“Kaa Ndani Yangu, Nami Ndani Yako; Kwa Hiyo, Tembea Pamoja Nami”
Dondoo
“Bwana alimwambia Henoko: …
“… Nawe utakaa ndani Yangu, nami ndani yako; kwa hiyo tembea nami” [Musa 6:32, 34; msisitizo umeongezwa]. …
Bwana Yesu Kristo anatoa mwaliko kwa kila mmoja wetu kukaa ndani Yake. Lakini tunajifunzaje na hatimaye kuja kukaa ndani Yake?
Neno kaa huashiria kubakia hapo hapo au imara na kuvumilia pasipo kushawishika. … Hivyo, tunakaa ndani ya Kristo wakati tunapokuwa imara na wasiotingishika katika ibada zetu kwa Mkombozi na malengo Yake matakatifu, nyakati zote nzuri na mbaya.
Tunaanza kukaa ndani ya Bwana kwa kutumia uhuru wetu wa kimaadili wa kujichukulia juu yetu nira Yake kupitia maagano na ibada za injili ya urejesho. …
Tunakaa ndani yake kwa kusherehekea maneno ya Kristo. …
Tunakaa ndani Yake kwa kujiandaa kwa dhati katika kushiriki katika ibada ya sakramenti. …
Ahadi ya Mwokozi kwa wafuasi Wake ina pande mbili: kama tukikaa ndani Yake, Yeye atakaa ndani yetu. Lakini je, ni kweli inawezekana kwa Kristo kukaa ndani yako na kwangu—binafsi? Jibu kwa swali hili ni ndiyo!
… Muunganiko wa kimaagano tulionao pamoja na Baba yetu wa Mbinguni na Mwana Wake aliyefufuka na aliye hai ni chanzo kikuu cha mtazamo, tumaini, amani na shangwe ya kudumu …
Ninashuhudia ahadi ya Mwokozi ya kukaa ndani yetu ni ya kweli na inapatikana kwa kila muumini ashikaye maagano ya Kanisa Lake lililorejeshwa. …
Kama tutakaa ndani Yake, Yeye atakaa ndani yetu.