Hadithi za Maandiko
Mfalme wa Walamani Wote


“Mfalme wa Walamani Wote,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Mfalme wa Walamani Wote,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

Alma 20; 22–23

Mfalme wa Walamani Wote

Kutaka kujifunza kuhusu Bwana

mfalme ana hasira kali kwa Lamoni na Amoni

Walamani walikuwa na mfalme ambaye alitawala juu ya wafalme wao wengine wote. Alikuwa baba wa Mfalme Lamoni. Alifikiri Wanefi walikuwa adui Siku moja aliwaona Lamoni na Amoni Mfame alimwuliza Lamoni alikuwa anafanya nini Mnefi. Lamoni alimwamba mfalme kwamba walikuwa wanakwenda kuwaweka huru ndugu wa Amoni kutoka gerezani.

Mosia 10:11–17; Alma 20:1–12

mfalme akiongea

Mfalme alikasirika. Alifikiri Wanefi walikuwa wanadanganya kujaribu kuiba kutoka kwa Walamani. Alimwambia Lamoni amuuwe Amoni na aje na yeye.

Alma 20:13–14

Lamoni akiongea

Lamoni hangeweza kumuua Amoni Alimwambia mfalme kwamba Amoni na ndugu zake walikuwa manabii wa Mungu. Alisema atawasaidia kaka za Amoni.

Alma 20:15

mfalme na Amoni wakipigana

Mfalme aliutoa upanga wake kumuumiza Lamoni, lakini Amoni akamzuia. Mfalme badala yake akamshambulia Amoni. Amoni akajilinda. Akaumiza mkono wa mfalme ili mfalme asiweze kupigana. Mfalme akaogopa kwa sababu ya jinsi Amoni alivyokuwa na nguvu. Aliahidi kumpa Amoni nusu ya ufalme wake kama Amoni angemwacha aishi.

Alma 20:16–23

Amoni akiongea na mfalme

Amoni hakutaka ufalme. Badala yake, alimwomba mfalme kuwaachia huru ndugu zake kutoka gerezani. Pia alimwomba mfalme kuacha kuwa na hasira na Lamoni. Amoni alisema mfalme anapaswa kumwacha Lamoni atawale kwa njia alifikiri ilikuwa nzuri sana.

Alma 20:24

mfalme akifikiria

Mfalme alishangazwa kuhusu jinsi Amoni alivyompenda sana Lamoni. Alikubali kufanya kila kitu Amoni alichoomba.

Alma 20:25–27

mfalme akiwa na furaha na akiongea na Lamoni na Amoni

Mfalme alitaka kujifunza zaidi kuhusu kile Amoni na Lamoni walimwambia kuhusu Mungu. Aliomba Amoni na kaka zake waje kumfundisha.

Alma 20:27

Amoni na Lamoni wakiwasaidia kaka zake Amoni

Amoni na Lamoni walikwenda nchi ya Midoni. Kaka za Amoni walikuwa gerezani pale. Walikuwa wamefungwa na kamba na hawakupewa chakula au maji. Lamoni alimshawishi mtawala wa Midoni kuwaacha huru kaka za Amoni.

Alma 20:28–30

Haruni akipiga magoti mbele ya mfalme

Mara walipokuwa huru, ndugu wa Amoni walikwenda kwa baba wa Lamoni. Walimsujudia mfalme na kuomba kuwa watumishi wake. Mfalme alisema hapana. Badala yake, aliwataka wamfundishe kuhusu injili. Mmoja wa kaka hao aliitwa Haruni. Alisoma maandiko kwa mfalme na alimfundisha kuhusu Mungu na Yesu Kristo.

Alma 22:1–14

Haruni na mfalme wakisali

Mfalme alimwamini Haruni. Alisema angeuacha ufalme wake wote umjue Mungu. Alimuuliza Haruni nini alihitaji kufanya. Haruni alimwambia mfalme atubu na aombe kwa Mungu kwa imani. Mfalme alitubu dhambi zake zote na aliomba.

Alma 22:15–18

mfalme akianguka sakafuni

Mfalme alianguka chini. Watumishi wa mfalme walikimbia kumwambia malkia.

Alma 22:18–19

malkia amekasirika sana

Malkia alikuja na kumwona mfalme ardhini. Alifikiri Haruni na ndugu zake wamemuua mfalme. Malkia alikasirika.

Alma 22:19

malkia akimuota Haruni kwa kidole.

Malkia aliwaambia watumishi wamuue Haruni na kaka zake. Lakini watumishi waliogopa. Walisema Haruni na kaka zake walikuwa wana nguvu mno. Sasa malkia alikuwa na hofu. Aliwatuma watumishi kuwaeleza watu ndani ya jiji nini kimetokea. Alitegemea watu watawaua Haruni na kaka zake.

Alma 22:19–21

Haruni akimsaidia mfalme kusimama

Haruni alijua watu wangekasirika. Pia alijua mfalme hakuwa amekufa. Alimsaidia mfalme kusimama wima. Mfalme alirudishiwa nguvu zake na alisimama. Malkia na watumishi walishangaa.

Alma 22:22–23

mfalme akiwafundisha malkia na watumishi

Mfalme aliwafudisha malkia na watumishi kuhusu Yesu. Wote waliamini katika Yesu. Mfalme alitaka watu wake wote kujifunza kuhusu Yesu. Aliweka sheria kwamba Haruni na ndugu zake wangefundisha injili popote katika ufalme wake. Waliwafundisha watu na waliita makuhani na waalimu nchini.

Alma 22:23–27; 23:1-4