Njia Yangu ya Agano
Kupata Baraka Yako ya Patriaki
Liahona yako binafsi inakusubiri!
Rais Thomas S. Monson (1927–2018) alisema, “Baraka yako ya patriaki kiuhalisia imebeba sura kutoka kwenye kitabu chako cha milele cha mtu unayeweza kuwa. . . .
Inatakiwa kusomwa . . . kupendwa . . . kufuatwa. Ni Liahona binafsi kwako . . . itakuongoza kupita hatari za maisha. Itakuvusha kupita giza la usiku.
Ni pasiposti yako ya amani katika maisha haya.”1
Kila muumini mwenye kustahili, aliyebatizwa ana haki ya kupokea na anapaswa kupokea baraka ya patriaki. Baraka yako ni ya milele na takatifu. Ni ufunuo ulio wazi kwa ajili yako. Inafunua pia tamko la ukoo wako katika nyumba ya Israeli.
Baraka ya patriaki hutolewa na mtu mwenye ukuhani ambaye amechaguliwa mahususi na kutawazwa kwa ajili ya wito huu mtakatifu. Jukumu lake ni kumsikiliza Baba wa Mbinguni na kukupatia wewe baraka zako maalum unapokuwa tayari. Jukumu lako ni kujifunza kuhusu baraka za ukuhani, kuamua ni lini uko tayari kupokea baraka hii na kumtafuta Askofu wako au Rais wa Tawi ili kujua jinsi unavyoweza kupokea baraka yako binafsi.
Baraka za patriaki zinaweza kukusaidia na kukuongoza kila siku. Shuhuda hizi na zikupe msukumo:
Nilipokwenda kumfanyia mahojiano Amina Inot kutoka tawi la Kabiria, Nairobi Kenya Kigindi cha West, alitabasamu kwa utulivu na kusema, “Oo, nilikuwa punde tu nikiwaza kuhusu baraka yangu ya patriaki! Nilikuwa sipigi hatua kwenye baadhi ya malengo niliyoweka na nilikwenda kusoma baraka yangu ili niweze kurejesha fokasi yangu. Inanikumbusha mambo ambayo kiuhalisia ni muhimu zaidi kwenye maisha yangu. Ndipo niliweza kuona jinsi ya kusonga mbele. Nimeahidiwa baraka nyingi za kupendeza ikiwa nitafanya sehemu yangu. Baraka yangu ni kama Liahona kwangu.”
Heritier Bukasa kutoka Kata ya Mangungu, Kigingi cha Ngaliema huko Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, ana haya ya kusema: “Baada ya kupokea baraka yangu, ilikuwa mwongozo kwa ajili ya maisha yangu. Kidogo kidogo ninaona baraka na ahadi zikitimia kwenye maisha yangu na maisha ya familia yangu changa. Nina shukrani kubwa!”
Haron Kamto kutoka Kayole Kata ya 1st, Nairobi Kigindi cha Gast, Kenya, alipokea baraka yake akiwa mtu mzima mnamo 2012. “Nilipokea baraka yangu ya patriaki kama maandalizi yangu ya kwenda hekaluni. Nilimhisi Roho kwa nguvu wakati huo na kila mara ninapoisoma kwa ajili ya ushauri, faraja, msukumo, huruma na mwongozo, ninamhisi roho yuleyule kwa nguvu na ushahidi kwamba haya ni maneno na ahadi za Bwana kwangu.”
Baba wa Mbinguni anazo baraka binafsi kwa ajili ya kila mmoja wetu ili kutusaidia kupita kwenye maisha ya duniani. Ni juu yako wewe na mimi kujiandaa kwa ajili ya baraka na kuitafuta baraka hiyo. Kila mmoja wetu anahitaji Liahona yake binafsi.