Njoo, Unifuate 2024
Januari 15–21: “Njoo na Ule Tunda.” 1 Nefi 6–10


“Januari 16–21: ‘Njoo na Ule Tunda.’ 1 Nephi 6–10,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)

“Januari 15–21. 1 Nefi 6–10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)

Picha
Ono la Lehi la mti wa uzima

Ndoto ya Lehi, na Steven Lloyd Neal

Januari 15–21: “Njoo na Ule Tunda”

1 Nefi 6–10

Ndoto ya Lehi—na fimbo yake ya chuma, ukungu wa giza, jengo kubwa na mti wenye matunda “matamu zaidi ya yote”—ni mwaliko wa kutia msukumo wa kupokea baraka za upendo na dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi. Kwa Lehi, hata hivyo, ono hili pia lilihusu familia yake: “Kwa sababu ya kitu ambacho nilikuwa nimekiona, nina sababu ya kushangilia katika Bwana kwa sababu ya Nefi na pia ya Samu. … Lakini tazama, Lamani na Lemueli, ninaogopa sana kwa sababu yenu” (1 Nefi 8:3–4). Wakati Lehi alipomaliza kuelezea ono lake, aliwasihi Lamani na Lemueli “wasikilize maneno yake, kwamba pengine Bwana angekuwa mwenye huruma kwao” (1 Nefi 8:37). Hata kama umejifunza ono la Lehi mara nyingi, mara hii lifikirie jinsi Lehi alivyolifikiria—fikiria kuhusu mtu unayempenda. Unapofanya hivyo, usalama wa fimbo ya chuma, hatari za jengo pana, na utamu wa tunda vitakuwa na maana mpya. Na utaelewa kwa kina zaidi “huruma zote [za] mzazi mwema” ambaye alipata ono hili kuu.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

1 Nefi 7:6–21

Mimi ninaweza kuwasamehe wengine.

Ni kipi kinakuvutia kuhusu mfano wa Nefi kwenye 1 Nefi 7:6–21? Ni kwa namna ipi tunabarikiwa pale “tunaposameheana kwa dhati”? Video “The Lord Delivers Nephi from His Rebellious Brothers” (Gospel Library) ingeweza kuwa na msaada katika kujifunza kwako.

1 Nefi 8

Kushikilia kwa nguvu neno la Mungu huniongoza kwa Mwokozi na hunisaidia nihisi upendo Wake.

Ono la Lehi linatoa mwaliko wa kutafakari wapi ulipo katika safari yako binafsi ya kuwa kama Kristo. Rais Boyd K. Packer alisema juu ya ono hili: “Wewe uko ndani yake; sisi sote tupo ndani yake. Ndoto au ono la Lehi juu ya fimbo ya chuma lina kila kitu ndani yake … ambacho Mtakatifu wa Siku za Mwisho anahitaji kuelewa juu ya mtihani wa maisha” (“Lehi’s Dream and You,” New Era, Jan. 2015, 2).

Unapojifunza fikiria kujaza chati kama hii hapa.

Ishara kutoka kwenye ono la Lehi

Maana

Maswali ya kutafakari

Ishara kutoka kwenye ono la Lehi

Mti na tunda lake (1 Nefi 8:10–12)

Maana

Maswali ya kutafakari

Ninafanya nini ili kuwaalika wengine washiriki upendo wa Mungu?

Ishara kutoka kwenye ono la Lehi

Mto (1 Nefi 8:13)

Maana

Maswali ya kutafakari

Ishara kutoka kwenye ono la Lehi

Fimbo ya Chuma (1 Nefi 8:19–20, 30)

Maana

Maswali ya kutafakari

Ishara kutoka kwenye ono la Lehi

Ukungu wa giza (1 Nefi 8:23)

Maana

Maswali ya kutafakari

Ishara kutoka kwenye ono la Lehi

Jengo kubwa na pana (1 Nefi 8:26–27, 33)

Maana

Maswali ya kutafakari

Ishara kutoka kwenye ono la Lehi

Maana

Maswali ya kutafakari

Ungeweza pia kutafuta kutoka katika mistari ifuatayo ili kujifunza kuhusu makundi manne ya watu Lehi aliyoyaona: 1 Nefi 8:21–23, 24–28, 30, na 31–33. Je, ni tofauti ipi unayoiona kati ya makundi haya? Je, ni kwa nini baadhi ya watu waliondoka hata baada ya kufika kwenye mti na kula tunda (ona mistari 24–28)? Je, unajifunza nini kutokana na uzoefu huu?

Ona pia Kevin W. Pearson, “Stay by the Tree,” Liahona, Mei 2015, 114–16; “Lehi Sees a Vision of the Tree of Life” (video), Gospel Library.

Waruhusu wanafunzi washiriki kile walichogundua. Fikiria kuwaalika wanafunzi watafute wao wenyewe maandiko juu ya kweli wanazozipata. Kwa mfano, ungeweza kuwaalika watafute marejeleo ya maandiko kwenye chati hapo juu wao wenyewe au wakiwa kwenye makundi madogo madogo. Watakumbuka na kuthamini kweli wanazozipata.

