“Samweli Nabii,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Samweli Nabii
Kufundisha kuhusu kuzaliwa na kifo cha Yesu
Nabii Mlamani aliyeitwa Samweli alikwenda kuwafundisha Wanefi huko Zarahemla. Alifundisha kuhusu toba. Wanefi hawakumsikiliza na walimfukuza atoke nje ya mji.
Samweli alikuwa karibu kurudi kwa watu wake. Lakini Bwana alimwambia arudi kuwafundisha Wanefi.
Bwana alimwambia Samweli Yeye angemwambia nini cha kusema. Samweli alimtii Bwana. Alirudi Zarahemla. Lakini Wanefi hawakumruhusu kuingia mjini.
Samweli alipanda ukuta wa mji. Alisema vitu Ambavyo Bwana aliweka moyoni mwake. Aliwaonya watu wangeangamizwa kwa sababu walikuwa wanafanya mambo mabaya. Alisema kwamba toba na imani tu katika Yesu Kristo ingeweza kuwaokoa. Alisema Yesu, Mwana wa Mungu, angezaliwa ndani ya miaka mitano.
Helamani 13:4–11; 14:2, 8, 12–18
Samweli alisema kutakuwa na ishara za kuzaliwa kwa Yesu. Aliwaambia watu kutazamia ishara. Ishara moja itakuwa usiku bila giza. Ishara zingine zingekuwa kwamba nyota mpya na vitu vingi vya ajabu vingetokea angani.
Samweli alitaka watu wawe na imani katika Yesu. Alisema Yesu angekufa na kufufuka ili kwamba watu wote waweze kuokolewa kama watatubu.
Samweli alisema kutakuwa na ishara za kifo cha Yesu. Watu wasingeweza kuona jua, mwezi, au nyota. Hakungekuwa na nuru kwa siku tatu.
Kungekuwa na muungurumo na mwanga wa radi. Matetemeko ya ardhi yangekuja, na miji ingeharibiwa.
Baadhi ya watu walimwamini Samweli, lakini Wanefi wengi walimkasirikia. Walimrushia mawe na kumlenga kwa mishale. Bwana alimlinda Samweli alipokuwa amesimama ukutani. Hakuna hata mawe na mishale iliyoweza kumpiga.
Wakati hakuna mtu aliyeweza kumpiga Samweli, watu wengi zaidi waliamini maneno yake. Lakini watu wengi bado walikuwa na hasira. Walijaribu kumchukua Samweli na kumfunga. Samweli alitoroka na kwenda nyumbani. Aliendelea kuwafundisha watu wake.
Wanefi ambao walimwamini Samweli walitubu na kubatizwa na nabii Nefi. Walimwamini Yesu na kutazamia ishara za kuzaliwa kwa Yesu ambazo Samweli alikuwa amewaambia kuzihusu.