“Kapteni Moroni na Zerahemna,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Kapteni Moroni na Zerahemna
Vita na ahadi ya kuishi kwa amani
Zerahemna alikuwa kiongozi wa majeshi ya Walamani. Alitaka kuwatawala Wanefi na kuwafanya wawatumikie watu wake. Zerahemna aliongoza majeshi yake kuwashambulia Wanefi.
Wanefi walitaka kulinda nyumba zao, familia zao na dini yao. Walijua wasingeweza kumwabudu Bwana kama Walamani wangewatawala. Wanefi walichagua kupigana na maadui zao.
Mtu aliyeitwa Moroni alikuwa kapteni wa majeshi ya Wanefi. Moroni alihakikisha majeshi yake yalikuwa tayari kupigana.
Askari wa Moroni walileta silaha, na Moroni aliwapa deraya imara na ngao za kuwalinda.
Moroni alienda na majeshi yake kupigana na Walamani. Lakini wakati Walamani waliwaona Wanefi wako na silaha na ngao, walikuwa na uoga wa kupigana. Walamani walikuwa tu na mavazi mepesi na hawakuwa na silaha ya kuwalinda.
Walamani waliondoka. Walijaribu kuingia kisiri kwenye nchi tofauti ya Wanefi. Walifikiria Moroni hangejua pale walikwenda.
Lakini punde Walamani walipoondoka, Moroni aliwatuma wapelelezi kuwafuata.
Kisha Moroni alituma ujumbe kwa nabii Alma. Alimtaka Alma amuulize Bwana kile Walamani walikuwa wanapanga kufanya. Bwana alimwambia Alma kwamba Walamani walikuwa wanapanga kushambulia nchi hafifu iliyoitwa Manti. Moroni alimsikiliza Alma. Aliongoza majeshi yake kupigana dhidi ya Walamani.
Majeshi yalipigana Walamani walikuwa na nguvu sana na walikuwa na hasira sana. Wanefi wakawa wanawaogopa Walamani na walikuwa wanataka kutoroka. Lakini Moroni aliwakumbusha wao juu ya familia zao na imani yao, hivyo waliendelea kupigana.
Wanefi walisali kwa Bwana kwa ajili ya msaada. Bwana alijibu sala zao na akawapa nguvu nyingi. Sasa Walamani wakawa wanaogopa. Walikuwa wamenaswa kwenye mtego na hawakuweza kutoroka. Wakati Moroni alipoona kwamba Walamani wanaogopa, aliwaambia askari wake na kusitisha mapigano. Moroni hakutaka kuwaua Walamani.
Moroni alimwambia Zerahemna kwamba Walamani wangeenda zao kama wangeahidi kutopigana na Wanefi tena. Zerahemna alikasirika na kujaribu kuendelea kupigana, lakini hangeweza kuwashinda askari wa Moroni. Kisha Zerahemna na majeshi yake wakaahidi kuishi kwa amani, na Moroni akawaacha waende zao.