Njoo, Unifuate
Aprili 15–21: “Anafanya Kazi ndani Yangu ili Nitende Kulingana na Mapenzi Yake” Enoshi–Maneno ya Mormoni


“Aprili 15–21: ‘Anafanya Kazi ndani Yangu ili Nitende Kulingana na Mapenzi Yake.’ Enoshi–Maneno ya Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)

“Aprili 15–21. Enoshi–Maneno ya Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)

Enoshi kama mvulana mdogo pamoja na Yakobo, baba yake na mama yake

Yakobo na Enoshi, na Scott Snow

Aprili 15–21: “Anafanya Kazi ndani Yangu ili Nitende Kulingana na Mapenzi Yake”

Enoshi–Maneno ya Mormoni

Ingawa Enoshi alienda porini kuwinda wanyama ili akidhi njaa ya kimwili, aliishia kubaki pale siku nzima na mpaka usiku kwa sababu “roho yake ilihisi njaa.” Njaa hii ilimsababisha Enoshi “kupaza sauti [yake] juu kiasi kwamba ilifika mbinguni.” Analielezea tukio hili kama mweleka mbele ya Mungu (ona Enoshi 1:2–4). Kutoka kwa Enoshi tunajifunza kwamba sala ni juhudi za dhati za kusonga karibu na Mungu na kutafuta kuyajua mapenzi Yake. Wakati unaposali kwa nia hii, unaelekea kugundua, kama Enoshi alivyogundua, kwamba Mungu anakusikia na hakika anakujali wewe, wapendwa wako na hata maadui zako (ona Enoshi 1:4–17). Wakati unapofahamu mapenzi Yake, unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutimiza mapenzi Yake. Kama vile Mormoni, unaweza “usijue mambo yote; lakini Bwana anajua mambo yote …; kwa hivyo, anafanya kazi ndani [yako] ili utende kulingana na mapenzi yake” (Maneno ya Mormoni 1:7).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Enoshi 1:1–17

Mungu atasikia na kujibu sala zako.

Uzoefu wako wa sala huenda usiwe wa kushangaza kama wa Enoshi, lakini haupaswi kupuuzwa. Haya ni baadhi ya maswali ya kutafakari wakati ukisoma Enoshi 1:1–17:

  • Ni maneno yapi yanaeleza juhudi za Enoshi alipokuwa akisali?

  • Je, ni kwa namna ipi sala za Enoshi zilibadilika kutoka mstari wa 4 hadi wa 11?

  • Je, ninajifunza kipi kutokana na sala za Enoshi ambacho kinaweza kunisaidia niboreshe sala zangu?

Ona pia “Enos Prays Mightily” (video), Gospel Library; “Sala Tamu,” Nyimbo za Dini, na. 74.

Kushiriki maswali ya majadaliano. Kama unawafundisha wengine, fikiria kuweka maswali ambayo ungependa kujadili kwenye sehemu ya wazi ili kwamba kila mtu aweze kuyaona. Hii itasaidia watu watafakari maswali na kutoa majibu yenye msukumo zaidi.

ikoni ya seminari

Enoshi 1:1–4

Bwana anaweza kunisaidia niishawishi familia yangu kwa wema.

Pengine kuna mtu fulani kwenye familia yako ambaye unatamani ungemsaidia aje kwa Kristo, lakini unajiuliza kama juhudi zako zinaleta tofauti yoyote. Ni kipi unaweza kujifunza kutoka Enoshi 1:1–4 kuhusu ushawishi wa Yakobo kwa mwanawe Enoshi? Kwa mfano, kishazi “malezi na maonyo ya Bwana” kina maanisha nini kwako? Unawezaje kualika ushawishi Wake nyumbani kwako?

Wakati ukiifikiria familia yako, fikiria maswali na nyenzo hizi:

Mzee Dieter F. Uchtdorf alishiriki ushauri wenye msaada kwa ajili ya familia kwenye “Katika Kuwasifu Wale Wanaookoa” (Ensign au Liahona, Mei 2016, 77–80). Je, ujumbe wake unakusukuma ufanye kipi ili kuimarisha familia yako? (Ona hasa sehemu yenye kichwa cha habari “Kuziokoa Familia Zetu”).

Ona Mada za Injili, “Familia,” Gospel Library; “Home and Family—Through Small Things” (video), Gospel Library.

Enoshi 1:1–18

Ninaweza kupokea msamaha wakati nikitumia imani yangu kwa Kristo.

Wakati mwingine unaweza kujiuliza kama dhambi zako zimesamehewa, hata baada ya kuwa umetubu dhambi hizo. Ni utambuzi upi unaupata kutokana na uzoefu wa Enoshi katika Enoshi 1:1–8? Ni kwa jinsi gani Enoshi alionesha imani kwa Yesu Kristo kabla na baada ya kuwa amepokea msamaha?

Yoramu–Omni

Kadiri ninavyojitahidi kushika amri Zake, Mungu atanibariki.

Vitabu vya Yaromu na Omni vinaeleza uhusiano kati ya haki na mafanikio. Unajifunza kipi kutoka Yaromu 1:7–12; Omni 1:5–7, 12–18? Ni kwa namna ipi maana za kiulimwengu juu ya mafanikio ni tofauti na maana kutoka kwa Bwana? Je, ni kwa namna gani Bwana huwasaidia watu wake wafanikiwe? (ona Alma 37:13; 48:15–16).

