Kwa ajili ya Wazazi
Mpango wa Wokovu na Kuamini katika Bwana
Wapendwa Wazazi,
Unaweza kutumia makala yafuatayo na picha zake kufungua majadiliano pamoja na familia yako na kuwasaidia kuelewa mada muhimu kama vile mpango wa wokovu na kuamini katika Bwana.
Mpango wa wokovu
Tumia “Misingi ya Injili” ukurasa wa 6 kuwafundisha watoto wako kuhusu mpango wa wokovu. Jadilini jinsi elimu ya mpango wa wokovu inavyokubariki wewe na familia yako. Fikiria kuwataka watoto wako kuchora picha za mpango wa wokovu na kumtaka kila mmoja wao kuelezea sehemu tofauti ya mpango huo.
Mtumaini Bwana
Soma uzoefu wa Kaka Milton Camargo kwenye ukurasa wa 21. Unapoujadili uzoefu na watoto wako, fikiria kuuliza: Ni kwa jinsi gani mmisionari alionesha imani yake katika Mungu? Jinsi gani unaonesha imani yako katika Bwana? Ni njia zipi ambazo umeweza kubarikiwa ulipomtumainia Bwana?
Kushughulikia Unyanyasaji
Tumia mawazo katika makala kwenye ukurasa wa 14 ili kujifunza jinsi ya kutambua unyanyasaji, kuuzuia, na wafunze watoto jinsi ya kujilinda wenyewe.