Mtandaoni
Uchimbaji Msingi Sierra Leone
Waumini wa Sierra Leone walisherehekea tukio la kihistoria mnamo mwezi Machi. Msingi ulichimbwa kwa ajili ya hekalu la kwanza kujengwa kwenye ardhi ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Mzee Hugo E. Martinez, rais wa Kanisa wa Eneo la Magharibi mwa Afrika, alisema kwenye sala yake ya uwekaji wakfu: “Utubariki kama wafuasi wa Mwana Wako Yesu Kristo ili tuishi maisha yenye kukupendeza Wewe”.
“Tunaomba waumini wote wenye kustahili waingie kupitia milango yake ili wawatumikie wengine katika mada tukufu kuliko zote za injili ya milele ya Yesu Kristo, ambayo ni, ibada kwa niaba ya mababu zao. Tunaomba wahisi Roho wako na wapate maarifa na mwongozo wa kurejea kwenye uwepo Wako kama familia za milele.”
Bi Nabeela Farida Tunis, waziri wa eneo la magharibi la Sierra Leone, alikuwepo kwenye tukio hilo. Alisema, “Kwa dhati nalipongeza Kanisa hili na juhudi zake za kuleta hekalu kwenye nchi yetu. Mungu libariki Kanisa hili. Mungu utubariki sisi sote. Mungu ibariki Sierra Leone.”
Ona picha na kusoma zaidi kwenye: https://news-africa.churchofjesuschrist.org/