Scripture Stories
Imani ya Malkia


“Imani ya Malkia,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Imani ya Malkia,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

Alma 18–19

Imani ya Malkia

Kupata Shangwe katika Yesu Kristo

Picha
mume wa malkia akianguka sakafuni

Malkia Mlamani alitawala pamoja na mume wake, Mfalme Lamoni. Mfalme alimwomba Mnefi aliyeitwa Amoni kumfundisha kuhusu Bwana. Mfalme aliamini kile Amoni alichomwambia. Mfalme alipiga magoti kusali na alimwomba Bwana amsamehe. Alipokuwa anasali, mfalme alianguka ardhini. Ilionekana kana kwamba alikuwa amekufa.

Alma 18:21, 24–42

Picha
malkia akimwangalia mume wake aliyeanguka

Watumishi wa mfalme walimpeleka kwa malkia. Walimlaza kwenye kitanda chake Alilala pale na hakusogea kwa siku mbili mchana na usiku.

Alma 18:43

Picha
malkia akizungumza na mtumishi

Wakati ule, malkia na watoto wake walikuwa na huzuni sana. Walikaa na mfalme na walimlilia. Baadhi ya watu walisema mfalme anapaswa kuzikwa. Lakini malkia alitaka kuzungumza na Amoni kwanza. Alisikia kwamba alikuwa na nguvu za Mungu. Watumishi wa malkia walimwomba Amoni kwenda kwa malkia.

Alma 18:43; 19:1–3, 5

Picha
malkia akiongea na Amoni

Malkia alimwambia Amoni kuwa alisikia ya kuwa yeye alikuwa nabii wa Mungu. Alimwomba Amoni kwenda kumwona mfalme Amoni alijua mfalme alikuwa hai. Ilikuwa ni nguvu ya Mungu, ambayo ilisababisha mfalme alale. Amoni alimwambia malkia kwamba mume wake ataamka siku inayofuata.

Alma 19:3–8

Picha
malkia akipumzisha kichwa chake juu ya mume wake.

Malkia alimwamini Amoni na alikuwa na imani kubwa katika Mungu. Aliiamini mume wake ataamka siku ifuatayo. Amoni alisema alibarikiwa kwa sababu ya imani yake kubwa. Alimwambia malkia alikuwa na imani zaidi kuliko waliyokuwa nayo watu wake mwenyewe. Malkia alikaa karibu na akamtunza mume wake usiku kucha.

Alma 19:9–11

Picha
malkia akifurahi mumewe aliamka

Siku iliyofuata, mfalme aliamka. Alimwambia malkia kwamba amemwona Yesu Kristo. Malkia na mfalme walijua kiasi gani Yesu aliwapenda, na walijawa na shangwe.

Alma 19:12–13

Chapisha