Yesu Kristo Ni Nguvu kwa Wazazi
Dondoo
Kama vile Yesu Kristo alivyo nguvu kwa vijana, Yesu Kristo pia ni nguvu kwa wazazi. …
Upendo wa mzazi kwa mtoto ni mojawapo ya kani zenye nguvu zaidi katika ulimwengu. Ni mojawapo ya mambo machache hapa duniani ambayo hakika yanaweza kuwa ya milele. …
Nguvu nyingine uliyonayo, kama mzazi, ni fursa ya kila siku ya ushawishi endelevu. …
Njia nyingine yenye nguvu ambayo Bwana huwasaidia wazazi ni kupitia karama ya ufunuo binafsi. Mungu anatamani sana kuimimina Roho Yake ili iwaongoze wazazi. …
Pengine msaada muhimu zaidi ambao Yesu Kristo huutoa kwa wazazi ni “badiliko kuu” la moyo. Ni muujiza ambao kila mmoja wetu anauhitaji. …
… Kupitia neema ya Mwokozi, kidogo kidogo, utakuza zaidi sifa ambazo wazazi wanazihitaji: upendo kwa Mungu na watoto Wake, subira, kutokuwa na ubinafsi, imani katika Kristo na ujasiri wa kufanya chaguzi za haki. …
Jitihada zetu za kujenga imani katika Yesu Kristo zimejikita nyumbani, zikifokasi kwa mtu binafsi. Na zinaungwa mkono na Kanisa. Licha ya kutoa maandiko matakatifu na maneno ya manabii, Kanisa la Mwokozi hutoa nyenzo nyingi ili kuwasaidia wazazi na watoto wafanye chaguzi za haki. …
Katika mpango wa Baba wa Mbinguni, uhusiano wa familia unakusudiwa kuwa wa milele. Hii ndiyo sababu, kama mzazi, hutakata tamaa, hata kama huoni fahari jinsi mambo yalivyokuwa huko nyuma.
Ukiwa na Yesu Kristo, Mponyaji Mkuu na Mwokozi, daima kunaweza kuwa na mwanzo mpya; Yeye daima hutoa tumaini.
Yesu Kristo ni nguvu kwa familia[,] vijana[, na] wazazi.