Scripture Stories
Saria


“Saria,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

“Saria,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

1 Nefi 2–3; 5

Saria

Safari ya imani ya mwanamke

Picha
Saria na Lehi

Saria aliishi Yerusalemu pamoja na familia yake. Mumewe, Lehi, alikuwa nabii wa Mungu. Siku moja Bwana alimwambia Lehi aondoke Yerusalemu pamoja na familia yake.

1 Nefi 2:1–3

Picha
Saria akisali

Saria alikuwa na imani katika Bwana. Yeye na familia yake waliacha nyumba yao. Waliiacha dhahabu na fedha yao na kwenda pamoja na Lehi nyikani.

1 Nefi 2:4–5

Picha
Saria akiwa nyikani

Saria na Lehi walichukua chakula na vitu vingine walivyohitaji. Baada ya kusafiri kwa siku nyingi, walijenga mahema kuishi katika nyika. Kisha walijenga madhabahu na walimshukuru Bwana kwa ajili ya msaada Wake.

1 Nefi 2:4, 6–7, 15

Picha
Saria akiwa mwenye wasiwasi na Lehi kwa mbali.

Siku moja Bwana aliwataka wana wa Saria na Lehi kwenda Yerusalemu na kuchukua mabamba ya shaba. Saria alitishika wakati wanawe walipokuwa hawarudi. Alifikiri walikuwa wamekufa. Lehi alimfariji Saria. Walichagua kuamini kwamba Bwana atawalinda wana wao.

1 Nefi 3:1–2, 4–6; 5:1–6

Picha
Saria na Lehi wakiwakaribisha wana wao

Saria alikuwa amejawa na furaha wana wao waliporudi kutoka Yerusalemu. Sasa alijua kwamba Bwana alikuwa amewalinda. Aliamini kwamba Bwana atawapa uwezo kufanya kile Yeye alichowaomba. Familia yote ya Saria ilikuwa na furaha, na walimshukuru Bwana.

1 Nefi 5:7–9

Chapisha