“Julai 22–28: ‘Pandeni Neno Hili Mioyoni Mwenu.’ Alma 32–35,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)
“Julai 22–28. Alma 32–35,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)
Alma 22–28: “Pandeni Neno Hili Mioyoni Mwenu”
Alma 32–35
Kwa Wazoramu, sala ilijumuisha kusimama mahali ambapo kila mtu angeweza kuona na kurudia maneno matupu, ya kujiridhisha mwenyewe. Wazoramu walikosa imani katika Yesu Kristo—hata wakakana uwepo Wake—na kuwatesa maskini (ona Alma 31:9–25). Kinyume chake, Alma na Amuleki walifundisha kwamba sala inahusika zaidi na kile kinachofanyika ndani ya mioyo yetu badala ya kwenye jukwaa la umma. Na kama hatutaonesha huruma kwa watu walio na uhitaji, maombi yetu ni “bure, na hayatakupatia … chochote” (Alma 34:28). Muhimu zaidi, tunasali kwa sababu tuna imani katika Yesu Kristo, ambaye anatoa ukombozi kupitia “dhabihu Yake isiyo na mwisho na ya milele” (Alma 34:10). Imani kama hii, Alma alieleza, inaanza na unyenyekevu na “kutamani kuamini” (Alma 32:27). Baada ya muda, kwa lishe ya kila siku, neno la Mungu hukita mizizi ndani ya mioyo yetu mpaka linakuwa “mti utakaokua na kuzaa matunda yasiyo na mwisho” (Alma 32:41).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ninaonesha imani katika Yesu Kristo kwa kupanda na kulisha neno Lake moyoni mwangu.
Unaposoma Alma 32:17–43, tilia maanani maneno na virai ambavyo vinakusaidia uelewe jinsi ya kuwa na imani katika Yesu Kristo. Je, unajifunza kipi kuhusu imani ni nini na kipi ambacho siyo imani?
Njia nyingine ya kujifunza Alma 32 ni kuchora picha zinazowakilisha awamu tofauti za ukuaji wa mbegu. Kisha kwa kila picha weka nembo yenye maneno kutoka Alma 32:28–43 ambayo yanakusaidia uelewe jinsi ya kupanda na kulisha neno la Mungu katika moyo wako.
Ona Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 101–4.
Ninaweza kujua mimi mwenyewe.
Kwa Wazoramu ambao hawakuwa na uhakika kuhusu ushuhuda wa Alma juu ya Kristo, Alma alipendekeza wafanye “jaribio” (ona Alma 32:26). Majaribio yanahitaji shauku, utafiti, kitendo, na angalau imani kidogo—na yanaweza kuongoza kwenye ugunduzi wa ajabu! Fikiria kuhusu majaribio ambayo umewahi kuyaona au kuyashiriki. Kulingana na Alma 32: 26–26, ni aina ipi ya majaribio yanaweza kumwongoza mtu hadi kwenye imani katika Yesu Kristo?
Ni kwa jinsi gani “umefanyia majaribio” neno la Mungu na kuja kujua kwamba “neno ni zuri”? (Alma 32:28).
Ninaweza kumwabudu Mungu katika sala, wakati wowote na mahali popote.
Ushauri wa Alma na Amuleki kuhusu kuabudu na sala ulidhamiria kurekebisha sintofahamu maalumu Wazoramu walizokuwa nazo. Fikiria kuziorodhesha (ona Alma 31:13–23). Kando ya orodha hii, ungeweza kutengeneza orodha ya kweli kuhusu sala katika Alma 33:2–11 na 34:17–29. Je, ni kwa jinsi gani vitu ambavyo unajifunza kutoka kwenye mistari hii vitaathiri jinsi unavyosali na kuabudu?
Unaweza pia kupata maarifa kutoka kwenye wimbo kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, na. 142).
Ninamhitaji Yesu Kristo na Upatanisho Wake.
Tazama ni mara ngapi Amuleki alitumia maneno isiyo na mwisho na milele kuelezea dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi katika Alma 34:9–14. Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Upatanisho wa Mwokozi hauna mwisho na ni wa milele? Tafuta maneno na virai katika mistari hii ambavyo pia vinaelezea Upatanisho wa Mwokozi: Waebrania 10:10; 2 Nefi 9:21; Mosia 3:13.
Hata wakati sisi tunapojua nguvu za Yesu za kuokoa hazina mwisho na ni za milele, tunaweza wakati mwingine kuwa na shaka kwamba zinatumika kwetu—au kwa mtu ambaye ametenda dhambi dhidi yetu. Mzee David A, Bednar wakati mmoja alizungumza juu ya wa watu ambao “wanaonekana kuwa na imani katika Mwokozi, lakini hawaamini kwamba ahadi za baraka Zake zipo kwa ajili yao au zinaweza kufanya kazi katika maisha yao” (“Kama Mngenijua,” Liahona, Nov 2016, 104). Je, ni kipi kingetuzuia sisi kutopokea kikamilifu nguvu ya Mwokozi? Tafakari jinsi wewe unavyoweza kujua kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo hauna mwisho na ni wa milele.
