Unajua Kwa Nini Mimi Kama Mkristo Ninaamini katika Kristo?
Dondoo
Jioni moja baada ya kazi, miaka kadhaa iliyopita, nilipanda basi langu la kawaida kuelekea New Jersey kutoka Jiji la New York. Mwanamke niliyetokea kukaa karibu naye aliona nilichokuwa nikiandika kwenye kompyuta yangu na akauliza, “Unaamini katika … Kristo?” …
… Watoto na vijana: Je, mnaweza baadaye kuwauliza wazazi wenu au kiongozi “Kwa nini Yesu alipaswa kufa?” …
Basi, nilimjulisha rafiki yangu mpya kwamba tuna roho pamoja na mwili na kwamba Mungu ni Baba wa roho zetu. … Kwa sababu Yeye anampenda mtu huyu na watoto Wake wote, alitutengenezea mpango wa kupokea mwili katika mfano wa mwili Wake uliotukuzwa, kuwa sehemu ya familia, na kurudi kwenye uwepo Wake wa upendo kufurahia uzima wa milele pamoja na familia zetu, kama afanyavyo kwa familia Yake. Lakini, nilisema, tungekabiliwa na vikwazo vikuu viwili katika ulimwengu huu ulioanguka: (1) kifo cha kimwili—kutenganishwa kwa miili yetu na roho zetu. Na (2) kifo cha kiroho—kutengwa kwetu na Mungu kwa sababu ya dhambi zetu, makosa, na dosari zetu kama wanadamu hututenganisha na uwepo Wake mtakatifu. …
Nilishuhudia kwa rafiki yangu, na ninashuhudia kwenu, kwamba Yesu Kristo ndiye [huyo] Mwokozi, kwamba Yeye ilibidi ateseke, afe, na afufuke tena—Upatanisho Wake usio na mwisho—ili kuwakomboa wanadamu wote kutokana na kifo cha kimwili na kutoa uzima wa milele kuishi na Mungu na familia zetu kwa wote watakaomfuata Yeye. …
Hatua zilizofunuliwa na Mungu ambazo tunapaswa kuchukua ili kumfuata Yesu na kupokea uzima wa milele zinaitwa mafundisho ya Kristo. Zinajumuisha “imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, toba, ubatizo [katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho], kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho.” [Hubiri Injili Yangu (2029), 63]