Hadithi za Maandiko
Alma na Amuleki Gerezani


“Alma, Amuleki Gerezani,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 14.

Alma na Amuleki Gerezani

Imani katika Bwana wakati wa nyakati ngumu

Alma na Amuleki wakiwa na walinzi

Alma na Amuleki walifundisha injili katika mji wa Amoniha. Baadhi ya watu waliamini katika Bwana na kutubu. Lakini watu wengine wengi waliwakasirikia Alma na Amuleki na walitaka kuwaangamiza. Watu waliokasirika walimfunga Alma na Amuleki na wakawapeleka wanaume hawa wawili kwa mwamuzi mkuu wa mji.

Alma 8:29–30; 14:1–4

Alma na Amuleki wakiwa wamefungwa mikono

Mwamuzi mkuu hakuamini kwamba watu wake walihitaji kutubu. Watu walimkasirikia Alma na Amuleki. Waliwafanya wanaume walioamini kile ambacho Alma na Amuleki walikifundisha waondoke mji huo. Kisha waliwatupa wanawake na watoto ambao waliamini katika Bwana katika moto.

Alma 14:3, 5–9, 14, 16

Amuleki na Alma wanaonekana kuwa na huzuni

Amuleki alikuwa na huzuni sana wakati alipoona watu wakiwa katika maumivu. Alimuomba Alma atumie nguvu za Mungu ili kuwaponya wale watu. Lakini Alma alisema Roho wa Mungu hangeweza kumruhusu. Alimwambia Amuleki kwamba wanawake na watoto wangekuwa pamoja na Bwana. Bwana angewahukumu watu walio waua watu wale.

Alma 14:9–11

mwamuzi mkuu akicheka

Mwamuzi mkuu aliwadhihaki Alma na Amuleki kwa sababu Bwana hakuwalinda wale wanawake na watoto. Aliwapeleka Alma na Amuleki gerezani.

Alma 14:14–17

Alma na Amuleki gerezani

Baada ya siku tatu, mwamuzi mkuu alienda gerezani pamoja na makuhani wa uongo. Waliuliza maswali mengi. Lakini Alma na Amuleki hawakuwajibu.

Alma 14:18–19

mwamuzi mkuu akiwacheka Alma na Amuleki gerezani

Mwamuzi mkuu na makuhani wake walifanya mambo ya ukatili kwa Alma na Amuleki. Wao pia hawakuwapa Alma na Amuleki chakula cho chote au maji. Na walidhihaki kile ambacho Alma na Amuleki walikuwa wamefundisha.

Alma 14:19–22

Amuleki na Alma wakiwa wamefungwa na mwamuzi mkuu akiwa kando

Alma na Amuleki waliteseka kwa siku nyingi. Mwamuzi mkuu alikuja mara nyingine na makuhani wake. Aliwaambia Alma na Amuleki kwamba kama walikuwa na nguvu za Mungu, wanapaswa kukata kamba ambazo zimewafunga. Kisha yeye angewaamini.

Alma 14:23–24

Amuleki na Alma wanasimama

Alma na Amuleki walihisi nguvu za Mungu. Walisimama. Alma alikuwa na imani katika Bwana na akaomba nguvu za kukata kamba.

Alma 14:25–26

kamba zikikatika

Alma na Amuleki walikata kamba. Mwamuzi mkuu na makuhani wake waliogopa. Walijaribu kukimbia, lakini kisha ardhi ilianza kutetemeka.

Alma 14:26–27

Amuleki na Alma juu ya gereza lililoharibiwa

Kuta za gereza zilimwaangukia mwamuzi mkuu na makuhani wake, na wakafa. Lakini Bwana aliwaweka Alma na Amuleki salama. Watu walisikia sauti ile, walikimbia kuona ni nini kilikuwa kimetokea. Ilikuwa ni Alma na Amuleki wakitembea kutoka kwenye gereza. Watu waliwaogopa sana Alma na Amuleki kiasi kwamba waliwakimbia.

Alma 14:27–29