Mkutano Mkuu
Unajua Kwa Nini Mimi Kama Mkristo Ninaamini katika Kristo?
Mkutano mkuu wa Aprili 2023


Unajua Kwa Nini Mimi Kama Mkristo Ninaamini katika Kristo?

Yesu Kristo ilibidi kuteseka, kufa, na kufufuka tena ili kuwakomboa wanadamu wote kutokana na kifo cha kimwili na kutoa uzima wa milele kuishi na Mungu.

Jioni moja baada ya kazi, miaka kadhaa iliyopita, nilipanda basi langu la kawaida kuelekea New Jersey kutoka Jiji la New York. Mwanamke niliyetokea kukaa karibu naye aliona nilichokuwa nikiandika kwenye kompyuta yangu na akauliza, “Unaamini katika … Kristo?” Nikasema, “Ndiyo, ninaamini!” Tulipokuwa tukizungumza, nilijifunza kwamba alikuwa amehamia eneo hilo kutoka nchi yake nzuri ya Asia kufanya kazi katika sekta ya teknolojia ya habari ya New York yenye ushindani mkubwa.

Bila shaka, nilimuuliza, “Unajua Kwa Nini Mimi Kama Mkristo Ninaamini katika Kristo?” Yeye pia aliitikia kawaida na akanialika nimwambie. Lakini nilipokuwa nikienda kuongea, nilikuwa na mojawapo ya nyakati zile ambazo mawazo mengi huja akilini mwako. Hii ilikuwa mara ya kwanza ningeeleza “kwa nini” za Ukristo kwa mtu asiyeufahamu sana na mwenye akili nyingi. Nisingeweza kusema kwa urahisi, “Ninamfuata Yesu Kristo kwa sababu aliteseka kwa hiari na kufa kwa ajili ya dhambi zangu.” Angeweza kujiuliza, “Je, Yesu alipaswa kufa? Je, Mungu hangeweza tu kusamehe na kutusafisha dhambi zetu ikiwa tungemwomba Yeye afanye hivyo?”

Ni kwa jinsi gani ungejibu katika dakika chache? Ni kwa jinsi gani ungeelezea hili kwa rafiki? Watoto na vijana: Je, mnaweza baadaye kuwauliza wazazi wenu au kiongozi “Kwa nini Yesu alipaswa kufa?” Akina kaka na akina dada, nina ungamo la kufanya: licha ya yote niliyofikiri nilikuwa nikijua kuhusu mafundisho ya Kanisa, historia, sera, na kadhalika, jibu la swali hili kuu la imani yetu halikuja kwa urahisi. Siku hiyo niliamua kuangazia zaidi yale yaliyo muhimu zaidi kwa uzima wa milele.

Basi, nilimjulisha rafiki yangu mpya1 kwamba tuna roho pamoja na mwili na kwamba Mungu ni Baba wa roho zetu.2 Nilimwambia tuliishi na Baba yetu wa Mbinguni kabla ya kuzaliwa kwetu katika ulimwengu huu.3 Kwa sababu Yeye anampenda mtu huyu na watoto Wake wote, alitutengenezea mpango wa kupokea mwili katika mfano wa mwili Wake uliotukuzwa,4 kuwa sehemu ya familia,5 na kurudi kwenye uwepo Wake wa upendo kufurahia uzima wa milele pamoja na familia zetu,6 kama afanyavyo kwa familia Yake.7 Lakini, nilisema, tutakabiliwa na vikwazo vikuu viwili katika ulimwengu huu ulioanguka:8 (1) kifo cha kimwili—kutenganishwa kwa miili yetu na roho zetu. Bila shaka alijua kuwa sisi sote tutakufa. Na (2) kifo cha kiroho—kutengwa kwetu na Mungu kwa sababu ya dhambi zetu, makosa, na dosari zetu kama wanadamu hututenganisha na uwepo Wake mtakatifu.9 Alifahamu hili pia.

Nilimjulisha kuwa hili lilikuwa ni matokeo ya sheria ya haki. Sheria hii ya milele inadai kwamba adhabu ya milele ilipwe kwa kila moja ya dhambi zetu au ukiukaji wetu wa sheria za Mungu au ukweli, vinginevyo hatungeweza kurudi kuishi katika uwepo Wake mtakatifu.10 Ingekuwa si haki, na Mungu “hawezi kuzuia haki.”11 Alielewa hili lakini alielewa kwa urahisi kwamba Mungu pia ni mwenye rehema, upendo, na ana hamu ya kuleta uzima wetu wa milele.12 Nilimjulisha rafiki yangu kwamba tungekuwa na adui mjanja, mwenye nguvu—chanzo cha uovu na uongo—anayetupinga.13 Kwa hiyo, mtu mmoja aliye na nguvu nyingi zisizo na mwisho za kiungu za kushinda upinzani na vizuizi hivyo vyote angehitaji kutuokoa sisi.14

