Kwa Usalama Wamekusanyika Nyumbani
Dondoo
Baba wa roho zetu anatamani watoto Wake kwa usalama wakusanyike nyumbani. …
Wale wanaoikubali injili ya Yesu Kristo bila ya kujali ukoo wao huwa sehemu ya Israeli waliokusanywa. Kwa kusanyiko hilo na utangazwaji na ujenzi wa mahekalu mengi, tuko katika nafasi ya kipekee ya kuwakusanya Israeli pande zote mbili za pazia kuliko hapo awali chini ya mpango wa Baba.
… Tunashukuru kwamba waumini na wamisionari sasa wanatanua jitihada za kukusanya Israeli. … Hata hivyo, dhamira yetu ya kupenda, kushiriki, na kualika inaweza kukuzwa zaidi.
Sehemu muhimu ya juhudi hii ya kimisionari ni kwa waumini binafsi kuwa mfano wa kielelezo cha nuru popote tunapoishi. Hatuwezi kuwa wa kubadilika badilika. Mfano wetu kama wa Kristo wa ukarimu, haki, furaha na upendo wa dhati kwa watu wote unaweza kutengeneza siyo tu bikoni ya nuru iongozayo kwa ajili yao bali pia uelewa kwamba kuna bandari ya salama katika ibada za wokovu na kuinuliwa za injili ya urejesho ya Yesu Kristo.
Tunaheshimu haki ya kujiamulia. Katika ulimwengu huu wa kidunia, wengi hawataitikia na kushiriki katika kukusanya Israeli. Lakini wengi watajitahidi, na Bwana anawategemea wale ambao wamepokea injili yake kwa haraka wajitahidi kuwa mfano wa bikoni ya nuru ambayo itawasaidia wengine waje kwa Mungu. Hii inaruhusu akina dada na akina kaka kote duniani kufurahia baraka kutoka mbinguni na ibada za injili ya Yesu Kristo ya urejesho na kwa usalama kukusanyika nyumbani.