Hadithi za Maandiko
Gidioni, Alma, na Nehori


“Gidioni, Alma, na Nehori,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Gidioni, Alma, na Nehori.” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

Alma 1

Gidioni, Alma, na Nehori

Kutetea ukweli kwa maneno ya Mungu

Alma Mdogo akimsikiliza Baba yake

Wanefi walimchagua Alma Mdogo kuwa mwamuzi wao mkuu. Alma pia alikuwa kuhani mkuu wa Kanisa.

Mosia 29:41-44

Nehori akionesha kwa kidole angani

Mtu aliyeitwa Nehori alianza kuwafundisha watu kitu alichoita neno la Mungu. Lakini alifundisha watu kwamba hawakuhitaji kumtii Mungu au kutubu.

Alma 1:2–4, 15

watu wakimleta Nehori pesa

Watu wengi walimpenda na kuamini kile Nehori alichosema. Aliwataka watu wampe pesa na kumsifu. Alifikiri kuwa alikuwa bora zaidi kuliko watu wengine. Alitengeneza kanisa lake mwenyewe, na watu wengi walimsikiliza yeye.

Alma 1:3, 5–6

Nehori akibishana na Gidioni

Siku moja, Nehori alkutana na mtu mzee aliyeitwa Gidioni. Gidioni alikuwa mwalimu katika Kanisa la Mungu na alikuwa amefanya mengi yaliyo mazuri. Nehori alitaka watu waondoke Kanisani, kwa hiyo alibishana na Gidioni. Gidioni alitumia maneno ya Mungu ili kuonesha kwamba Nehori hakuwa anafundisha ukweli. Nehori alikasirika sana! Alimuua Gidioni kwa upanga wake.

Alma 1:7–9, 13

Nehori akibishana na Alma

Watu walimchukuwa Nehori kwa Alma ili ahukumiwe. Nehori alijaribu kutetea kile alichokifanya. Hakutaka kuadhibiwa.

Alma 1:10–11

Alma akitoa hukumu

Alma alisema kwamba mafundisho ya Nehori yalikuwa sio sahihi na yangeweza kuwaumiza watu. Alma alifuata sheria. Kwa sababu Nehori alimuua Gidioni, Nehori naye aliuawa,

Alma 1:12–15

Alma akifikiri kuhusu watu

Kabla hajafa, Nehori aliwaambia watu kwamba alikuwa amedanganya. Hakuwa amefundisha neno la Mungu. Hata hivyo Nehori alisema alikuwa amekosa, watu wengi walifuata mfano wake. Walidanganya kwa watu ili kupata sifa na pesa. Lakini watu wengine walimsikiliza Alma. Waliwatunza masikini na kushika amri za Mungu.

Alma 1:15–16, 25–30