Omni 1:25–26

“Njooni kwa Kristo, ambaye ni Mtakatifu Pekee wa Isareli.”

Mwaliko wa “Kuja kwa Kristo” unaonekana mara nyingi katika Kitabu cha Mormoni. Ukweli ni kwamba, moja ya lengo kuu la kitabu hiki ni kutoa mwaliko huu kwa kila mtu. Unaposoma Omni 1:25–26, ni maneno yapi au kifungu kipi cha maneno kinaeleza jinsi ya kuja kwa Kristo? Je, utafanya kipi ili uje kwa Kristo kwa ukamilifu zaidi?

Mormoni akiyaweka pamoja mabamba ya dhahabu

Mormoni Akiweka Pamoja Mabamba ya Dhahabu, na Jorge Cocco

Maneno ya Mormoni 1:1–8

Mungu atafanya kazi kupitia mimi pale ninapofuata mwongozo Wake.

Sababu mojawapo ya Bwana kumpa msukumo Mormoni kujumuisha mabamba madogo ya Nefi katika Kitabu cha Mormoni ilikuwa ni kwa sababu Mungu alijua kwamba kurasa 116 za mwanzo zilizotafsiriwa za Kitabu cha Mormoni zingepotea (ona Mafundisho na Maagano 10; Watakatifu, juzuu ya 1, sura ya 5). Je, ni kwa nini wewe una shukrani kwamba Mormoni alifuata maelekezo ya Bwana ya kujumuisha maneno haya (yakijumuisha 1 nefi mpaka Omni)? Ni sababu zipi Mormoni alizitoa juu ya kuyajumuisha? (ona Maneno ya Mormoni 1:3–7). Je, ni wakati upi umeona Mungu akifanya kazi Yake kupitia wewe au wengine?

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Enoshi 1:1–5

Ninaweza kuzungumza na Baba wa Mbinguni kupitia sala.

  • Je, unawezaje kuwasaidia watoto wako wafanye sala zao ziwe zenye maana zaidi? Fikiria kuwaonesha picha ya Enoshi akisali; waruhusu waeleze kile wanachokiona. Kisha wangeweza kufumba macho na kuvuta taswira kwamba wanazungumza na Baba wa Mbinguni ana kwa ana. Je, ni jambo lipi wangependa kulizungumzia? Je, ni jambo lipi wangetaka Yeye aseme kwao?

  • Unaposoma kwa sauti Enoshi 1:1–5, watoto wadogo wangejifanya kuwa Enoshi kwa kuigiza wakiwa wanawinda, wakipiga magoti kusali na kadhalika. Watoto wakubwa wangeweza kusikiliza neno au kifungu cha maneno ambacho kinafafanua sala za Enoshi. Je, maneno haya hutuambia nini kuhusu sala za Enoshi? Shiriki uzoefu ambapo nafsi yako “ilipata njaa” na wewe “ukamlilia” Bwana (Enoshi 1:4).

familia ikisali

Kama watoto wa Mungu, tunaweza kusali kwa Baba yetu wa Mbinguni.

Enoshi 1:2–16

Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zangu.

  • unawezaje kuwasaidia watoto wako waelewe kwamba Baba wa Mbinguni atasikia na kujibu sala zao? Fikiria kuwaalika wasikilize vitu ambavyo mara nyingi wanaviomba kwenye sala. Kisha ungeweza kuwasaidia wapate kile ambacho Enoshi alikiomba kwenye Enoshi 1:2, 9, 13–14, na 16 (ona pia “Mlango wa 11: Enoshi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 30–31).

    Ni yapi yalikuwa matokeo ya sala ya Enoshi? (Ona mistari 6, 9, 11).

    Je tunajifunza kipi kutoka kwenye uzoefu wa Enoshi kuhusu kuboresha namna tunavyosali?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13). Pengine watoto wako wangeweza kunyanyua mikono yao kila mara wanaposikia neno “sali” au “sala” au neno lingine linalojirudia. Waambie watoto wako kuhusu baadhi ya njia ambazo Baba wa Mbinguni amejibu sala zako.

Maneno ya Mormoni 1:3–8

Ninaweza kuwabariki wengine wakati ninapomsikiliza Roho Mtakatifu.

  • Mormoni alifuata mwongozo wa Roho Mtakatifu kujumuisha mabamba madogo ya Nefi katika Kitabu cha Mormoni. Kila kitu tunachojifunza kwenye Kitabu cha Mormoni mwaka huu kimetufikia kwa sababu Mormoni alifanya uamuzi wa kumsikiliza Roho. Unawezaje kuwasaidia watoto wako wajifunze kuhusu kumsikiliza Roho? Waalike wafanye zamu ya kusoma mistari kutoka Maneno ya Mormoni 1:3–8. Ungeweza kuzungumza kuhusu kile wanachojifunza kutoka kwenye kila mstari. Watoto wako kisha:

    • Wangeshiriki kile ambacho wamejifunza kutoka kwenye masimulizi kutoka Kitabu cha Mormoni kwa mwaka huu (picha kutoka Njoo, Unifuate zinaweza kuwasaidia wakumbuke).

    • Imbeni pamoja wimbo kuhusu Roho Mtakatifu, kama vile “The Still Small Voice” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 106–7).

    • Zungumza kuhusu uzoefu wa wakati ambapo waliongozwa na Roho kufanya kitu fulani ambacho kilimbariki mwingine.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Enoshi akisali

Enoshi Akisali, na Robert T. Barrett