Njoo, Unifuate 2024
Agosti 5–11: “Mpango Mkuu wa Furaha.” Alma 39–42


Agosti 5–11:‘Mpango Mkuu wa Furaha.’ Alma 39–42,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Agosti 5–11. Alma 39–42,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
Yesu akitoka kaburini

Amefufuka, na Del Parson

Agosti 5–11: “Mpango Mkuu wa Furaha”

Alma 39–42

Wakati mtu tunayempenda anapokuwa ametenda kosa kubwa, inaweza kuwa vigumu kujua jinsi ya kujibu. Sehemu ya kile kinachofanya Alma 39–42 kuwa yenye thamani kubwa ni kwamba inafunua jinsi Alma—mfuasi wa Kristo ambaye kwa wakati mmoja alikuwa na dhambi zake mwenyewe za kutubu—alishughulikia hali kama hiyo. Koriantoni mwana wa Alma alikuwa ametenda dhambi ya uasherati, na Alma, kama alivyojifunza katika huduma yake, aliamini uwezo wa mafundisho ya kweli ili kumpa mwanaye mtazamo wa milele na kuhamasisha toba (ona Alma 4:19; 31:5). Katika sura hizi, tunaona ujasiri wa Alma katika kulaani dhambi na huruma na upendo wake kwa Koriantoni. Na hatimaye, tunahisi kujiamini kwa Alma kwamba Mwokozi “atakuja kuondoa dhambi za ulimwengu [na] kutangaza habari njema ya wokovu kwa watu wake” (Alma 39:15). Ukweli kwamba Koriantoni alitubu na hatimaye kurejea kwenye kazi ya huduma (ona Alma 49:30) unaweza kutupa tumaini kwa ajili ya msamaha na ukombozi wakati tunaposumbuliwa kuhusu dhambi zetu au dhambi za mtu tunayempenda (ona Alma 42:29).

Ona pia “Alma Counsels His Sons” (video), Maktaba ya Injili.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Alma 39

Picha
seminary icon
Ninaweza kuepuka dhambi ya uasherati.

Ushauri wa Alma kwa mwanaye Koriantoni katika Alma 39 hutupatia nafasi kubwa ya kujifunza kuhusu athari haribifu za dhambi ya uasherati, ikijumuisha ponografia. Pengine cha muhimu zaidi, inaweza pia kukusaidia wewe uelewe zawadi ya Mwokozi ya msamaha na uponyaji kwa watu wanaotubu. Maswali haya na shughuli hizi zinaweza kusaidia:

  • Ni makosa yapi yalimsababisha Koriantoni kuvunja sheria ya usafi wa kimwili? (ona Alma 39:2–4, 8–9). Matokeo ya matendo yake yalikuwa yapi? (ona mistari 5–13). Ni ushahidi gani tunao kwamba Koriantoni alitubu? (ona Alma 42:31; 49:30; 48:18). Unajifunza nini kumhusu Mwokozi kutokana na uzoefu huu?

  • Soma ukurasa wa 19–20 wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi. Kisha andika maelezo yako mwenyewe ya ponografia ni nini, kwa nini ni hatari na utafanya nini utakapokumbana nayo. (Ona pia Mathayo 5:27–28 na Mafundisho na Maagano 63:16.)

  • Ni kwa jinsi gani ungeweza kumwelezea rafiki kwa nini ulichagua kuepuka ponografia na kuishi sheria ya usafi wa kimwili? Ni umaizi gani ungeshiriki kutoka kwenye “Mwili Wako ni Mtakatifu” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi (ukurasa wa 22–29)?

  • Fikiria kutazama video “To Look Upon” (Gospel Library). Simamisha video kila wakati ambapo Daudi angefanya chaguo tofauti. Ni kwa jinsi gani chaguzi za Daudi ni sawa na chaguzi ambazo ungeweza kukabiliana nazo?

Tulia kwa muda ili kutafakari. Wakati unapotazama video, iwe unafundisha au kujifunza wewe mwenyewe, tuliza video mara kwa mara ili kuuliza, “Ninajifunza nini?” Hii inaweza kualika umaizi kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Ona pia Bradley R. Wilcox, “Ustahili Sio Kukosa Dosari,” Liahona, Nov. 2021, 61–67; “Pornography” katika mkusanyiko wa “Life Help” wa Maktaba ya Injili.

Alma 40–41

Nini kitatokea baada ya mimi kufa?

Koriantoni alikuwa na maswali fulani kuhusu nini hutokea baada ya kifo. Wasiwasi wake ulimwongoza Alma kufundisha kanuni zinazopatikana katika Alma 40–41. Unapojifunza, tengeneza orodha ya kweli ambazo unazipata kuhusu vitu kama ulimwengu wa kiroho, ufufuko na hukumu. Fikiria kusoma milango hii kutoka taswira ya mtu ambaye, kama Koriantoni, anahitaji kutubu—hata hivyo, hiyo ni kweli kwetu sote.

Alma 40

Ninaweza kutafuta majibu ya maswali yangu kwa imani katika Yesu Kristo.

Wakati mwingine tunaweza kudhani kwamba manabii wanajua majibu kwa kila swali la injili. Lakini kumbuka maswali ambayo hayakuwa na majibu aliyokuwa nayo Alma katika Mlango wa 40. Ni kipi alifanya ili kupata majibu? Yeye alifanya nini wakati alipokuwa hana majibu? Ni kwa jinsi gani mfano wa Alma unaweza kukusaidia wewe?

