Njoo, Unifuate
Julai 29–Agosti 4: “Mtegemee Mungu na Uishi.” Alma 36–38


“Julai 29–Agosti 4: ‘Mtegemee Mungu na Uishi.’ Alma 36–38,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Julai 29–Agosti 4. Alma 36–38,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

mwanamke akisali

Mwanamke, na Jen Tolman, isinakiliwe

Julai 29– Agosti 4: “Mtegemee Mungu na Uishi”

Alma 36–38

Wakati Alma alipoona uovu uliomzunguka, alihisi “huzuni sana,” majonzi, “mateso,” na “maumivu makali ya moyo” (Alma 8:14). “Uovu miongoni mwa watu hawa,” alisema hivi kuwahusu Wazoramu, “unaumiza roho yangu” (Alma 31:30). Alihisi sawa na vile alivyohisi baada ya kurejea kutoka kwenye misheni yake kwa Wazoramu—aliona kuwa mioyo ya Wanefi wengi “ilianza kuwa migumu, na kwamba walianza kuudhika kwa sababu ya uhalisia wa neno,” na hili lilisababisha moyo wake “kuhuzunika sana” (Alma 35:15). Alma alifanya nini kuhusu yale aliyoyaona na kuhisi? Hakukatishwa tamaa tu au kuwa mbeuzi kuhusu hali ya ulimwengu. Badala yake, “alisababisha kwamba wanawe wakusanywe pamoja” na aliwafundisha “vitu vinavyohusiana na haki” (Alma 35:16). Aliwafundisha kwamba: “Hakuna njia nyingine yoyote au njia ambayo mwanadamu anaweza kuokolewa, ila tu katika Kristo na kupitia Kristo. … Tazama, yeye ni neno la ukweli na haki” (Alma 38:9).

Mawazo kwa ajili ya Kufundisha Nyumbani na Kanisani

Alma 36; 38:5–6

Ninaweza kuzaliwa na Mungu.

Ni wachache wetu ambao watakuwa na uzoefu wa ajabu kama vile uongofu wa Alma. Lakini kila mtu lazima “azaliwe na Mungu,” ingawa hiyo hutokea taratibu (Alma 36:2338:6). Unaposoma Alma 36, fikiria kuhusu kile inachomaanisha kuzaliwa na Mungu. Kwa mfano, katika mchakato wa kuzaliwa na Mungu, ni kwa jinsi gani unahisi kuhusu dhambi? kumhusu Yesu Kristo? Ni kwa jinsi gani kuzaliwa na Mungu kunaathiri kile unachofanya kama mjibizo kwa makosa yako mwenyewe? Ni mabadiliko yapi mengine yanatokea katika imani yako na vitendo vyako? Tafakari jinsi unavyopata uzoefu wa mabadiliko haya.

Ona pia Mosia 5:7; 27:25–26; Alma 5:14; 22:15; Helamani 3:35; “Alma the Younger Is Converted unto the Lord,”(video), Maktaba ya Injili.

Alma 36:12–24; 38:8–9

Yesu Kristo hubadili huzuni kwa shangwe.

Wakati mwingine watu wanaogopa kutubu kwa sababu wanaona toba kama adhabu inayoumiza kwa ajili ya dhambi. Ni kipi unadhani Alma angeweza kusema kuhusu hilo? Ili kugundua, ungeweza kufananisha vile maisha ya Alma yalivyokuwa kabla hajatubu (ona Alma 36:6–17) na maelezo yake juu yake mwenyewe baada ya kutubu (ona mistari 18–27). Kulingana na Alma 36:17–18, ni kwa jinsi gani Alma alipata msamaha huu?

Ona pia Matthew S. Holland, “Zawadi ya Kupendeza ya Mwana,” Liahona, Nov. 2020, 45–47.

Alma 37

Maandiko yamekuwa yakitunzwa “kwa kusudi la busara.”

Fikiria ni muujiza na baraka iliyoje kuwa na maandiko leo hii! Unaposoma Alma 37, tafuta baraka zinazotokana na kuwa na maandiko (ona, kwa mfano, mistari 7–10, 18–19, 44–45).

Katika Alma 37:38–47, Alma alilinganisha “neno la Kristo” na Liahona. Unapotafakari ulinganisho huu, tafakari kuhusu njia ambazo umepata uzoefu wa muujiza na nguvu ya mafundisho ya Kristo “siku hadi siku” (Alma 37:40).

Ona pia D. Todd Christofferson, “Baraka ya Maandiko,” Liahona, Mei 2010, 32–35; “Nisomapo Maandiko,” Nyimbo za Dini, na. 159; “Alma Testifies to His Son Helaman” (video), Maktaba ya Injili.

mwanamke akisoma maandiko

Maandiko hunifundisha jinsi ya kumfuata Mungu.

Alma 37:1–14

seminary icon
“Kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka.”

Wakati mwingine tunaweza kuhisi kwamba shida zetu ni kubwa kupindukia na tatanishi kiasi kwamba suluhu lazima ziwe kubwa na tatanishi pia. Lakini hiyo daima siyo njia ya Bwana. Unaposoma Alma 37:1–14, fikiria ni kipi kinakuvutia kuhusu jinsi Yeye anavyofanya kazi Yake. Kisha unaweza kutafakari na kuandika njia ambazo umeona kanuni hii ikifanya kazi maishani mwako.

