“Abishi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Abishi
Aliwasaidia watu wake kuamini katika Yesu
Abishi alimfanyia kazi malkia ambaye alikuwa Mlamani. Abishi alikuwa amejifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka kwa ono la baba yake. Kwa miaka mingi, aliamini katika Yesu na alitaka kumfuata Yeye. Lakini alikuwa hajamwambia Mlamani mwingine bado.
Siku moja, Mnefi aliyeitwa Amoni alikuja kwenye ufalme huu ili kuwafundisha Walamani kuhusu Yesu na Mungu. Malkia na mfalme waliamini kile Amoni alichofundisha. Malkia na mfalme walijua kwamba Yesu angekuja ulimwenguni na kumfanya kila mmoja ambaye aliamini katika Yeye aweze kusamehewa.
Alma 17:12–13; 18:33–36, 39–40; 19:9, 13
Malkia na mfalme walihisi Roho Mtakatifu na walikuwa na furaha sana kwamba walianguka ardhini. Amoni na watumishi walianguka pia. Abishi alikuwa ndiye tu aliyekuwa amesimama.
Abishi alitaka kuwaambia watu kuhusu muujiza huu. Alitumaini watu wangeamini katika nguvu za Mungu wakati walipoona kile kilichotokea. Kwa hiyo Abishi alikimbia nyumba hadi nyumba. Aliwaambia watu waende wakaone kile Mungu amefanya kwa ajili ya malkia na mfalme.
Watu wengi walikuja kwenye nyumba ya malkia na mfalme. Walishangaa kwa sababu ilionekana kana kwamba malkia, mfalme na watumishi wote walikuwa wamekufa.
Watu walikanganyikiwa. Walibishana kuhusu kile kilichomtokea malkia na mfalme.
Wakati Abishi aliporudi, aliona watu wakibishana. Alikuwa na huzuni sana kwa sababu hawakuona nguvu za Mungu. Kisha alichukua mkono wa malkia, na malkia alisimama na kumsifu Yesu.
Malkia alishikilia mkono wa mumewe, na alisimama. Mfalme aliwaambia watu kuhusu Yesu. Kisha Amoni na watumishi wengine walisimama. Waliwaambia watu kwamba Yesu alikuwa amewabadilisha wao. Sasa walitaka kufanya mambo mema tu. Watu wengi waliwaamini wao.
Kama vile Abishi alikuwa ametumaini, watu waliona nguvu za Mungu. Watu wengi waliamini katika Yesu na wakabatizwa. Walikuwa na Roho wa Mungu pamoja nao Hata walianzisha Kanisa katika nchi yao. Waliona kwamba Yesu anamsaidia kila mmoja ambaye anatubu na kuamini katika Yeye.