi2)

  • Eneo la Kanisa: Kusini Mashariki mwa Afrika

  • Misheni: 1 (Sehemu ya Misheni ya Uganda Kampala)

  • Mikusanyiko: 4

Chapisha