2022
February 1998: A Prophetic Promise of a Temple
Februari 2022


MWEZI HUU KATIKA HISTORIA YA KANISA

February 1998: A Prophetic Promise of a Temple

President Gordon B. Hinckley (1910–2008) aliwasili Nairobi, Kenya, mnamo Februari 12, 1998. Katika chumba kikubwa cha mkutano kwenye hoteli yake, aliwahutubia takribani waumini 900, ikiwa ni pamoja na baadhi ambao walikuwa wamesafiri kutoka Ethiopia, Somalia, Tanzania na Uganda. Katika maeneo ambayo watu hawakuweza kusafiri kufika Nairobi, walitoa fedha zao kuwatuma wawakilishi ambao wangeweza kuhudhuria, kurudi na kushiriki uzoefu pamoja nao.

“Kuna muunganiko wa upendo mkubwa ambao unakua miongoni mwa Watakatifu wa Mungu popote wanapoweza kupatikana,” alisema Rais Hinckley katika hotuba yake. “Ni jambo la kupendeza na la kustaajabisha. Ninapotazama nyuso zenu, ninaona muunganiko ule ule wa kujali wakati ninapotazama nyuso za watu katika Tabenako la Salt Lake. Sisi sote ni sehemu ya familia hii kubwa—Kanisa hili la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.”

Rais Hincley pia alisema: “Hakuna shaka yoyote katika akili yangu kwamba wakati utafika, ikiwa mtatembea katika imani na uvumilivu, kwamba hekalu litajengwa katika ardhi hii ili kukidhi mahitaji ya watu.Sasa, msitarajie hili ndani ya miaka michache, . . . lakini itakuwa hivyo.”

Mnamo Jumamosi, September 11, 2021, ardhi ilichimbwa kwa ajili ya hekalu la Nairobi Kenya. Mzee Joseph W. Sitati, Rais wa Eneo na muumini wa mwanzo wa Kanisa nchini Kenya, aliweka wakfu ardhi kwa ajili ya hekalu lililosubiriwa kwa muda mrefu. Unabii wa Rais Hinckley wa hekalu nchini Kenya sasa unakuwa uhalisia.