Kisha nilishiriki naye habari njema—“habari njema ya furaha kuu … kwa watu wote”15—kwamba “Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”16 Nilishuhudia kwa rafiki yangu, na ninashuhudia kwenu, kwamba Yesu Kristo ndiye huyo Mwokozi, kwamba Yeye ilibidi ateseke, afe, na afufuke tena—Upatanisho Wake usio na mwisho—ili kuwakomboa wanadamu wote kutokana na kifo cha kimwili17 na kutoa uzima wa milele kuishi na Mungu na familia zetu18 kwa wote watakao mfuata Yeye. Kitabu cha Mormoni kinatangaza, “Hivyo Mungu … alipata ushindi juu ya kifo; akimpa Mwana uwezo wa kufanya maombezi kwa ajili ya watoto wa watu … ; akijawa na [rehema na] huruma … ; baada ya kuzivunja kamba za mauti, na kujitwika juu yake uovu wao na makosa yao, akiwa amewakomboa, na kukidhi matakwa ya haki.”19

Hatua zilizofunuliwa na Mungu ambazo tunapaswa kuchukua ili kumfuata Yesu na kupokea uzima wa milele zinaitwa mafundisho ya Kristo. Zinajumuisha “imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, toba, ubatizo [katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho], kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho.”20 Nilishiriki hatua hizi kwa rafiki yangu, lakini hapa kuna baadhi ya njia ambazo manabii na mitume wamefundisha hivi majuzi jinsi mafundisho ya Kristo yanavyoweza kuwabariki watoto wote wa Mungu.

Rais Russell M. Nelson alielekeza: “Mafundisho safi ya Kristo yana nguvu. Hubadili maisha ya kila mmoja ambaye anaelewa na kutafuta kuyatekeleza katika maisha yake.”21

Mzee Dieter F. Uchtdorf alifundisha, “Kijitabu cha [mwongozo] cha Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana kwa ujasiri kinatangaza mafundisho ya … Kristo [na] kuwakaribisha [vijana] kufanya chaguzi kulingana na [mafundisho hayo].”22

Mzee Dale G. Renlund alifundisha, “Tunawaalika wamisionari wafanye kile wanachowataka wale wanaowafundisha wafanye: … kutumia mafundisho ya Kristo maishani mwao [na] kuingia na kubakia kwenye njia ya agano.”23

Mafundisho ya Kristo yanawatia nguvu wale wanaohangaika au kuhisi kuwa si wa Kanisa kwa sababu yanawasaidia, kama Mzee D. Todd Christofferson alivyosema, “kuthibitisha: Yesu Kristo alikufa kwa ajili yangu [na] ananipenda.”24

Wazazi, ikiwa mtoto wako anatatizika na kanuni ya injili au mafundisho ya kinabii, tafadhali pinga aina yoyote ya maneno maovu25 au harakati dhidi ya Kanisa au viongozi wake. Mbinu hizi ndogo, za kiulimwengu ziko chini yako na zinaweza kuwa zenye madhara kwenye uaminifu wa muda mrefu wa mtoto wako.26 Huzungumza vizuri sana juu yako kwamba ungemlinda au kumtetea mtoto wako wa thamani au kuonesha ishara za mshikamano naye. Lakini mimi na mke wangu, Jayne, tunajua kutokana na uzoefu binafsi kwamba kumfundisha mtoto wako mpendwa kwa nini sisi sote tunamhitaji sana Yesu Kristo na jinsi ya kutumia mafundisho Yake ndiko kutakakomuimarisha na kumponya. Hebu tuwaelekeze kwa Yesu, ambaye ndiye mwombezi wao wa kweli kwa Baba. Mtume Yohana alifundisha, “Yeyote … adumuye katika mafundisho ya Kristo … ana Baba na Mwana pia.” Kisha anatuonya tujihadhari na “mtu afikaye kwetu, na asilete mafundisho haya.”27

