Njoo, Unifuate 2024
Julai 1–7: “Nitawafanya Muwe Chombo.” Alma 17–22


Julai 1–7:‘Nitawafanya Muwe Chombo.’ Alma 17–22,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Julai 1–7. Alma 17–22,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
Amoni akizungumza na Mfalme Lamoni

Amoni na Mfalme Lamoni, na Scott M. Snow

Julai 1–7: “Nitawafanya Muwe Chombo”

Alma 17–22

Fikiria kuhusu sababu zote ambazo watu wanaweza kutoa za kutokushiriki injili: “Sijui vya kutosha” au “Sina uhakika kama watavutiwa” au pengine “ninaogopa nitakataliwa.” Pengine umejikuta wewe mwenyewe ukifikiria mambo kama haya nyakati zingine. Wanefi walikuwa na sababu ya ziada ya kutoshiriki injili kwa Walamani: walikuwa wameelezwa kama “wasio staarabika na wakaidi na wakali; watu ambao walifurahia kuwaua Wanefi” (Alma 17:14; ona pia Alma 26:23–25). Lakini wana wa Mosia walikuwa hata na sababu kubwa zaidi ya kwa nini walihisi kuwa lazima washiriki injili na Walamani: “Walitamani kwamba wokovu utangaziwe kila kiumbe, kwani hawangevumilia kwamba nafsi ya mwanadamu yoyote iangamie” (Mosia 28:3). Upendo huu ambao uliwatia msukumo Amoni na ndugu zake unaweza pia kukutia msukumo wewe kushiriki injili na familia yako, marafiki na watu unaowafahamu—hata wale ambao wanaonekana kwamba huenda wasiikubali.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Alma 17:1–4

Vitendo rahisi, endelevu vya kujitolea kwa Kristo vinanisaidia nipokee nguvu Zake.

Unajifunza nini kutoka kwenye Alma 17:1–4 kuhusu jinsi ya kufanya ushuhuda wako na dhamira yako katika Kristo kuwa imara? Wana wa Mosia walifanya nini, na ni kwa jinsi gani Bwana aliwabariki?

Unaposoma kuhusu uzoefu wa wana wa Mosia katika Alma 17–22, angalia jinsi maandalizi yao ya kiroho yalivyoathiri huduma yao miongoni mwa Walamani (kwa mfano, ona Alma 18:10–18, 34–36; 20:2–5; 22:12–16). Je, unahisi kuvutiwa kufanya nini ili kufuata mfano wao?

Alma 17:6–12; 19:16–36

Picha
ikoni ya seminari
Ninaweza kuwa chombo katika mikono ya Mungu.

Matukio ya uongofu tunayoyasoma katika maandiko mara nyingi ni matukio ya ajabu, lakini kwenye kiini mara nyingi tunapata watu ambao walikuwa na ujasiri wa kuzungumza na kushiriki imani yao katika Yesu Kristo. Fikiria kuhusu hili unaposoma kuhusu Abishi na wana wa Mosia wiki hii.

Unafikiri inamaanisha nini kuwa chombo katika mikono ya Mungu? Ingeweza kuwa msaada kufikiria chombo au vifaa ambavyo unaweza kuvitumia katika maisha yako ya kila siku. Katika Alma 17:6–12, tafuta ni kipi wana wa Mosia walifanya ili waweze kuwa vyombo katika mikono ya Mungu. Ni kwa jinsi gani ungekuwa chombo chenye ufanisi zaidi katika kuwasaidia wengine waje kwa Kristo?

Ni kipi kinakuvutia kuhusu Abishi katika Alma 19:16–36? Unajifunza nini kutoka kwake kuhusu kuwasaidia wengine kujenga imani katika Kristo? Kwa mfano, unahisi ni kitu gani kingewasaidia watu unaowapenda “waamini katika uwezo wa Mungu”? (Alma 19:17).

Ungeweza kulinganisha uzoefu wa Abishi na kanuni ambayo Mzee Dieter F. Uchtdorf aliifundisha katika “Kazi ya Umisionari: Kushiriki Kilichopo Moyoni Mwako” (Liahona, Mei 2019, 15–18). Ni kwa jinsi gani Abishi alionesha mfano wa “Mapendekezo Matano Rahisi” ya Mzee Uchtdorf? Jaribu kuandika baadhi ya mambo ambayo ungesema kumhusu Yesu Kristo. Kwa mfano, “Kwangu mimi, Yesu Kristo …” au “Mwokozi hunisaidia mimi …”

Ona pia Mada za Injili, “Kuhudumu kama Mwokozi Anavyofanya,” Maktaba ya Injili; “Brightly Beams Our Father’s Mercy,” Nyimbo, na. 335; “Come and See,” “Come and Help,” “Come and Belong” (video), Maktaba ya Injili.

Tumia masomo ya vitendo. Wakati wowote watu wanapoweza kuona au kugusa kitu kinachohusiana na kile wanachojifunza, wana uwezekano wa kukumbuka kwa muda mrefu zaidi. Kama unafundisha kuhusu Alma 17:11, kwa mfano, fikiria kuonesha chombo cha muziki au kifaa cha kuandikia ili kusaidia kuchochoea mazungumzo kuhusu kuwa chombo katika mikono ya Mungu.

Alma 17–19

Tunapowaonesha wengine upendo, tunaweza kuwasaidia wapokee injili ya Yesu Kristo.

