Mambo Muhimu ya Kitabu cha Maelezo
Msingi
Msingi ni programu nzuri ndani ya Kanisa kwa ajili ya watoto wa umri wa miezi 18 mpaka miaka 11. Hizi ni kanuni chache kutoka kwenye kitabu cha maelezo kuhusu Msingi:
Msingi—Wajibu wa Wazazi na Viongozi:
Wazazi wana jukumu la kuwafundisha watoto wao injili na kuwasaidia kuiishi (ona Mafundisho na Maagano 68:25–28). Viongozi na walimu wa Msingi wanawasaidia wazazi katika jukumu hili [kwa kuhakikisha] kwamba masomo ya Msingi, muda wa kuimba, na huduma na shughuli vinawasaidia watoto kufuata mfano wa Mwokozi.
Viongozi wanapaswa kuwa wepesi katika kuwatambua watoto ambao hawana msaada wa familia kwa ajili ya kuishi injili.1
Msingi—Muda wa Kuimba
Muda wa Kuimba huwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni na kujifunza kuhusu mpango Wake wa furaha. Wakati watoto wakiimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu hushuhudia kweli hizo. Maneno na muziki vitabakia katika akili na mioyo ya watoto maisha yao yote.
Muda wa kuimba ni tofauti na muda wa darasa. Wakati wa muda wa kuimba, watoto hujifunza wakati wanaposhiriki ipasavyo katika kuimba. Viongozi wa muziki wa Msingi hufundisha kanuni za injili, lakini hufanya hivyo mahususi kupitia muziki.2
Walimu wa—Msingi
Wakati watu wazima wakiwafundisha watoto katika mazingira ya Kanisa, angalau watu wazima wawili wanaowajibika wanapaswa kuwepo. Watu wazima wawili wanaweza kuwa wanawake wawili, wanaume wawili au wanandoa. Kama hili haliwezekani, viongozi wanapaswa kuunganisha madarasa. Viongozi na walimu wanapaswa kukamilisha mafunzo kwenye www.ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org.
Vijana hawapaswi kufundisha darasa la Msingi, wala kuwa kama mbadala.
Walimu wa Msingi na viongozi wa darasa la awali hukaa na watoto muda wote wa Msingi, ikiwa ni pamoja na muda wa kuimba na muda wa mabadiliko. Wakati wa kuimba, walimu hushiriki pamoja na madarasa yao. Walimu wanapaswa kubaki na watoto wadogo baada ya darasa la Msingi kumalizika mpaka pale mwanafamilia anapokuja kuwachukua.3