2021
Chapisho Jipya kwa ajili ya Kanisa la Ulimwengu Wote
Januari 2021


Karibu kwenye Toleo Hili

Ni Chapisho Jipya kwa ajili ya Kanisa Ulimwenguni Kote

Wapendwa akina kaka na dada zetu,

Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kupatikana katika nchi nyingi kote ulimwenguni. Ingawa tunaongea lugha nyingi, tumeungana katika jitihada zetu katika kumfuata Mwokozi, na tunafurahia katika kujua kwamba sisi sote ni watoto wa Mungu.

Tangu mwanzoni mwa siku za urejesho wa Kanisa, machapisho kama magazeti ya Kanisa yamekuwa yakiwasaidia waumini katika juhudi zao za kujifunza, kuishi, na kushirikiana na wengine injili ya Yesu Kristo. Ujumbe wenye kuvutia umewasaidia waumini kuwa na uhusiano na viongozi wa Kanisa na kila mmoja wao. Pamoja na kutamani kutoa baraka hizi kwa watoto wa Mungu wengi zaidi, tumefarijika kushiriki toleo hili la kwanza la Liahona mpya pamoja nawe.

Mabadiliko mengine kwenye magazeti ya Kanisa yanajumuisha machapisho mapya kwa ajili ya watoto na vijana ulimwenguni kote. Kila moja ya magazeti haya— Liahona, Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana na Rafiki—yatafanya kazi pamoja na Njoo, Unifuate nyenzo ya kujifunza maandiko ambayo inasaidia kujifunza injili majumbani mwenu. Magazeti haya pia yatakuwa yakipatikana katika njia za kidigitali

Madhumuni ya magazeti ya Kanisa yanabaki vile vile: ni kuwasaidia watoto wa Mungu kuongolewa zaidi katika Mwokozi wao, Yesu Kristo. Tunashukuru sana kwa kutamani kwako kujifunza na kuishi injili, na tunajua kwamba magazeti haya yatakusaidia katika jitihada zako hizo.

Wako waaminifu,

Urais wa Kwanza

Chapisha