Hosana kwa Mungu Aliye Juu Sana
Dondoo
Takribani miaka 2,000 iliyopita Jumapili ya Matawi iliashiria kuanza kwa wiki ya mwisho ya huduma ya duniani ya Yesu Kristo. …
… Kuingia kwa Yesu Kristo kwa shangwe huko Yerusalemu na yale matukio ya wiki ambayo yalifuatia yanaonesha kwa mfano fundisho tunaloweza kutumia katika maisha yetu leo. …
Kwanza, unabii. …
Pili, wenza wa Roho Mtakatifu. …
Tatu, Ufuasi. …
Nne, Upatanisho wa Yesu Kristo. …
Wiki hiyo ya mwisho yenye matukio mengi katika huduma Yake ya duniani, Yesu Kristo alitoa mfano wa wanawali kumi. … Alitumia picha ya taa zilizowashwa, pamoja na akiba ya mafuta ili taa isizime, kama kielelezo cha utayari wa kuishi kwa njia Yake, kukumbatia ukweli Wake na kushiriki nuru Yake. …
Sisi, kama wale wanawali kumi, tunazo taa; lakini je, tunayo mafuta? Nina hofu kuna baadhi ambao wanaendelea tu na mafuta kidogo sana, wana kazi nyingi sana na mashinikizo ya kidunia. Mafuta huja kutokana na kuamini na kutendea kazi unabii na maneno ya manabii walio hai, hususani Rais Nelson, Washauri wake na Mitume Kumi na Wawili. Mafuta yanazijaza nafsi zetu tunaposikia na kumhisi Roho Mtakatifu na kufanyia kazi mwongozo huo wa kiungu. Mafuta yanamiminika katika mioyo yetu pale chaguzi zetu zinapoonesha tunampenda Bwana na tunapenda kile anachokipenda. Mafuta huja kutokana na kutubu na kutafuta uponyaji wa Upatanisho wa Yesu Kristo.