Hadithi za Maandiko
Amoni


“Amoni,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 17–18

Amoni

Mtumishi Mnyenyekevu

Amoni na kaka zake wanapunga mikono ya kwaheri

Amoni na kaka zake walitaka kuwafundisha Walamani kuhusu Bwana. Walienda kwenye nchi ambayo Walamani waliishi. Njiani, walifunga na kusali kumwomba Bwana msaada. Bwana aliwafariji. Aliwaambia wawe na subira na wawe mifano mizuri. Kila mmoja alienda sehemu tofauti ili kufundisha.

Mosia 28:1–2; Alma 17:6–13

Amoni anapiga magoti mbele ya mfalme na malkia

Amoni alienda mahali palipoitwa Ishmaeli. Huko watu walimfunga kamba na kumpeleka mpaka kwa mfalme Lamoni. Amoni alimwambia Lamoni kwamba alitaka kuishi pamoja na Walamani. Lamoni alimpenda Amoni na akamuacha huru. Alimtaka Amoni kumuoa mmoja wa mabinti zake, lakini Amoni alichagua badala yake kuwa mtumishi wake.

Alma 17:20–25

Amoni anatazama kondoo kupitia juu ya bega lake.

Lamoni alimwambia Amoni awatunze wanyama wake. Siku moja, Amoni na watumishi wengine waliipeleka mifugo kunywa maji. Wakati mifugo ikinywa maji, wanyang’anyi walikuja na kuitawanya. Watumishi wengine waliogopa kuwa wangeadhibiwa kwa kupoteza wanyama wa Lamoni.

Alma 17:25–28; Alma 18:7

Amoni

Amoni alijua hii ilikuwa ni fursa ya kuonyesha nguvu za Bwana. Amoni aliwaambia watumishi wengine wasiwe na wasiwasi na aliwasaidia kuipata mifugo iliyopotea.

Alma 17:29–32

Amoni anashikilia kombeo la ngozi na anawanyooshea wanyang’anyi

Wanyang’anyi walirudi tena kuitawanya mifugo. Lakini wakati huu, Amoni aliwaambia watumishi wengine wabaki kuichunga mifugo isitawanyike.

Alma 17:33

Amoni anasimama mbele ya wanyang’anyi

Amoni alienda kuwazuia wanyang’anyi wasiwatawanye kondoo. Wanyang’nyi hawakumwogopa Amoni. Walifikiri walikuwa na nguvu zaidi kuliko yeye. Lakini hawakujua kwamba Bwana alikuwa anamsaidia Amoni.

Alma 17:34–35

Amoni anawatupia wanyang’anyi jiwe kwa kombeo

Amoni aliwatupia wanyanganyi mawe kwa kombeo lake. Baadhi yao walikufa. Hii iliwafanya wanyang’anyi wengine kukasirika, walitaka kumuua Amoni. Walistaajabu kwa sababu hawakuweza kumpiga Amoni kwa mawe yao. Hawamkutarajia kuwa ana nguvu kama hivyo.

Alma 17:36

Amoni anautwaa upanga wake wakati wanyang’anyi wakitumia marungu

Wanyang’anyi walijaribu kumpiga Amoni na marungu yao. Lakini kila wakati walipojaribu, Amoni alikata mikono yao kwa upanga wake ili kwamba wasiweze kupigana tena. Punde, wakaingiwa na woga sana kuendelea kupigana na wakakimbia.

Alma 17:37–39

Watumishi wawili wanamwelezea Mfalme Lamoni kile kilichotokea

Watumishi walimwambia Lamoni jinsi Amoni alivyookoa mifugo. Lamoni alishangaa. Alidhania Amoni alikuwa Roho Mkuu, ambaye alikuwa na nguvu kubwa na anajua vitu vyote.

Alma 18:1–5, 18

Mfalme Lamoni anaonekana kuwa na wasiwasi

Lamoni alitaka kuzungumza na Amoni, lakini alikuwa pia na wasiwasi.

Alma 18:8–11

Amoni anapiga magoti mbele za Mfalme Lamoni

Amoni alienda kumuona Lamoni, lakini Lamoni hakujua nini cha kusema. Bwana alimsaidia Amoni kujua mawazo ya Lamoni. Amoni alisema kwamba yeye hakuwa Roho Mkuu. Alimwambia Lamoni kwamba Roho Mkuu ni Mungu. Lamoni alitaka kujifunza zaidi kuhusu Mungu.

Alma 18:12–28

Amoni anazungumza na Mfalme Lamoni

Amoni alisema kwamba Mungu aliumba ulimwengu na kila mtu aliye ndani yake. Kisha Amoni akamwambia Lamoni kwamba Mungu ana mpango wa wokovu. Kama sehemu ya mpango huo, Yesu Kristo angekuja. Lamoni aliamini kile ambacho Amoni alisema. Lamoni alisali na kumuomba Mungu awe na rehema juu yake na watu wake.

Alma 18:24–36, 39–42