Mimi na Jayne hivi karibuni tulitembelea nyika ambapo Musa aliinua nyoka wa shaba mbele ya wana wa Israeli waliokuwa wakitangatanga. Bwana alikuwa ameahidi kuwaponya wote walioumwa na nyoka wenye sumu kama tu wangemtazama yule nyoka wa shaba.28 Kwa njia sawa na hiyo nabii wa Bwana hunyanyua mafundisho ya Kristo mbele yetu, “ili aweze kuponya mataifa.”29 Kwa kung’atwa au sumu au mapambano yoyote tunayopitia katika nyika hii ya duniani, tusiwe kama wale ambao, zamani na sasa, wangeweza kuponywa lakini, cha kusikitisha, “hawangetazama … kwa sababu hawakuamini kwamba wangeponywa.”30 Kitabu cha Mormoni kinathibitisha: “Tazama, … hii ndiyo njia; na hakuna njia nyingine wala jina lililotolewa chini ya mbingu ambalo mwanadamu anaweza kuokolewa katika ufalme wa Mungu. Na sasa, tazama, hili ndilo fundisho la Kristo.”31

Jioni hiyo huko New Jersey, kushiriki ni kwa nini tunamhitaji Yesu Kristo na mafundisho Yake kulinipa dada mpya, na yeye, kupata kaka mpya. Tulihisi ushuhuda wa amani, wenye kuthibitisha wa Roho Mtakatifu. Kwa kawaida kabisa, nilimwalika anipe namba yake ya simu kwa mawasiliano zaidi na kuendeleza mazungumzo na wamisionari wetu. Alifurahi kufanya hivyo.

“Kwa hiyo, ni ya umuhimu iliyoje kwa kufanya mambo haya yajulikane kwa wakazi wa dunia,” Kitabu cha Mormoni kinatangaza—kupenda, kushiriki na kualika32 tunapokusanya Israeli katika jumuiya zetu zote na familia—“ili wapate kujua kwamba hakuna mwenye mwili awezaye kukaa katika uwepo wa Mungu, isipokuwa tu kwa wema, na rehema, na neema [na mafundisho] ya Masiya Mtakatifu.”33 Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Nimechagua kutotangaza jina la rafiki yangu au kutumia jina la uwongo.

  2. Ona Warumi 8:15–17; Waebrania 12:9; Mafundisho na Maagano 88:15.

  3. Ona Yeremia 1:4–5; Mafundisho na Maagano 138:55–56; Ibrahimu 3:22–23, 26; Mwongozo katika Maandiko, “Premortal Life,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org; “Lesson 2: The Plan of Salvation,” Hubiri Injili Yangu (2019), 48.

  4. Ona “Somo la 2: Mpango wa Wokovu,” Hubiri injili Yangu, 48.

  5. Mpango mkamilifu wa Baba—unaoitwa mpango mkuu wa furaha, ni mpango wa wokovu, na ni mpango wa ukombozi, miongoni mwa marejeo mengine, umepangwa ili kwamba kila mtu anayekuja katika maisha ya duniani lazima afanye hivyo katika familia, na kila mtu ni sehemu ya familia. Bila shaka, si hali zote za kifamilia ambazo ni bora au zinapatana na maono ya upendo ya Baba yetu kwa watoto Wake wote, na baadhi ya hali ni za kusikitisha. Hata hivyo, tunapoishi mafundisho ya Kristo, Yesu Kristo hutusaidia kupokea baraka zote ambazo Baba anazo kwa watoto Wake kupitia mpango Wake wa huruma na jumuishi. Tazama pia maelezo ya mwisho 6.

  6. Moja ya ahadi kuu zaidi ambazo Mungu ametoa kwa watoto Wake pia ni zawadi kuu zaidi ya zawadi zake zote kwetu: kuinuliwa, au uzima wa milele, ambao ni kuishi milele “mbele ya Mungu na kuendelea kama familia” ( Mada za Injili, “Uzima wa Milele,” topics.ChurchofJesusChrist.org; ona pia Mafundisho na Maagano 14:7). “Familia” inajumuisha mume, mke, na watoto, pamoja na ndugu zetu wa ukoo walio hai na waliokufa wanaokubali na kuishi fundisho la Kristo. Tayari wanafamilia waliokufa katika ulimwengu wa roho ambao hawakuweza kukumbatia fundisho la Kristo katika maisha haya wanaweza kufanya hivyo katika ulimwengu wa roho kama ibada kama ubatizo, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na nyinginezo ambazo hutusaidia tuvumilie hadi mwisho zinafanywa kwa upendo na jamaa walio hai katika mahekalu ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Zaidi ya hayo, ahadi ya uzima wa milele sio tu kwa wale waliofunga ndoa katika maisha haya. Rais M. Russell Ballard alifundisha, “Maandiko na manabii wa siku za mwisho wanathibitisha kwamba kila mmoja aliye mwaminifu katika kushika maagano ya injili atapata fursa ya kuinuliwa” (“Tumaini katika Kristo,” Liahona, Mei 2021; msisitizo umeongezwa). Akiwanukuu Rais Russell M. Nelson na Rais Dallin H. Oaks, Rais Ballard aliendelea, “Wakati sahihi na namna ambayo baraka za kuinuliwa hutolewa haijafichuliwa yote, lakini hata hivyo zimehakikishwa” (”Tumaini katika Kristo,” 55; msisitizo umeongezwa.). Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Katika njia na wakati wa Bwana mwenyewe, hakuna baraka watakayonyimwa Watakatifu Wake waaminifu. Bwana atahukumu na kumlipa kila mtu kulingana na hamu ya moyoni pamoja na matendo yake” (”Celestial Marriage,” Liahona, Nov. 2008). Na Rais Oaks alieleza, “Mambo mengi muhimu zaidi yaliyopotoshwa ulimwenguni yatarekebishwa katika wakati wa Milenia, ambao ni wakati wa kutimiza yale yote ambayo hayajakamilika katika mpango mkuu wa furaha kwa watoto wote wanaostahili wa Baba yetu” (“Mpango Mkuu wa Wokovu,” Ensign, Nov. 1993, 75). Tazama pia maelezo ya mwisho 5.

