Hadithi za Maandiko
Alma Mdogo


“Alma mdogo,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Alma Mdogo.” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

Mosia 25–8; Alma 36

Alma Mdogo

Badiliko kuu

Mosia na Alma Mkubwa

Mfalme Mosia alimpa Alma nguvu kuongoza Kanisa katika Zarahemla. Alma aliwafundisha watu kutubu na kuwa na imani katika Bwana.

Mosia 25:19–24; 26

Alma Mdogo

Alma alikuwa na mwana ambaye pia aliitwa Alma. Alma Mdogo hakuamini kile baba yake alichofundisha.

Mosia 27:8

Alma Mdogo na wana wa Mosia wakizungumza na watu.

Mosia alikuwa na wana ambao hawakuamini katika Bwana. Walikuwa marafiki na Alma mdogo. Wote walitaka watu kuacha Kanisa. Alma na wana wa Mosia waliwaongoza watu wengi kufanya vitu ambavyo vikuwa kinyume na amri za Mungu.

Mosia 27:9–10; Alma 36:6

Alma Mdogo na wana wa Mosia wakimwogopa malaika

Siku moja Bwana alimtuma malaika kuwasitisha. Malaika aliwaambia waache kujaribu kuangamiza Kanisa. Alma na wana wa Mosia waliogopa sana walianguka chini.

Mosia 27:11–18; Alma 36:6–9

Alma Mdogo akiwa kwenye maumivu

Alma hakuweza kusema au kutembea kwa siku tatu mchana na usiku. Kwa kweli alijisikia vibaya kwa sababu ya vitu vyote vibaya alivyovifanya. Alikuwa pia na wasiwasi kwa sababu amewaongoza watu wengi mbali kutoka kwa Bwana.

Mosia 27:19; Alma 36:10–16

Alma Mdogo akipiga magoti

Alma alihisi maumivu makali sana kwa sababu ya dhambi zake. Kisha alimkumbuka baba yake akizungumza kuhusu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

Alma 36:17

Alma Mdogo mwenye furaha

Alma alisali ili Yesu amsamehe. Baada ya yeye kusali, hakuweza kukumbuka maumivu yake. Alijua Bwana alikuwa amemsamehe. Hakujisikia vibaya kuhusu dhambi zake tena. Badala yake, Alma alijisikia mwenye furaha sana.

Mosia 27:24–28; Alma 36:18–22

Alma Mdogo na wana wa Mosia wakimsaidia mtu fulani

Alma alirejewa na nguvu zake tena. Yeye na wana wa Mosia waliamua kutubu na kujaribu kurekebisha maumivu yote waliyoyasababisha. Walimtumikia Bwana kutoka wakati ule na kuendelea kwa kuwasaidia wengine kutubu Walisafiri kote katika nchi ambayo Mosia alitawala na waliwafundisha watu kuhusu Yesu.

Mosia 27:20–24, 32–37; Alma 36:23–26

wana wa Mosia wakiondoka

Alma na wana wa Mosia walitaka kushiriki shangwe ambayo mafundisho ya Yesu yalileta kwenye maisha yao. Walifanya kazi kwa bidii kumtumikia Mungu na watu. Wana wa Mosia walichagua kuondoka na kuwafundisha Walamani kuhusu Yesu. Alma alichagua kubaki na kuendelea kuwafundisha Wanefi.

Mosia 27:32–37; 28:1–10; 29:42–43