Njoo, Unifuate 2024
Januari 22–28: “Kujikinga kwa Utakatifu na kwa Nguvu za Mungu.” 1 Nefi 11–15


“Januari 22–28: ‘Kujikinga kwa Utakatifu na kwa Nguvu za Mungu.’ 1 Nefi 11–15,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)

“Januari 22–28. 1 Nefi 11–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)

Picha
watu wakila tunda la mti wa uzima

Upendo wa Mungu, na Sabrina Squires

Januari 22–28 “Kujikinga kwa Utakatifu na kwa Nguvu za Mungu”

1 Nefi 11–15

Wakati Mungu anapokuwa na kazi kubwa ya kufanywa na nabii Wake, mara nyingi Yeye humpa nabii huyo ono kubwa. Musa, Yohana, Lehi na Joseph Smith wote walikuwa na maono kama hayo—maono ambayo yalipanua mawazo yao na kuwasaidia waone jinsi kazi ya Mungu ilivyo kuu na ya kushangaza.

Nefi pia alikuwa na moja ya maono haya yabadilishayo maisha. Aliona huduma ya Mwokozi, mambo yajayo ya kizazi cha Lehi kwenye nchi ya ahadi na hatima ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Baada ya ono hili, Nefi alikuwa ameandaliwa vyema kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele yake. Kusoma juu ya ono hili kunaweza kukuandaa wewe pia—kwa ajili ya kazi ambayo Mungu anayo kwa ajii yako katika ufalme Wake. Wewe ni miongoni mwa “watakatifu wa kanisa la Mwanakondoo” aliloliona Nefi, “ambao walitawanyika kote usoni mwa dunia; na walikuwa wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu” (1 Nefi 14:14).

Ona pia “Nephi Sees a Vision of Future Events” (video), Gospel Library.

Mawazo kwa ajili ya kujifunza nyumbani na Kanisani

1 Nefi 11

Mungu alimtuma Yesu Kristo kama dhihirisho la upendo Wake.

Wakati Nefi alipomuuliza malaika kuhusu maana ya mti kwenye ono la Lehi, malaika angeweza kusema kwa urahisi, “Unawakilisha upendo wa Mungu.” Badala yake, alimuonesha Nefi mfululizo wa ishara na matukio kutoka kwenye maisha ya Kristo. Tafuta ishara hizo na matukio hayo wakati ukisoma na kutafakari 1 Nefi 11. Je, unapata nini ambacho kinakusaidia uelewe kwa nini Yesu Kristo ni dhihirisho la juu la upendo wa Mungu?

Ungeweza pia kufikiria kuangalia video za Biblia kwenye Maktaba ya Injili ambazo zinashabihiana na matukio ambayo Nefi aliyaona. Je, ni kwa namna gani Mwokozi alikusaidia wewe uhisi upendo wa Baba yako wa Mbinguni?

Ona pia Susan H. Porter, “Upendo wa Mungu: Ni wa Shangwe Kuu kwenye Nafsi,” Liahona, Nov. 2021, 33–35.

1 Nefi 12–14

Ninaweza “Kujihami kwa Utakatifu” na Nguvu.

Nefi asingeishi kushuhudia mengi ya kile alichokiona katika ono lake. Kwa nini unadhani ilikuwa ya thamani kwa Nefi kuvijua vitu hivi? Kwa nini ni ya thamani kwako wewe kuvijua vitu hivi? Uliza maswali haya kila wakati unaposoma kuhusu kitu fulani ambacho Nefi alikiona katika ono lake (ona 1 Nefi 12–14). Ni misukumo ipi unaipokea kuhusu jukumu lako katika “kazi kuu na ya … ajabu ya Bwana”? (1 Nefi 14:7). Ni baadhi ya mambo yapi makuu na ya ajabu ambavyo Ameyafanya kwa ajili yako?

Fikiria hasa ahadi kwenye 1 Nefi 14:14. Je, ni kwa namna gani Mwokozi ametimiza ahadi hii katika maisha yako? (Kwa baadhi ya mifano, ona David A. Bednar, “Kwa Nguvu za Mungu katika Utukufu Mkuu,” Liahona, Nov. 2021, 28–30, hasa vipengele viwili vya mwisho.)

1 Nefi 13:1–9; 14:9–11

Je, “kanisa kuu na la machukizo” ambalo Nefi aliliona ni kitu gani?

Mzee Dallin H. Oaks alieleza kwamba lile “kanisa kuu na la machukizo” lililozungumziwa na Nefi linawakilisha “falsafa yoyote au shirika lolote linalopinga imani katika Mungu. Na ‘utumwa’ ambao ‘kanisa’ hili linatafuta kuuleta kwa watakatifu hautakuwa kuzuiliwa kimwili bali utumwa wa mawazo ya uwongo” (“Stand as Witnesses of God,” Ensign, Mar. 2015, 32). Tafakari jinsi Mwokozi anavyokusaidia kuepuka—na kunusurika kutokana na—utumwa wa mawazo ya uongo.

1 Nefi 15:1–11

Mungu atanijibu iwapo nitaomba kwa imani.

Je, umewahi kuhisi kana kwamba ulikuwa hupokei ufunuo binafsi—kwamba Mungu alikuwa hazungumzi na wewe? Ni ushauri upi Nefi aliwapa ndugu zake walipohisi hivyo? (Ona 1 Nefi 15:1–11.) Unawezaje kutumia ushauri wa Nefi katika maisha yako?

Picha
ikoni ya seminari

1 Nefi 15:23–25

Kushikilia kwa nguvu neno la Mungu hunisaidia nipinge ushawishi wa Shetani.