Tafuta mistari katika Alma 17–19 ambayo inaonesha jinsi upendo wa Amoni kwa Walamani ulivyochochea juhudi zake za kushiriki injili ya Yesu Kristo. Ni kweli zipi zingine kuhusu kushiriki injili tunazojifunza kutokana na mfano huu?

Ona pia “Ammon Serves and Teaches King Lamoni” (video), Maktaba ya Injili.

Picha
Amoni akiokoa kondoo wa Mfalme

Minerva K. Teichert (1888–1976), Amoni anaokoa makundi ya kondoo ya Mfalme, 1949–1951 mafuta juu ya ubao, 35 15/16 × 48 inchi. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu Cha Brigham Young, 1969.

Alma 19:36

Bwana atanisaidia nitubu.

Baada ya kusimulia uongofu wa Lamoni na watu wake, Mormoni alifanya muhtasari wa maelezo na uchunguzi kuhusu Yesu Kristo. Ni kipi Alma 19:36 inakufundisha kuhusu sifa za Bwana? Ni kipi kingine ambacho maelezo katika Alma 19:16–36 yanakufundisha kumhusu Yeye? Ni wakati gani umehisi mkono wa Bwana ukinyoshwa kwako?

Alma 20:23; 22:15–18

Kumjua Mungu kuna thamani ya dhabihu yoyote.

Linganisha kile ambacho baba wa Lamoni alikuwa tayari kukiacha ili kuokoa maisha yake (ona Alma 20:23) na kile ambacho baadaye alikuwa tayari kukiacha ili kupokea shangwe ya injili na kumjua Mungu (ona Alma 22:15, 18). Tafakari kile ambacho wewe uko radhi kutoa dhabihu ili uweze kumjua Mungu kikamilifu zaidi.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana .

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Alma 17:2–3

Ushuhuda wangu juu ya Yesu Kristo unakua pale ninaposoma maandiko, kusali na kufunga.

  • Ni kwa jinsi gani mifano ya wana wa Mosia inawasaidia watoto wajenge shuhuda zao juu ya Yesu Kristo? Ungeweza kuwasaidia watoto watafute kile ambacho wana wa Mosia walikifanya ili kujenga nguvu yao ya kiroho katika Alma 17:2–3. Kisha wangeweza kuchora picha au kupata vielelezo ambavyo vinawasilisha vitu hivi. Wasaidie wapange kile ambacho wao watafanya ili kuimarisha shuhuda zao juu ya Yesu Kristo.

Alma 17–19

Ninaweza kushiriki injili ya Yesu Kristo kwa wengine.

  • Ili kujifundisha kuhusu kuwa chombo katika mikono ya Mungu, kama vile wana wa Mosia walivyokuwa, wewe na watoto mngeweza kutazama chombo au kifaa na kuzungumza kuhusu namna gani chombo hicho kinatumika. Kisha mngeweza kusoma Alma 17:11 na kuzungumza kuhusu inamaanisha nini kuwa chombo cha Baba wa Mbinguni cha kuwasaidia watu wajifunze kuhusu Yesu Kristo.

  • Ukurasa wa shughuli ya wiki hii una picha zinazowakilisha kweli ambazo Amoni alimfundisha Mfalme Lamoni. Unaweza pia kuwasaidia watoto wako watafute kweli hizi katika Alma 18:24–40. Watoto wangeweza kujifanya kuwa wamisionari na kushiriki kile wanachokijua kuhusu kweli hizi.

  • Baada ya kusoma na watoto wako kuhusu Abishi (ona Alma 19:16–20, 28–29), wangeweza kujifanya kuwa Abishi kwa kukimbia hapo hapo walipo, kubisha milango, na kusimulia kuhusu kile kilichotendeka katika Alma 19:1–17. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama Abishi na kushiriki kile tunachokijua kuhusu Yesu Kristo na injili Yake? Watoto wako wangeweza kuchora picha zaao wenyewe wakishiriki injili na mtu au imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu injili, kama vile “Called to Serve” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, 174–75).

Alma 17:21–25; 20:8–27; 22:1–3

Ninaweza kuwasaidia wengine waje kwa Kristo kwa kuonesha upendo wangu kwao.

  • Kwanza, wote Mfalme Lamoni na baba yake walikuwa na mioyo migumu kwenye injili. Baadaye, mioyo yao ililainika, na wakaamini katika Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani hili lilitokea? Wasaidie watoto wako wagundue majibu ya swali hili wakati unapopitia pamoja nao uzoefu wa Amoni. Wangeweza kuigiza “Mlango wa 23: Amoni: Mtumishi Mkuu” na “Mlango wa 24: Amoni Anakutana na Baba wa Mfalme Lamoni” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 64–68, 69–70). Au pengine watoto wako wangeweza kuchora picha za sehemu tofauti za hadithi hiyo na kutumia picha hizo kusimulia hadithi hizo. Ni kipi Amoni alifanya ili kumsaidia Lamoni na baba yake wafungue mioyo yao kwa injili ya Yesu Kristo? (ona Alma 17:21–25; 20:8–27; 22:1–3).

  • Pengine wewe na watoto wako mngeweza kumfikiria mtu ambaye anahitaji kujua kuhusu Yesu Kristo. Wasaidie wafikirie njia ambazo wao wanaweza kuwa mifano mizuri na kuonesha upendo kwa mtu huyo, kama vile Amoni alivyofanya kwa Lamoni na baba yake.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki .

Picha
Kielelezo cha Abishi

Kielelezo cha Abishi, na Dilleen Marsh

Chapisha