Scripture Stories
Wanawake Nyikani


“Wanawake Nyikani,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

1 Nefi 16–17

Wanawake Nyikani

Kutembea na Bwana

Picha
wanawake wakifanya kazi

Mabinti wa Ishmaeli walisafiri na familia yao nyikani. Safari ilikuwa ngumu. Baada ya muda fulani, waliolewa na wana wa Lehi na Saria.

1 Nephi 16:7; 17:1

Picha
mabinti wenye huzuni karibu na kaburi la Ishmael

Siku moja, Ishmaeli alikufa. Mabinti zake walihuzunika sana. Walimkosa baba yao. Mabinti walikuwa na wasiwasi kwamba wao na familia zao watakufa pia nyikani Walifadhahishwa na Lehi na Nefi, na walitaka kurudi nyumbani Yerusalemu.

1 Nefi 16:34–36

Picha
Akina dada wakifarijiana wao kwa wao.

Sauti ya Bwana ilisema kwa mabinti wa Ishmaeli na familia zao. Walitubu na Bwana akawabariki.

1 Nefi 16:39

Picha
Saria pamoja na watoto wadogo

Wanawake walipata watoto nyikani. Saria pia alipata wana wawili zaidi, Yakobo na Yusufu.

1 Nephi 17:1; 18:7

Picha
familia zikisafiri

Bwana aliwasaidia wanawake kwenye safari yao. Aliwabariki wakawa na maziwa mengi kwa ajili ya watoto wao. Aliwasaidia wanawake wakawa wenye nguvu zaidi walipokuwa wanasafiri.

1 Nefi 17:1–3

Picha
akina mama na watoto ndani ya hema.

Bwana alisema kwamba Yeye alikuwa anawaongoza mabinti na familia zao kwenda nchi ya ahadi. Bwana aliahidi familia kwamba watakuwa na vyote ambavyo walivihitaji wanapokuwa wanasafiri. Alikifanya chakula walichowinda kiwe kizuri kwa kula, na aliwaongoza.

1 Nefi 17:35, 12–14

Picha
familia kwenye ufukwe wa bahari

Baada ya miaka minane nyikani, familia zilifika kwenye bahari. Wanawake walishangilia pamoja na familia zao. Ardhi karibu na bahari ilikuwa nzuri sana. Waliita mahali hapa Neema kwa sababu palikuwa pamejaa matunda na asali ya kula. Bwana alikuwa ametayarisha vyote kwa ajili yao.

1 Nefi 17:4–6

Chapisha