Hadithi za Maandiko
Miti ya Mizeituni


“Miti ya Mizeituni,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Yakobo 5–6

Miti ya Mizeituni

Upendo wa Mungu kwa watu Wake

picha ya miti ya mizeituni imeoneshwa wakati Yakobo anaposema.

Yakobo alikuwa nabii wa Mungu. Alitaka kuwafundisha Wanefi kuhusu kiasi gani Mungu anawapenda watu Wake. Yakobo aliwasimulia hadithi kuhusu shamba la miti ya mizeituni. Bwana wa shamba la mizabibu na watumishi Wake walifanya kazi pamoja kutunza shamba la mizabibu

Yakobo 5:1–4, 7; 6:4–5

Bwana wa shamba la mizabibu anachimba na sepetu karibu na mti wa mizeituni

Bwana alikuwa na mti maalumu wa mizeituni ambao ulizaa matunda mazuri. Yakobo alisema kwamba mti huu ulikuwa kama watu wa Mungu, au nyumba ya Israeli. Tunda lilikuwa kama matendo ya watu. Bwana aliutunza sana mti huu. Aliusaidia kukua kwa kuilisha mizizi yake na kupogoa matawi yake. Aliupa kile ilichohitaji ili kuishi.

Yakobo 5:1–3, 5; 6:1,7

mti wa mizeituni unaanza kufa

Baada ya muda, mti Wake maalumu ulianza kufa. Kulikuwa na matawi machache tu yenye afya. Hii ilimfanya Bwana ahuzunike. Aliutaka uendelee kuzaa matunda mazuri.

Yakobo 5:3, 6–8

Bwana wa shamba la mizabibu, anakata na kuondoa tawi lenye afya.

Kuokoa matawi yenye afya, Bwana aliyaondoa na akayapachika kwenye miti mingine. Kisha aliyabadilisha na matawi yenye afya kutoka miti mingine.

Yakobo 5:7–14

Bwana wa shamba la mizabibu na watumishi wanaitumza miti ya mizeituni

Muda mrefu ulipita. Bwana na mtumishi walikuja kwenye shamba la mizabibu mara kwa mara. Waliutunza mti maalumu wa Bwana. Pia walitunza matawi maalumu ambayo yalikuwa yametawanyika katika miti sehemu yote ya shamba ya mizabibu. Karibu matunda yote ambayo yalikuwa mazuri Matunda mazuri yalimfanya Bwana na mtumishi Wake wafurahi.

Yakobo 5:15–29, 31

Bwana wa shamba akizungumza na mtumishi kuhusu miti ya mizeituni

Baada ya muda fulani, kila mmoja wa miti ulizaa matunda zaidi. Lakini sasa matunda yote yalikuwa mabaya. Bwana alihuzunuka sana. Hakutaka kupoteza shamba Lake la mizabibu au matunda yake! Alifanya kazi kwa nguvu kuisaidia miti Yake. Alishangaa nini kingine angeweza kufanya. Aliongea na mtumishi na alichagua kuendelea kujaribu.

Yakobo 5:29–51

kibarua anakata na kuondoa tawi lenye afya

Ili kuokoa shamba lake, Bwana aliwaambia wakusanye matawi aliyoyapogoa kutoka mti ule maalumu. Alisema wayapachike kwenye mti maalumu tena.

Yakobo 5:51–60

matawi yenye afya yamepachikwa kwenye mti tofauti wa mzeituni

Hii ilikuwa “wakati wa mwisho” ambapo Bwana angefanya kazi katika shamba Lake. Aliwaita watumishi wengine ili kusaidia. Kila mmoja alifanya kazi pamoja ya kukusanya na kupachika matawi.

Yakobo 5:61–72

matawi ya mti wa mzeituni wenye afya na matunda.

Waliitunza miti yote. Waliondoa matawi mabaya na kuyaacha yale mazuri. Baada ya muda, mti maalumu wa Bwana ulizaa matunda mazuri tena. Miti mingine pia ilizaa matunda ambayo yalikuwa mazuri kama tunda la mti maalumu. Bwana alifurahi. Miti Yake iliokolewa! Yote ilizaa matunda Aliyoitaka iwe nayo.

Yakobo 5:73–75

Bwana wa shamba na watumishi wanaangalia miti mkubwa wa mizeituni wenye afya

Bwana aliwashukuru watumishi. Aliwaambia walikuwa wamebarikiwa kwa ajili ya kufanya kazi kwa bidii na kutii amri Zake. Alishiriki tunda pamoja nao, na iliwafanya wawe na furaha sana. Kwa muda mrefu, Bwana alilifurahia tunda lile.

Yakobo 5:75–77

picha ya Yesu Kristo ilionyeshwa wakati Yakobo alipokuwa akiongea

Yakobo alimaliza hadithi ile ya miti ya mizeituni. Aliwafundisha watu kwamba anawajali wao kama vile Bwana wa shamba la mizabibu alivyoijali miti Yake. Yakobo alimtaka kila mmoja kutubu na kujongea karibu zaidi na Mungu. Aliwafundisha kumpenda na kumtumikia Mungu kwa sababu Mungu siku zote anatafuta kuwasaidia.

Yakobo 6:1–5, 7 11