Misingi ya Injili
Mungu Anazungumza Nasi Leo
Baba wa Mbinguni anataka kutusaidia. Je, tunamsikiliza?
Miaka 200 iliyoipita, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtokea kijana aliyeitwa Joseph Smith. Ono hili la Kwanza linatufundisha ukweli wa muhimu. Yesu kwa mara nyingine analiongoza Kanisa duniani. Manabii wapo leo kama nyakati za kale. Na Mungu anamjua kila mmoja wetu kwa jina na anasikiliza maombi yetu. Tunabarikiwa wakati tunapojaribu kuisikiliza sauti Yake kila siku.
Ufunuo ni Nini?
Wakati Mungu anapoongea na watoto Wake, huo unaitwa “ufunuo.” Kuna aina tofauti za ufunuo
Ufunuo binafsi ni wakati Mungu anapoongea na sisi mmoja mmoja kupitia Roho Mtakatifu. Anaweza kutufariji na kutuongoza.
Tunaweza pia kupokea ufunuo kuhusu jinsi ya kuwasaidia wale walioitwa kuongoza. Kwa mfano, wazazi wanaweza kupokea ufunuo kuhusu familia zao, na askofu akapokea ufunuo kuhusu kata yake.
Ni nabii pekee anaweza kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa zima, lakini kila mmoja wetu anaweza kuomba kujua kama kile viongozi wetu wanatufundisha ni cha kweli.
Je, ni kwa jinsi gani Ninaweza Kualika Ufunuo?
Tunaweza kuzungumza na mpendwa, mwenye nguvu zote, mjua yote, Baba wa Mbinguni wakati wo wote kupitia maombi. Yeye anatutaka tumshukuru Yeye kwa ajili ya baraka, kuzungumza naye kuhusu maisha yetu, na kumwomba kwa ajili ya kile tunachohitaji. Kisha tunapaswa kuwa makini na mawazo na hisia ambazo huja kutoka kwa Roho Mtakatifu, ambaye ni kama mjumbe kutoka kwa Baba wa Mbinguni.
Je, Ufunuo Husikikaje?
Hakuna njia moja ya kuelezea ufunuo. Mungu huongea kwa kila mmoja wetu katika njia ambayo sisi tutaelewa (ona Mafundisho na Maagano 1:24). Watu wakati mwingine huona kupitia ndoto na maono. Lakini mara nyingi zaidi, Mungu huzungumza na sisi kupitia hisia tulivu kutoka kwa Roho Mtakatifu, kama vile mwako ndani ya moyo amani, au furaha.
Katika mafunzo ya mwezi huu ya Mafundisho na Maagano, tunasoma kuhusu Oliver Cowdery, ambaye alifundishwa kwamba ufunuo ungekuja akilini na moyoni mwake (ona Mafundisho na Maagano 8:2).
Je, Ipi ni Mifano ya Ufunuo katika Maandiko?
Hadithi nyingi za maandiko zinamwelezea Mungu akiongea na watu Wake:
-
Mungu alimwambia Nuhu jinsi ya kuisalimisha familia yake (ona Mwanzo 6:17–18).
-
Baba wa Mbinguni na Yesu walimfariji mfuasi aliyeitwa Stefano (ona Matendo 7:55).
-
Ufunuo ulimsaidia Nefi kushika amri (ona 1 Nefii 4:6).
-
Wakati maandiko mengine yanatokana na maandiko ya kale, Mafundisho na Maagano kinatengenezwa na ufunuo wa wakati wa sasa. Mwaka huu tunayo fursa maalum ya kujifunza kitabu kilichojaa maneno ya moja kwa moja kutoka kwa Bwana.