  7. Tazama Mwongozo wa Maandiko, “Mpango wa Ukombozi,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org; ona pia Mada za Injili, “Mpango wa Wokovu,” topics.ChurchofJesusChrist.org, “Somo la 2: Mpango wa Wokovu,” Hubiri Injili Yangu, 48–50, 53.

  8. Ona “Somo la 2: Mpango wa Wokovu,” Hubiri Injili Yangu, 49.

  9. Ona “Somo la 2: Mpango wa Wokovu,” Hubiri Injili Yangu, 47–50.

  10. Ona “Somo la 2: Mpango wa Wokovu,” Hubiri Injili Yangu, 47–50.

  11. Mosia 15:27. Marejeleo ya haki ya milele au haki ya Mungu ni mengi katika maandiko, lakini ona hasa Alma 41:2–8 na Alma 42.

  12. Ona Alma 42:14; Musa 1:39.

  13. Ona “Somo la 2: Mpango wa Wokovu,” Hubiri Injili Yangu, 47–50.

  14. Ona Alma 34:9–13; ona pia Mosia 13:28, 34–35; 15:1–9; Alma 42:15.

  15. Luka 2:10.

  16. Yohana 3:16.

  17. Ona Helamani 14:15–17; Mormoni 9:12–14.

  18. Ona mwisho wa maelezo 5 na 6.

  19. Mosia 15:8–9.

  20. Madhumuni Yangu ni Nini kama Mmisionari?,” Hubiri Injili Yangu, 1; ona pia “Somo la 3: Injili ya Yesu Kristo,” Hubiri Injili Yangu, 63.

  21. Russell M. Nelson, “Ukweli Halisi, Mafundisho Halisi na Ufunuo Halisi,” Liahona, Nov. 2021, 6.

  22. Dieter F. Uchtdorf, “Yesu Kristo Ni Nguvu kwa Vijana,” Liahona, Nov. 2022; ona pia Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Uchaguzi (2022), 4.

  23. Dale G. Renlund, “Lifelong Conversion of Missionaries” (hotuba iliyotolewa katika warsha ya marais wa misheni wapya, Juni 25, 2021), 1, Church History Library, Salt Lake City.

  24. D. Todd Christofferson, “Mafundisho ya Kuwa Sehemu Ya,” Liahona, Nov. 2022; ona pia D. Todd Christofferson, “Furaha ya Watakatifu,” Liahona, Nov. 2019.

  25. Ona Yakobo 4:11; Mafundisho na Maagano 20:54; Mwongozo wa Maandiko, “Kuzungumza Uovu,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org.

  26. Ona Ahmad S. Corbitt, “Activism vs. Discipleship: Protecting the Valiant” (address given at the chaplains’ seminar, Oct. 2022), cdn.vox-cdn.com/uploads/chorus_asset/file/24159863/Brother_Corbitt_Chaplain_seminar.pdf; video: media2.ldscdn.org/assets/general-authority-features/2022-chaplain-training-seminar/2022-10-1000-activism-vs-discipleship-1080p-eng.mp4.

  27. 2 Yohana 1:9–10.

  28. Ona Hesabu 21:5–9.

  29. 2 Nefi 25:20.

  30. Alma 33:20

  31. 2 Nefi 31:21.

  32. Ona “2021 Broadcast: Principles of Love, Share, and Invite,” broadcasts.ChurchofJesusChrist.org; ona pia Gary E. Stevenson, “Penda, Shiriki, Alika,” Liahona, Mei 2022, 84–87.

  33. 2 Nefi 2:8.

Chapisha