Scripture Stories
Lehi na Saria Wanaondoka Yerusalemu


“Lehi na Saria Wanaondoka Yerusalemu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Lehi na Saria Wanaondoka Yerusalemu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

1 Nefi 1–2

Lehi na Saria Wanaondoka Yerusalemu

Onyo la Bwana kwa familia

Picha
ono la Bwana

Lehi na Saria waliishi Yerusalemu pamoja na watoto wao. Lehi aliona ono kutoka kwa Bwana. Aliona kwamba Mwokozi atakuja ulimwenguni siku moja. Bwana pia alimwonyesha kwamba Yerusalemu itaangamizwa.

1 Nefi 1:4–18

Picha
Lehi akizungumza na watu wenye hasira

Lehi aliwaambia watu kuhusu ono lake. Aliwaambia kwamba Yesu Kristo angekuja siku moja kuuokoa ulimwengu.

1 Nefi 1:18–19

Picha
ono la majengo yaliyobomolewa

Lehi pia aliwaambia watu kwamba Yerusalemu itaangamizwa. Aliwaomba watubu.

1 Nefi 1:14, 18–19

Picha
watu walio kasirika

Watu walikasirika. Bwana alisema tena na Lehi katika ndoto. Lehi alijifunza kwamba yeye na familia yake hawatakuwa salama Yerusalemu. Ilibidi waondoke.

1 Nefi 1:19–20; 2:1–2

Picha
familia ikiondoka jijini

Lehi na Saria walimtii Bwana. Waliondoka jijini pamoja na familia yao. Lehi na Saria walikuwa na wana wanne walioitwa Lamani, Lemueli, Samu, na Nefi. Ilibidi waache nyumba yao na vitu vyao vizuri.

1 Nefi 2:3–5

Picha
familia ikisafiri

Familia ilisafiri nyikani karibu na Bahari ya Shamu. Lehi alimshukuru Bwana kwa kuibariki familia yake. Alifundisha familia yake kumfuata Bwana na kushika amri Zake.

1 Nefi 2:5–10

Picha
familia ikiwa jangwani

Lamani na Lemueli walinung’unika. Walikosa nyumba yao na vitu vyote walivyoviacha nyuma. Hawakuelewa kwa nini Bwana aliwataka kuondoka. Hawakuamini jiji kubwa kama Yerusalemu lingeweza kuangamizwa.

1 Nefi 2:11–13

Picha
Lamani na Lemueli

Lamani na Lamueli walifikiri kwamba Lehi alikuwa anawaza maono yake. Ingekuwaje kama familia yao ingepotea nyikani milele?

1 Nefi 2:11

Picha
Nefi

Nefi alitaka kujua yeye mwenyewe kwamba kile Lehi alichosema kilikuwa kweli. Alisali na alimwuliza Bwana.

1 Nefi 2:16

Picha
Nefi

Baba alimtuma Roho Mtakatifu kumsaidia Nefi kuamini maneno ya baba yake. Nefi alimwamini Bwana na alishiriki kile alichojifunza na kaka zake. Samu alimsikiliza Nefi na kumwamini, lakini Lamani na Lemueli hawakusikiliza.

1 Nefi 2:16–18

Chapisha