“Mfalme Nuhu na Mfalme Nuhu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Mfalme Nuhu na Mfalme Limhi
Kutoroka kutoka kwa Walamani
Mfalme Nuhu alitawala kundi la Wanefi. Alifanya mambo mengi mabaya, na baadhi ya watu walimkasirikia sana. Mtu aliyeitwa Gidioni alipigana na Nuhu kwa upanga. Nuhu alikimbia na kupanda mnarani. Kutoka kwenye mnara, aliona jeshi la Walamani likija. Nuhu alijifanya alikuwa anawaogopa watu wake, kwa hiyo Gidioni alimwacha aishi.
Nuhu na watu wake wanakimbilia mbali. Lakini Walamani waliwafukuza na wakaanza kuwashambulia. Nuhu aliwaambia wanaume waache familia zao na waende pamoja naye.
Baadhi ya wanaume waliondoka na Nuhu. Lakini wengi wa wanaume walichagua kubaki pamoja na familia zao. Limhi mwana wa Nuhu pia alichagua kubaki.
Mabinti wengi walisimama mbele ya jeshi na kuwaomba Walamani wasiziumize familia zao. Walamani waliwasikiliza mabinti wale na wakawaacha Wanefi waishi. Badala yake, Walamani waliwateka Wanefi.
Wanaume ambao walikimbia walitaka kurudi kwa familia zao. Nuhu alijaribu kuwazuia, kwa hiyo walimuua. Kisha wakarudi kwa familia zao.
Wanaume walikuwa na furaha sana kwamba familia zao zilikuwa salama. Walimwambia Gidioni kile kilichomtokea Nuhu.
Watu wanamchagua Limhi kuwa mfalme wao mpya. Limhi alimwahidi mfalme Mlamani kwamba wangewalipa Walamani nusu ya kila kitu walichomiliki. Kama malipo, mfalme wa Walamani aliahidi hangewaumiza watu wa Limhi.
Waliishi kwa amani kwa miaka kadhaa. Kisha Walamani wakaanza kuwatendea watu wa Limhi vibaya. Watu walitaka kuwa huru tena. Walijaribu kupigana na Walamani, lakini walishindwa. Watu walisali kwa Mungu kwa ajili ya msaada.
Siku moja, Mnefi mmoja aliyeitwa Amoni alimtembelea Limhi na watu wake. Amoni alitokea nchi iliyoitwa Zarahemla. Limhi alikuwa na furaha kumwona Amoni.
Amoni angewaongoza watu wa Limhi hadi Zarahemla, lakini iliwabidi watoroke kutoka kwa Walamani kwanza. Gidioni alikuwa na mpango.
Usiku, Gidioni aliwapa walinzi Walamani kileo zaidi ili kuwafanya walale. Wakati walinzi wamelala, Limhi na watu wake waliutoroka mji. huo
Walienda hadi Zarahemla na kuungana na Wanefi huko. Limhi na watu wake walijifunza zaidi kuhusu Mungu. Walifanya agano, au ahadi maalumu, kumtumikia Mungu na kutii amri Zake. Walibatizwa na kuwa sehemu ya Kanisa la Mungu. Walikumbuka kwamba Mungu aliwasaidia kutoroka kutoka kwa Walamani.