Picha
watu wakishikilia fimbo ya chuma inayoelekeza kwenye mti wa uzima

Uzi wa Kawaida, na Kelsy na Jesse Barrett

1 Nefi 10:2–16

Manabii wa kale walijua kuhusu misheni ya Yesu Kristo na walimshuhudia Yeye.

Kwa nini unadhani Bwana alipenda familia ya Lehi—na sisi sote—tujue ukweli unaopatikana katika 1 Nefi 10:2–16? Fikiria jinsi gani ungeweza kuwasaidia wapendwa wako wamwalike Mwokozi maishani mwao.

Picha
ikoni ya seminari

1 Nefi 10:17–19

Mungu atafunua ukweli kwangu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. 

Je, ni kwa namna ipi unaitikia wakati unapotakiwa kuishi kanuni ya injili ambayo huielewi? Katika maandiko yafuatayo, gundua tofauti kati ya mwitikio wa Nefi kwenye ono la Lehi (ona 1 Nefi 10:17–1911:1) na mwitikio wa Lamani na Lemueli (ona 1 Nefi 15:1–10). Ni kweli zipi ambazo Nefi alizielewa ambazo zilimuongoza kuitikia kama alivyofanya?

Ukiwa na mfano wa Nefi mawazoni, tengeneza orodha ya kanuni za injili ambazo ungependa uzielewe vizuri zaidi. Je, ungefanya nini ili kupata majibu wewe mwenyewe? (Ona pia “Ukweli Utakuweka Huru” katika Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 30–33.)

Kama vile Nefi alivyopata mwenyewe ukweli wa maneno ya baba yake, nasi pia tunaweza kufanya vivyo hivyo pale tunaposikia maneno ya manabii na mitume wa sasa. Je, ni kipi mitume na manabii wametufundisha kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni? Je, umepata ushuhuda binafsi wa kile walichokifundisha?

Ona pia 1 Nefi 2:11–19; Mafundisho na Maagano 8:1–3; “Search, Ponder, and Pray,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109; Mada za Injili, “Ufunuo,” Gospel Library.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

1 Nefi 8

Neno la Mungu huniongoza Kwake na hunisaidia nihisi upendo wake.

  • Watoto wako wangeweza kufurahia kuchora picha ya ono la Lehi wakati mkisoma 1 Nefi 8 kwa pamoja. Waruhusu washiriki picha zao, na wasaidie wagundue kile ambacho alama kweye ono la Lehi huwakilisha (ona 1 Nefi 11:21–22; 12:16–18; 15:23–33, 36 na ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Waombe washiriki majibu mengi kadiri wawezavyo ya swali hili: Je tunajifunza nini kutoka kwenye ono la Lehi?

  • Je, una kitu ambacho kinaweza kuwakilisha fimbo ya chuma kwenye ono la Lehi kama vile bomba au fimbo? Waruhusu watoto wakishikilie wakati ukiwaongoza kuelekea kwenye chumba chenye picha ya Mwokozi. Kwa nini fimbo ya chuma ni muhimu sana katika ono la Lehi? (Ona 1 Nefi 8:20, 24, 30). Ni kwa namna gani fimbo ya chuma ni kama neno la Mungu?

  • Waalike baadhi ya watoto wako wasome 1 Nefi 8:10–12 na waeleze kile Lehi alichokiona. Waombe wengine wasome 1 Nefi 11:20–23 na waeleze kile Nefi alichokiona. Kwa nini malaika alimwonesha Nefi mtoto Yesu ili kumfundisha kuhusu upendo wa Mungu? Zungumza na watoto wako kuhusu jinsi gani wamehisi upendo wa Mungu katika maisha yao. Wimbo kama “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75 ungeweza kuwasidia wafikirie mifano.

1 Nefi 10:17–19; 11:1

Mungu atafunua ukweli kwangu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

  • Je, ungewezaje kuwasaidia watoto wako waelewe kile ambacho Nefi alikifundisha katika 1 Nefi 10:19? Pengine ungeweza kukunja picha ya Mwokozi au kitu kingine muhimu ndani ya blanketi na uwaalike watoto wako wakifungue. Wakati unaposoma 1 Nefi 10:19, wangeweza kunyanyua mikono yao wakati wakisikia maneno “watafunguliwa” na “Roho Mtakatifu.” Kisha ungeweza kushiriki tukio wakati ambapo Roho Mtakatifu alikusaidia ugundue ukweli.

  • Waombe watoto wazungumze kuhusu kile wanachokifanya ili kupata majibu ya swali. Je, Nefi angesema nini kama mtu angemuuliza namna ya kupata majibu ya swali linalohusu injili? Wahimize watoto watafute majibu kwa kusoma 1 Nefi 10:17–19; 11:1.

  • Je, watoto wako wamewahi kuhisi kwamba Roho Mtakatifu aliwasaidia wajue kwamba jambo fulani ni la kweli? Waruhusu washiriki uzoefu wao. Je, ungesema nini kwa rafiki ambaye anadhani kwamba hawezi kupokea majibu kupitia Roho Mtakatifu? Tunapata nini katika 1 Nefi 10:17–19 na 11:1 ambacho kingeweza kumsaidia rafiki huyo?

Kwa msaada zaidi, ona toleo la gazeti la mwezi huu la Rafiki.

Picha
Ono la Lehi

Mti wa Uzima, na Avon Oakeson

Chapisha