Picha
mwanamke akisali

Sala ni njia mojawapo ambayo tunaweza kupata majibu ya maswali ya injili.

Alma 42

Upatanisho wa Yesu Kristo huleta uwezekano wa ukombozi.

Koriantoni aliamini kwamba adhabu kwa ajili ya dhambi haikuwa haki (ona Alma 42:1). Katika Alma 42, ni kwa jinsi gani Alma alishughulikia wasiwasi wake? Ungeweza kupanga vifungu katika sura hii katika makundi mawili: “Mungi ni wa haki” na “Mungu ni mwenye rehema.” Ni kwa jinsi gani Upatanisho wa Mwokozi unafanya vyote haki na rehema kuwezekana? Tafuta utambuzi wa ziada katika video “The Mediator” (Maktaba ya Injili).

Ona pia: “Ni Upendo Ulioje,” Nyimbo za Dini, na. 108.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Alma 39:1, 10–11

Mfano wangu mzuri unaweza kuwaongoza wengine kwa Kristo.

  • Ushauri wa Alma kwa Koriantoni unaweza kuwasaidia watoto wako waelewe umuhimu wa kuwa mfano mzuri. Fikiria kusoma pamoja Alma 39:1. Ni kwa jinsi gani Shibloni kaka wa Koriantoni alikuwa mfano mzuri? Waombe watoto wako watafute majibu ya ziada kwa swali hili katika Alma 38:2–4.

  • Mngeweza pia kucheza mchezo ambapo wewe na watoto mnapeana zamu kufuatana au kila mmoja akimwigiza mwingine. Tumia mchezo huu kuonesha jinsi matendo yetu yanavyoweza kuwasaidia wengine kufanya chaguzi nzuri. Imbeni pamoja “I Am like a Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 163), na uwasaidie watoto wako wafikirie njia wanazoweza kuwa mfano mzuri.

  • Ukiwa na tochi au picha ya jua, ungeweza kulinganisha mwanga na nguvu ya mfano mwema. Wewe na watoto wako mngeweza pia kutazama picha za Yesu akifanya mambo mazuri na kuzungumza kuhusu mfano mzuri ambao Yeye ametuwekea. Video “Shine Your Light So Others May See” na “Lessons I Learned as a Boy” zingeweza kuwasaidia watoto wako wajadili jinsi mifano yao inavyoweza kuwaongoza watu kwa Kristo.

Alma 39:9–13

Kwa sababu ya Yesu Kristo, ninaweza kutubu wakati ninapofanya makosa.

  • Bila kwenda kwenye maelezo ya kina kuhusu asili ya dhambi yake, eleza kwamba Koriantoni alifanya uchaguzi mbaya. Tungeweza kusema nini ili tumsaidie? Fikiria kuwasomea watoto wako Alma 39:9, na uwasaidie waelewe kutubu na kuacha humaanisha nini. Shuhudia kwamba toba inawezekana kupitia Yesu Kristo na Upatanisho wake.

  • Hapa kuna somo la vitendo ili kuonesha furaha ya toba: Mpe mtoto kitu kizito akishikilie wakati ukisimulia hadithi kuhusu mtu aliyefanya jambo baya na akahisi vibaya. Waambie watoto wako kwamba kitu kile ni sawa na hisia mbaya tunazoweza kuwa nazo tunapofanya kosa. Chukua kitu hicho kizito kutoka kwa mtoto huku ukishuhudia kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kuondoa hisia nzito, mbaya na kutusaidia tusahihishe makosa yetu pale tunapotubu.

Alma 40:6–7, 11–14, 21–23

Baada ya sisi kufa, roho zetu huenda kwenye ulimwengu wa roho hadi Ufufuko na Hukumu.

  • Ni kawaida kujiuliza nini hutokea kwetu baada ya kufa. Unaweza kufanya nini ili kuwasaidia watoto wako wapate majibu yenye mwongozo? Ungeweza kuandika kifo, ulimwengu wa roho (paradiso na kifungo cha roho), ufufuo, na hukumu kwenye vipande tofauti vya karatasi. Wasaidie watoto wako waelewe maana ya maneno haya. Mnaposoma pamoja Alma 40: 6–7, 11–14, 21–23, watoto wako wangeweza kuweka maneno ubaoni katika mpangilio ambao yanatokea katika mistari hii.

  • Watoto wakubwa wanaweza kufaidika kutokana na majibu ya maswali kwa kupekua Alma 40:6–7, 11–14, 21–23. Fikiria kuwauliza watoto wako maswali ambayo yanaweza kujibiwa katika mistari hii, kama vile “Mwili wangu utakuwa vipi wakati nitakapofufuka? Waalike wapekue kwa ajili ya majibu katika mistari sahihi.

    Picha
    Mariamu na Yesu

    Mariamu na Bwana Aliyefufuka, na Harry Anderson

  • Je, watoto wako wanamjua mtu aliyekufa? Pengine wewe ungeweza kuzungumza kwa ufupi kuhusu mtu huyo. Toa ushuhuda wako kwamba siku moja yeye—na yeyote mwingine—watafufuka kwa sababu ya Yesu Kristo. Kama itahitajika, tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kueleza kile inachomaanisha kufufuka.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Alma na Koriantoni

Huyu ni Mwanangu, na Elspeth Caitlin Young

Chapisha