Kama unaenda kufundisha kanuni hii kwa mtu, ni mifano ipi kutoka kwenye asili au maisha ya kila siku ungetumia kuionesha? Unaweza kupata baadhi katika ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Vitu Vidogo na Rahisi” (Liahona, Mei 2018, 89–92).

Je, ni baadhi ya vitu gani vilivyo vidogo na rahisi ambavyo vinakuleta karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Kila mara, chaguzi zetu “ndogo na rahisi” huleta tofauti kubwa maishani mwetu. Fikiria kuchagua mada kutoka kwenye Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi na ujiulize maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani chaguzi zangu kuhusu hili hunigusa mimi na watu wanaonizunguka? Ni mabadiliko yapi madogo na rahisi ninaweza kufanya ambayo yataongoza kwenye amani kuu na furaha?

Ona pia Michael A, Dunn, “Asilimia Moja Bora Zaidi,” Liahona, Nov. 2021, 106–8; Mada za Injili, “Haki ya kujiamulia,” Maktaba ya Injili.

Tumia vitu vidogo na rahisi. Kama vitu vingine vingi katika maisha, kufundisha na kujifunza injili kunaweza kufanyika kupitia njia ndogo na rahisi. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani chumvi kidogo au chachu inaweza kutumiwa kujifunza nguvu ya vitu vidogo na rahisi? (ona Mathayo 5:13; 13:33).

Alma 37:35–37

“Shauriana na Bwana.”

Katika Alma 37:35–37, tafuta mialiko ya Alma kwa mwanawe Helamani. Je, ni ipi kati ya mialiko hii unahisi msukumo wa kuitendea kazi? Kwa mfano, unaweza kutafakari inamaanisha nini “kushauriana na Bwana” (mstari wa 37). Je, ni kwa jinsi gani ulijaribu kufanya hivi? Je, ni jinsi gani Yeye amekuelekeza kwa ajili ya mema?

Alma 38

Kushiriki ushuhuda wangu juu Yesu Kristo kunaweza kuwaimarisha wale ninaowapenda.

Maneno ya Alma kwa mwanaye Shibloni yanatoa mfano mzuri wa jinsi ya kuimarisha na kuwahimiza watu tunaowapenda katika kuishi injili. Kujifunza Alma 38 kungeweza kukupa mawazo fulani kwa ajili ya kuwasaidia wanafamilia na marafiki kupata nguvu katika Yesu Kristo. Andika kile unachokipata.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Alma 36:6–24

Toba huniletea shangwe katika Yesu Kristo.

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe kwamba toba huleta shangwe, ungeweza kumpa kila mtoto kipande cha karatasi chenye uso wa furaha upande mmoja na uso wa huzuni upande mwingine. Waombe wasikilize wakati ukisoma au ukifanya muhtasari wa Alma 36:13, 17–20 na wanyanyue mojawapo ya nyuso kuonesha jinsi Alma alivyokuwa akihisi. Watoto wakubwa wangeweza kuandika maneno au virai vinavyoelezea jinsi alivyohisi. Ni kipi kilimfanya Alma kuhuzunika na ni kipi kilimletea shangwe? Kisha waambie kuhusu shangwe unayohisi wakati unapotubu.

Alma 37:6–7

“Kupitia vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka.”

  • Watoto wako wangeweza kufurahia kupata vitu vidogo ambavyo hufanya vitu vikubwa kutokea. Vitu kama betri, funguo ya gari, au hata mwanasesere ambaye huwafariji wao ingeweza kuwa mifano. Mngeweza kisha kusoma Alma 37:6–7 pamoja na kufikiria baadhi ya vitu vidogo na rahisi ambavyo Mungu anatutaka tuvifanye. Ni vitu gani vikubwa vinaweza kutokea wakati tunapotii hizi amri ndogo au rahisi?

  • Watoto wako wangeweza pia kujaribu kitu fulani kama hiki: kuanza kujaza kikombe kwa maji, tone moja kwa wakati. Ni kwa jinsi gani hii inahusiana na Alma 37:6–7? Kisha ungeweza kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo “vitu vidogo na rahisi” vya Bwana, kama vile kusoma maandiko kila siku, ni kama matone ya maji katika kikombe.

  • Wasaidie watoto wako wafikirie njia ambazo wao watafanya vitu vikubwa nyumbani, shuleni, au kanisani. Wimbo “‘Give,’ Said the Little Stream” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 236) pia unaelezea kanuni hii.

Alma 37:38–47

Maandiko yanaweza kunisaidia mimi kila siku.

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto wako wakuze upendo kwa ajili ya neno la Mungu, kama Alma alivyofanya kwa ajili ya Helamani? Fikiria kuwaonesha picha ya Liahona (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 68), au waalike watoto wachore picha wakati wakishiriki kile wanachokijua kuhusu picha hiyo (ona Alma 37:38–47; 1 Nefi 16:10, 28–29). Ni kwa jinsi gani maandiko ni kama Liahona?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

malaika akimtokea Alma na wana wa Mosia

Malaika Akimtokea Alma na Wana wa Mosia, na Clark Kelley Price