Scripture Stories
Teankumu na Moroni


“Teankumu na Moroni,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 62

Teankumu na Moroni

Kuonyesha ujasiri mkubwa

Picha
Amoroni pamoja na jeshi la Walamani wakipigana na jeshi la Wanefi

Baada ya Amalikia kufa, kaka yake Amoroni akawa mfalme wa Walamani. Amoroni aliendelea kupigana na Wanefi. Vita viliendelea kwa miaka mingi. Wanefi walianza kushinda, kwa hiyo majeshi yote ya Walamani yalikimbilia kwenye mji mmoja. Moroni, Teankumu na kapteni mwingine Mnefi walitembea wakiwafuata Walamani pamoja na majeshi yao.

Alma 52:3–4; 54:16–24; 62:12–35

Picha
Teankumu anashikilia mkuki na anakaribia mji usiku

Teankumu alikuwa amekasirika kwamba Amalikia na Amoroni walikuwa wamesababisha vita kubwa, na ndefu. Kwa sababu ya vita, watu wengi walikuwa wamekufa na kulikuwa na chakula kidogo sana. Teankumu alitaka kumaliza vita vile. Alienda ndani ya mji usiku akimtafuta Amoroni.

Alma 62:35–36

Picha
Teankumu anashikilia kamba yenye kiopoo na anaruka ukuta

Teankumu alipanda juu ya ukuta wa mji. Alienda kutoka mahali hadi mahali katika mji mpaka alipopata pale ambapo Amoroni alikuwa amelala.

Alma 62:36

Picha
Teankumu anasimama kwenye mlango wa hema akiwa na mkuki na kamba.

Teankumu alimtupia mkuki Amoroni. Mkuki ule ulimchoma karibu na moyo. Lakini Amoroni aliwaamsha watumishi wake kabla hajafa.

Alma 62:36

Picha
Teankumu anakabiliana na askari Walamani wakiwa na mikuki

Watumishi wa Amoroni walimfukuza Teankumu na kumuua. Viongozi wengine wa Wanefi walihuzunika sana kwa kifo cha Teankumu. Alikuwa amepigana kwa ujasiri kwa ajili ya uhuru wa watu wake.

Alma 62:36–37

Picha
Askari Wanefi wanawateka askari Walamani

Ingawa yeye alikuwa amekufa, Teankumu alikuwa amewasaidia Wanefi kushinda vita ile. Alisababisha Walamani wampoteze kiongozi wao. Asubuhi iliyofuata, Moroni alipigana na Walamani na akashinda. Walamani waliondoka kwenye nchi ya Wanefi na vita viliisha.

Alma 62:37–38

Picha
Kapteni Moroni anawaelekeza wanaume kujenga kijiji, na familia zinatazama

Kulikuwa na amani hatimaye. Moroni alifanya kazi kwa bidii ili kufanya nchi ya Wanefi kuwa salama zaidi dhidi ya Walamani. Kisha Moroni alienda nyumbani na kuishi kwa amani. Manabii walifundisha injili na kuongoza Kanisa la Mungu. Watu walimtumainia Bwana na Yeye aliwabariki.

Alma 62:39–51

Chapisha