Hadithi za Maandiko
Kaka Nefi na Lehi


“Kaka Nefi na Lehi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Helamani 3–6

Kaka Nefi na Lehi

Kusikia sauti kutoka mbinguni

kaka Nefi na Lehi wanawafundisha watu, na jeshi la Walamani liko karibu

Nefi na Lehi walikuwa ndugu ambao walitaka kila mmoja kujua kuhusu injili ya Yesu Kristo. Wanefi na Walamani walikuwa vitani, lakini ndugu hawa bado waliwafundisha watu kutoka kwenye makundi haya mawili. Siku moja walikuwa wanasafiri kwenda kuwafundisha watu, jeshi la Walamani liliwatupa gerezani.

Helamani 3:20–21, 37; 4:4–5, 14; 5:4–21

Jeshi la Walamani linatembea kuelekea gerezani walipokuwa Nefi na Lehi

Siku nyingi baadaye, jeshi lilikuja gerezani ili kuwaua Nefi na Lehi.

Helamani 5:22

duara la moto na mwanga unawalinda Nefi na Lehi, askari wanaanguka chini, na wingu jeusi linatokea

Kabla ya yeyote kuweza kuwadhuru Nefi na Lehi, duara la moto lilitokea likawazunguka. Moto ule haukuwaunguza. Badala yake, Mungu aliwaweka salama. Kisha ardhi ikatetemeka. Ilikuwa kama kuta za gereza zilitaka kubomoka. Punde, wingu la giza likamfunika kila mtu ndani ya gereza. Watu walikuwa na hofu sana.

Helamani 5:23–28

Watu wanasimama ndani ya wingu la giza wakitazama mwale wa mwanga

Sauti ilitoka juu ya wingu la giza. Ilikuwa ya utulivu, kama mnong’ono, lakini watu waliihisi katika mioyo yao. Ilikuwa ni sauti ya Mungu. Mungu aliwaambia watubu.

Helamani 5:29–30, 46–47

wanaume na wanawake wanatazama juu kupitia mpasuko wa mawingu ya giza

Ardhi na kuta za gereza kutetemeka zaidi. Sauti ikarejea tena na kuwaambia watu watubu. Watu hawangeweza kutembea kwa sababu ya lile wingu na uoga wao.

Helamani 5:31–34

Aminadabu anawanyoshea kidole Nefi na Lehi, ambao walikuwa wanang’ara na kutazama juu

Mtu mmoja kwenye umati ule wa watu aliitwa Aminadabu. Kwa wakati fulani alikuwa wa Kanisa la Mungu. Aliona kwamba nyuso za Nefi na Lehi zilianza kung’ara sana. Walionekana kama malaika. Ilionekana kwamba walikuwa wanazungumza na mtu fulani mbinguni. Aminadabu alimwambia kila mmoja awatazame Nefi na Lehi.

Helamani 5:35–39

wanaume na wanawake wengi wanatazama juu kupitia mawingu ya giza na kusali

Watu walimuuliza Aminadabu wanaweza kufanya kitu gani ili kuondoa lile giza. Aminadabu alishiriki kile alichojua kuhusu Mungu na Yesu. Aliwaambia watu watubu, wawe na imani katika Yesu, na wasali kwa Mungu. Watu walimsikiliza Aminadabu. Walisali mpaka giza likatoweka.

Helamani 5:40–42

watu wanasali huku wamezungukwa na mwanga na moto

Moto kutoka kwa Mungu uliwazunguka watu wote na haukuwaunguza. Watu walijawa na Roho Mtakatifu na walikuwa na furaha sana. Walisema mambo ya kustaajabisha. Ile sauti ikaja tena. Iliwaambia wawe na amani kwa sababu ya imani yao katika Yesu. Malaika walikuja na kuzungumza na watu.

Helamani 5:43–49

Nefi na Lehi wanaondoka gerezani, na watu wanatazama

Nefi, Lehi na watu wote waliondoka gerezani. Waliwaambia watu wengi kote nchini ambao walikuwa wameona na kusikia siku ile. Wengi wa Walamani waliwaamini na wakachagua kumfuata Yesu. Waliacha kupigana vitani. Badala yake, waliwasaidia watu kuwa na imani katika Yesu na kutubu.

Helamani 5:50–52; 6:1–6