Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu
Mkutano mkuu wa Aprili 2023


Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu

Akina kaka na dada, ni heshima kwangu kuwasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kukubali kwako katika njia iliyozoeleka popote ulipo. Kama kuna wale wanaopinga mapendekezo yoyote yaliyowasilishwa, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na M. Russell Ballard kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: M. Russell Ballard, Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, na Ulisses Soares.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka wa Sabini wafuatao watapumzishwa kutoka kwenye majukumu yao na kupewa hadhi ya heshima, kuanzia tarehe 1 Agosti 2023: Wazee Benjamín De Hoyos, Juan A. Uceda na Kazuhiko Yamashita.

Wale ambao wangependa kuonyesha shukrani kwa Ndugu hawa na kwa wake zao na familia zao kwa miaka mingi ya kujitolea katika utumishi duniani kote wanaweza kufanya hivyo kwa kuinua mkono juu.

Sabini wa Maeneo wafuatao wamepumzishwa kutoka katika majukumu yao, kuanzia sasa: J. Kimo Esplin and Alan T. Phillips.

Wale wanaopenda kuungana pamoja nasi katika kutoa shukrani kwa huduma yao nzuri, tafadhali waonyeshe.

Tunatambua kwa shukrani Sabini wa Maeneo wengine ambao watamaliza huduma yao mwaka huu na ambao majina yao yanaweza kupatikana katika tovuti ya Kanisa.

Wale wanaotaka kuungana pamoja nasi katika kuonyesha shukrani zetu kwa ndugu hawa kwa huduma yao isiyo ya kibinafsi wanaweza kuonyesha.

Kuanzia sasa, tunawapumzisha Kaka Ahmad S. Corbitt na Bradley Ray Wiilcox kutoka kutumikia kama Mshauri wa Kwanza na wapili, katika mpangilio huo kwenye Urais Mkuu wa Wavulana.

Wale wanaopenda kuonyesha shukrani kwa Ndugu hawa kwa huduma yao ya kujitolea, tafadhali onyesheni.

Tunaupumzisha Urais Mkuu wa Wasichana ifikapo Agosti 1, 2023, kama ifuatavyo: Bonnie H. Cordon kama Rais, Michelle D. Craig kama Mshauri wa Kwanza na Rebecca L. Craven kama Mshauri wa Pili.

Wale wote wanaopenda kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa akina dada hawa kwa huduma yao ya kusifika, tafadhali onyesheni.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini Wakuu wenye Mamlaka: Ahmad S. Corbitt, Robert M. Daines, J. Kimo Esplin, Christophe G. Giraud-Carrier, and Alan T. Phillips.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Wale wanaopinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Tunawapeni taarifa kwamba Sabini wa Maeneo wapya 61 walikubaliwa wakati wa mkutano mkutano mkuu wa uongozi uliofanyika Alhamisi, Machi 30, na baadae kutangazwa kwenye tovuti ya Kanisa.

Tunawaalikeni muwakubali ndugu hawa katika majukumu yao mapya.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Urais Mkuu mpya wa Wasichana, utakaoanza kazi Agosti 1, 2023: Emily Belle Freeman kama Rais, Tamar Wood Runia kama Mshauri wa Kwanza, na Andrea Muñoz Spannaus kama Mshauri wa Pili.

Wale wanaounga mkono wanaweza kuonesha.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha vivyo hivyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kuhudumu kama washauri katika Urais wa Wavulana, kuanzia sasa: Bradley Ray Wilcox kama Mshauri wa Kwanza na Michael T . Nelson kama Mshauri wa Pili.

Wale wanaounga mkono wanaweza kuonesha.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa wakuu kama ilivyo sasa.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni kwa kuinua mkono.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Tunawashukuru, akina kaka na akina dada kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Mabadiliko kwa Sabini wa Eneo

Sabini wa Eneo wafuatao waliidhinishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Isaías Alcala, John D. Amos, Johnny O. Baddoo, Victor O. Bassey, Adrian Bettridge, A. Kaulle Bezerra, Carlos G. Cantero, Emerson B. Carnavale, Orlando A. Castaños, Bun Huoch Eng, Hutch U. Fale, Fernando R. García, Tomás García, C. Alan Gauldin, Aaron T. Hall, Darwin W. Halvorson, Jed J Hancock, Henry Herrera, Ndalamba Ilunga, Samuel M. T. Koivisto, Carlos J. Lantigua, Esau Lara, Stephen J. Larson, Thabo Lebethoa, G. Kenneth Lee, Israel Marin, Wayne E. Maurer, Lee G. McCann II, Robert Mendenhall, Adrian Mendez, Siyabonga Mkhize, Javier F. Monestel, Thomas B. Morgan, Jared V. Ormsby, Z. Rudy Palhua, Arturo D. Palmieri, Kenneth Pambu, Hugo O. Panameño, Kevin J. Parks, Paul Picard, David J. Pickett, Martin Pilka, Irineu E. Prado, Christopher R. Price, Miguel Ribeiro, James N. Robinson, Edward B. Rowe, Robert Schwartz, Gregory A. Scott, Dominic R. Sénéchal, Kofi G. Sosu, Michael B. Strong, Nithya Kumar Sunderraj, Thomas A. Thomas, Alejandro H. Treviño, Nefi M. Trujillo, Chimaroke G. Udeichi, Fernando Valdes, Helton C. Vecchi, Brent B. Ward na Tomasito S. Zapanta.

Sabini wa Maeneo wafuatao watapumzishwa mnamo au kabla ya Agosti 1, 2023:

Richard K. Ahadjie, Duane D. Bell, Hubermann Bien Aimé, Víctor R. Calderón, Michel J. Carter, Daniel Córdova, John N. Craig, William H. K. Davis, Fernando P. Del Carpio, Richard J. DeVries, Kylar G. Dominguez, Torben Engbjerg, Kenneth J. Firmage, Edgar Flores, Silvio Flores, Carlos A. Genaro, Mark A. Gilmour, Sergio A. Gómez, Roberto Gonzalez, Virgilio Gonzalez, Spencer R. Griffin, Marcel Guei, Oleksiy H. Hakalenko, Matthew S. Harding, David J. Harris, Kevin J. Hathaway, José Hernández, Glenn M. Holmes, Richard Neitzel Holzapfel, Okechukwu I. Imo, Michael D. Jones, Pungwe S. Kongolo, Ricardo C. Leite, Aretemio C. Maligon, Edgar A. Mantilla, Lincoln P. Martins, Carl R. Maurer, Daniel S. Mehr II, Glen D. Mella, Tomas S. Merdegia Jr., Allistair B. Odgers, R. Jeffrey Parker, Victor P. Patrick, Denis E. Pineda, Henrique S. Simplicio, Jeffrey H. Singer, Michael L. Staheli, Jeffrey K. Wetzel, Michael S. Wilstead na David L. Wright.

Chapisha