“Kijakazi Mnefi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Kijakazi Mnefi
Anasaidia kulinda watu wake
Kijakazi alimfanyia kazi kiongozi Mnefi aliyeitwa Moriantoni. Moriantoni alikuwa anasababisha vurugu miongozi mwa watu. Alikishambulia kikundi cha Wanefi na kujaribu kutwaa nchi yao. Kisha alipanga kusafiri kwenda kaskazini pamoja na watu wake ili kutwaa nchi huko.
Siku moja, Moriantoni alimkasirikia kijakazi. Alimtendea vibaya sana na kumuumiza. Kijakazi alitoroka na kukimbilia kwenye kambi ya Kapteni Moroni. Alimwambia Moroni kuhusu mambo mabaya ambayo Moriantoni alifanya. Moroni alimwamini kijakai huyo.
Kijakazi yule pia alisema kwamba Moriantoni alitaka kuondoka na kutwaa nchi iliyokuwa huko kaskazini. Moroni alipata hofu. Wanefi wangeweza kuwa katika hatari kama Moriantoni angetwaa nchi iliyopo kaskazini. Hiyo ingeweza kusababisha watu kupoteza uhuru wao.
Moroni alituma jeshi kumzuia Moriantoni. Watu wa Moriantoni walipigana na jeshi na wakashindwa. Waliahidi kudumisha amani na kurudi katika nchi yao. Kwa sababu kijakazi alimuonya Moroni, miji ya Wanefi ilibakia kuwa salama.