Ili kutafakari kiasi gani unahitaji Upatanisho wa Mwokozi, ingekuwa msaada kufikiria juu ya kitu fulani unachohitaji kila siku. Jiulize mwenyewe, “Maisha yangu yangekuwaje bila kitu hicho?” Kisha, unapojifunza Alma 34:9–16, tafakari maisha yako yangekuwa vipi bila Yesu Kristo. Ungeweza kupata umaizi mwingine katika 2 Nefi 9:7–9. Ni kwa jinsi gani ungefanya muhtasari wa Alma 34:9–10 kwa sentesi moja?
Ona pia Michael John U. Teh, “Mwokozi Wetu Binafsi,” Liahona, Mei 2021, 99–101; Mada za Injili, “Upatanisho wa Yesu Kristo,” Maktaba ya Injili; “Reclaimed” (video), Maktaba ya Injili.
“Sasa ndiyo wakati na siku ya wokovu wako.”
Fikiria kwamba wewe unataka kushiriki katika mbio za masafa marefu au onyesho la muziki. Ni nini kingetokea kama ungengojea hadi siku ya tukio ndiyo ujiandae? Ni kwa namna gani mfano huu unahusiana na maonyo ya Amuleki katika Alma 34:32–35? Kuna hatari gani kuchelewesha juhudi zetu za kutubu na kubadilika?
Mstari wa 31 pia una ujumbe kwa watu ambao wangeweza kuwa na wasiwasi kwamba tayari wamechelewa sana na wamepitwa sana na toba. Ungeweza kusema ujumbe huo ni upi?
Mapendekezo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Bwana anaweza kunifunza ninapochagua kuwa mnyenyekevu.
-
Alma na Amuleki walifanikiwa kuwafundisha Wazoramu ambao walikuwa wanyenyekevu. Je, inamaanisha nini kuwa mnyenyekevu? Wasaidie watoto wako watafute maana ya unyenyekevu katika Mwongozo wa Maandiko. Ni madokezo yapi mengine kuhusu maana ya maneno haya tunaweza kuyapata katika Alma 32:13–16? Waalike watoto wakamilishe sentensi kama vile “Mimi ninakuwa mnyenyekevu wakati ninapo .”
Ushuhuda wangu juu ya Yesu Kristo unakua ninapoulisha.
-
Mbegu, miti na matunda ni vitu vinavyojulikana ambavyo vinaweza kuwasaidia watoto waelewe kanuni za kinadharia kama imani na ushuhuda. Waruhusu watoto wako washikilie mbegu wakati ukisoma Alma 32:28. Kisha ungeweza kuwaomba wakusaidie kufikiria njia nyingi ambazo kukuza ushuhuda juu ya Yesu Kristo ni kama kupanda na kulisha mbengu (ona “Mlango wa 29: Alma Anafundisha kuhusu Imani na Neno la Mungu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 81). Pengine ungeweza kupanda mbegu yako na kuzungumza kuhusu kile kinachohitajika kusaidia mbegu hiyo—au ushuhuda—kukua.
-
Picha ya mti inaambatana na mwongozo huu; ungeweza kuitumia kuonesha kwa mfano maneno ya Alma katika Alma 32:28–43. Au ungeweza kwenda kwenye matembezi kutafuta mimea ikiwa kwenye awamu tofauti za ukuaji na kusoma mistari kutoka Alma 32 ambayo inalinganisha mmea unaokua na ushuhuda wetu. Au pengine watoto wako wangechora mti ubaoni na kuongeza jani au tunda kila wakati wanapofikiria juu ya jambo wanaloweza kufanya ili kusaidia ushuhuda wao katika Yesu Kristo ukue.
-
Ungeweza kuwaruhusu watoto wako wajaribu kuisukuma mbegu (ikiashira neno la Mungu) katika jiwe (ikiashiria moyo wenye kiburi) na kwenye udongo laini (ikiashiria moyo mnyenyekevu). Someni pamoja Alma 32:27–28. Zungumza kile inachomaanisha “kutoa nafasi” (mstari wa 27) kwa neno la Mungu katika mioyo yetu.
Mimi naweza kuomba kwa Baba yangu wa Mbinguni wakati wowote, kuhusu chochote.
-
Wasaidie watoto wako wapate vifungu vya maneno ambvyo vinaelezea mahali tunapoweza kusali (katika Alma 33:4–11) na mambo tunayoweza kusali kuyahusu (katika Alma 34:17–27). Pengine wangeweza kuchora picha zao wenyewe wakisali katika maeneo haya. Shirikianeni uzoefu wenu wakati ambao Baba wa Mbinguni alisikia sala zenu. Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13).