Nefi mara nyingi alikuwa na vitu vya msingi vya kuwaambia kaka zake. Lakini alionekana mwenye shauku sana kuhusu kile alichowaambia katika 1 Nefi 15:23–25. Je, ujumbe wa Nefi ulikuwa ni upi, na kwa nini unafikiri alihisi msukumo kuhusu hilo?

Mzee David A. Bednar alifundisha “neno la Mungu” linaweza kumaanisha maandiko, maneno ya manabii walio hai na Yesu Kristo Mwenyewe. Je, unadhani inamaanisha nini “kushikilia kwa nguvu” maandiko na maneno ya manabii walio hai? Inamaanisha nini “kushikilia kwa nguvu” kwa Yesu Kristo? Ungeweza kutafuta majibu ya maswali haya katika ujumbe wa Mzee Bednar “Lakini Hatukuwasikiliza” (Liahona, Mei 2022, 14–16).

Je, kushikilia kwa nguvu neno la Bwana kunakusaidia vipi umpinge adui? Kujaza chati kama hii ifuatayo kungeweza kukusaidia upange mawazo yako:

 … hunisaidia nishinde kiza cha majaribu? (ona 1 Nefi 12:17)

 … hunisaidia “kutofuata” utupu na kiburi cha ulimwengu huu? (1 Nefi 12:18)

Je, ni kwa namna gani kushikilia kwa nguvu maandiko na maneno ya manabii walio hai …

Je, ni kwa namna gani kushikilia kwa nguvu kwa Mwokozi …

Ona pia “Fimbo ya Chuma,” Nyimbo za Dini, na. 158; Jorge F. Zeballos, “Kujenga Maisha Kinzani Dhidi ya yule Adui,” Liahona, Nov. 2022, 50–52.

Picha
familia ikisoma maandiko

Maandiko ni kama fimbo ya chuma ambayo hutuongoza kwenye mti wa uzima.

Kwa msaada zaidi, tazama matoleo ya magazeti ya mwezi huu ya Liahona na Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo Kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

1 Nefi 11:16–33

Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kwa sababu Ananipenda.

  • Ili kumfundisha Nefi kuhusu upendo wa Mungu, malaika alimuonesha Nefi matukio kutoka kwenye maisha ya Mwokozi. Ungeweza kufanya vivyo hivyo kwa watoto wako—wape picha ya matukio aliyoyaona Nefi kwenye 1 Nefi 11:20, 24, 27, 31, na 33 (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 30, 35, 39, 4257). Wakati ukisoma mistari hii, wasaidie watoto wako watafute picha inayoendana na matukio hayo. Je, tunajifunza nini kuhusu Yesu Kristo kutoka katika mistari na picha hizi?

  • Kuimba wimbo kama “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,34–35) kungeweza kuwasaidia watoto wako wahisi upendo wa Mungu. Baada ya kuimba, waulize watoto wanajifunza nini kutoka kwenye wimbo huo. Je, ni kipi kingine tunachojifunza kuhusu upendo wa Mungu kutoka 1 Nefii 11:22–23?

Tumia sanaa kuwasaidia watoto wajifunze. Unapowafundisha watoto hadithi ya maandiko, tafuta njia za kuwasaidia wapate taswira yake. Ungeweza kutumia picha, video, vikaragosi, mavazi na kadhalika.

1 Nefi 13:26–29, 35–36, 40

Kitabu cha Mormoni kinafundisha kweli zenye thamani.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wathamini “kweli za wazi na za thamani” katika Kitabu cha Mormoni, ungeweza kuchora picha na waalike wabadili au waondoe sehemu za picha ili kuifanya ionekane tofauti. Ungeweza kutumia hili kufundisha kwamba vitu katika Biblia vilibadilishwa na kuondolewa kwa kadiri muda ulivyozidi kwenda. Someni pamoja 1 Nefi 13:40 na zungumzeni kuhusu jinsi Kitabu cha Mormoni (“maandishi haya ya mwisho”) hutusaidia tuelewe “vitu vilivyo wazi na vya thamani” ambavyo vilipotea kutoka katika Biblia (maandishi ya “kwanza”). Ni “kweli zipi za wazi na zenye thamani” ambazo umejifunza kutoka katika Kitabu cha Mormoni?

  • Video “The Book of Mormon—a Book from God” (Gospel Library) ingeweza kuwasaidia watoto wako waone kwa nini ni muhimu kuwa na vyote Biblia na Kitabu cha Mormoni. Watoto wangeweza kufurahia kutengeneza upya kielelezo kutoka kwenye video.

Picha
nakala za Kitabu cha Mormoni katika lugha mbalimbali

Kitabu cha Mormoni kinarejesha kweli za injili ambazo zilipotea wakati wa Ukengeufu.

1 Nefi 15:23–24

Kushikilia kwa nguvu neno la Mungu hunisaida nishinde majaribu.

  • Wape watoto wako nafasi ya kushiriki kile wanachokikumbuka kuhusu ono la Lehi. Ingeweza kusaidia kutumia picha, kama ile iliyoko kwenye muhtasari wa wiki iliyopita. Nini kiliwazuia watu wasiufikie mti? Nini kiliwasaidia waufikie? Ungeweza kuwaomba watafute fimbo ya chuma kwenye picha. Someni pamoja 1 Nefi 15:23–24 ili kupata fimbo ya chuma humaanisha nini na jinsi inavyoweza kutusaidia.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Ono la Nefi juu ya Mariamu na mtoto Yesu

Ono la Nefi juu ya Mariamu, na James Johnson

Chapisha