Scripture Stories
Mfalme Benyamini


“Mfalme Benyamini,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Mosia 1–5

Mfalme Benyamini

Kuwatumikia watu na Mungu

Picha
Benyanini akiandika kwenye mabamba ya dhahabu

Mfalme Benyamini alikuwa nabii wa Mungu ambaye alitawala nchi ya Zarahemla. Alifanya kazi kwa bidii kuwatumikia watu wake na kuwafundisha kuhusu Mungu. Kwa msaada kutoka kwa manabii wengine wa Mungu, Benyamini aliifanya Zarahemla kuwa sehemu ya amani na salama ya kuishi.

Maneno ya Mormoni 1:17–18; Mosia 1:1–7

Picha
Benyamini akiongea na Mosia

Benyamini alizeeka. Alimtaka mwanae Mosia kuwakusanya watu pamoja. Benyamini alitaka kuwaambia watu wake kwamba Mosia atatkuwa mfalme wao mpya.

Mosia 1:9–10

Picha
familia ndani ya hema

Watu wengi walikuja kutoka sehemu zote za nchi. Walijenga mahema yao karibu na hekalu ili kumsikiliza Benyamini.

Mosia 2:1, 5–6

Picha
watu karibu na mnara

Benyamini aliongea kutoka kwenye mnara ili kwamba watu wengi waweze kumsikia. Benyamini alisema kwamba Mungu alimsaidia kuwaongoza wao. Kama mfalme, aliwafundisha kutii amri za Mungu. Hakuchukua fedha zao au kuwafanya wamtumikie yeye. Badala yake, alifanya kazi kuwatumikia watu wake na Mungu.

Mosia 2:7–16

Picha
watu wakisaidiana wao kwa wao

Benyamini aliwaambia watu kwamba wanapotumikiana wao kwa wao, walikuwa pia wakimtumikia Mungu. Kisha akawaambia kwamba kila kitu walichokuwa nacho kilikuja kutoka kwa Mungu. Kama malipo, Mungu aliwataka wao kutii amri Zake. Walipotii, Mungu aliwapa baraka zaidi.

Mosia 2:17–24, 41.

Picha
Benyamini akiongea na Mosia akiwa karibu yake

Benyamini aliwaambia asingeweza kuwa mfalme wao au mwalimu zaidi ya hapo. Mwanawe Mosia atakuwa mfalme wao mpya.

Mosia 2:29–31

Picha
Yesu Kristo akimponya mtu

Kisha Benyamini aliwaambia watu wake kwamba malaika alimtembelea. Malaika alisema Mwana wa Mungu,Yesu Kristo, atakuja duniani. Atafanya miujiza na kuwaponya watu. Atateseka na maumivu na atakufa ili kuwaokoa watu wote. Benyamini alifundisha kwamba Yesu atamsamehe kila mtu ambaye alikuwa na imani katika Yeye na akatubu.

Mosia 3:1–12, 17–18

Picha
watu wenye furaha

Watu waliamini kile Benyamini alichowafundisha kuhusu Yesu. Walijua kwamba walihitaji kutubu. Watu wote walisali na kumwomba Mungu awasamehe. Baada ya kusali, Roho wa Mungu akawa pamoja nao. Walihisi furaha na kujua kwamba Mungu aliwasamehe kwa sababu ya imani yao katika Yesu.

Mosia 4:1–3, 6–8

Picha
watu pamoja na Benyamini na Mosia

Watu walijisikia tofauti na wapya ndani kwa sababu walikuwa na imani katika Yesu. Sasa walitaka kufanya mambo mema wakati wote. Walifanya ahadi ya kufuata amri za Mungu kwa maisha yao yote. Kwa sababu waliamini katika Yesu na walifanya ahadi hii, waliitwa watu wa Yesu.

Mosia 5:2–9, 15; 6:1–2

Chapisha