Historia ya Kanisa
Ameniachia Amani


“Ameniachia Amani,” Historia za Ulimwengu: Rwanda (2020)

“Ameniachia Amani,” Historia za Ulimwengu: Rwanda

Ameniachia Amani

Kati ya mwaka 1990 na 1994 Rwanda ilisambaratishwa na vita vya kikabila vilivyosababisha mamia ya maelfu ya mauaji kati ya Aprili na Julai 1994. Matukio haya ya kutisha yaliathiri maisha ya karibu kila mtu nchini. Wakati huu, Agnes Twagiramariya mwenye umri wa miaka 11 alishuhudia jirani akiwaua wazazi wake, ndugu zake wanne na watu wengi wa familia yake. Kwa miaka 12 iliyofuata, Agnes alipambana na uchungu wa vifo vya watu wa familia yake. “Kupoteza familia yangu, hasa wazazi wangu,” Agnes alieleza, “ni jambo baya sana maishani mwangu na lilikuwa limesababisha tabia fulani kama vile kuwa peke yangu, kuchukia watu, kutokuwa na furaha kwa muda fulani na moyo uliovunjika.”

Mnamo mwaka 2006, alipokuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Kigali, Agnes alihamia kwenye nyumba pamoja na binamu yake Yvonne, ambaye alikuwa muumini wa Kanisa. Walipokuwa wakiishi pamoja, Yvonne alianza kushiriki video za Kanisa kuhusu Yesu Kristo na Urejesho wa injili Yake kupitia Joseph Smith. Hatimaye, Yvonne alimwalika Agnes kusoma Kitabu cha Mormoni na kuhudhuria mikutano ya Kanisa pamoja naye. “Jambo la kwanza lililonivutia ni mafundisho,” Agnes alisema baadaye. “Jambo lingine ni tabia ya baadhi ya waumini wa Kanisa; wanaenenda kama watoto wa Bwana.”

Agnes alibatizwa Juni 13, 2010. Muda mfupi baadaaye aliitwa kufundisha watoto katika darasa la Msingi linalokua haraka la Tawi la Kigali. Wakati furaha yake katika injili ilikua, hata hivyo, Agnes bado alijiuliza kama angeiona familia yake tena, ikiwa bado walikuwa na uchungu, na maisha baada ya kifo yalikuwaje kwao. Mnamo mwaka 2012 Agnes alisafiri hadi Johannesburg, Afrika Kusini, kuhudhuria hekalu kwa mara ya kwanza—na kuunganishwa kwa wazazi na ndugu zake waliokufa kwa milele yote.

Picha
Agnes na kibali chake

Agnes Twagiramariya akiwa na kibali chake cha kwanza cha hekaluni, 2012.

Ingawa kifo daima kitakuwa ni sehemu ya maisha yake, Agnes alipata uponyaji kupitia injili ya urejesho. “Nimeanza kutabasamu na kuzungumza tena,” Agnes alisema. “Nilifanya mabadiliko katika maisha yangu, na ninaweza kuwa na furaha kwa muda mrefu. Nina amani na moyo wa kusamehe.”

“Ninaweza kuwasamehe wale wauaji wa familia yangu,” alisema. “Kwangu mimi, msamaha ni zawadi ambayo nimeipokea baada ya kuielewa injili.” Kristo, ambaye alikuwa ameteseka katika nyumba ya marafiki zake (ona Zakaria 13:6), alijua jinsi ya kumfikia katika mahangaiko yake. “Kanisa la kweli la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho likawa daraja langu la kuacha maisha ya kukanganyikiwa hadi maisha ya ukweli, kutoka kwenye huzuni hadi furaha ya kweli, kutoka kwenye majonzi hadi shangwe, kutoka kwenye hasira hadi msamaha,” alisema. “Ninashuhudia kwamba Mwokozi wetu Yesu Kristo anatupenda, na anataka tuwe na furaha na tuwe na shangwe ya kweli.”

Chapisha