Hadithi za Maandiko
Alma na Watu Wake


“Alma na Watu Wake,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Mosia 23–25

Alma na Watu Wake

Nguvu kutoka kwa Mungu wakati wa nyakati ngumu

Alma na watu wengine wakitazama nyumba zao

Alma na watu wake waliishi katika nchi nzuri sana. Walipanda mbegu na kujenga majumba. Alma alikuwa kuhani wa Mungu. Aliwafundisha watu wake kupendana. Watu walimsikiliza Alma na kushika amri za Mungu. Familia zao zilikua, na walijenga mji.

Mosia 23:4–5, 15–20

Alma anazungumza na Walamani

Siku moja, jeshi la Walamani lilikuja. Walikuwa wamepotea njia. Walamani waliahidi kuwaacha watu wa Alma bila matatizo kama Alma angewasaidia kupata njia ya kwenda nyumbani kwao. Alma aliwaonyesha Walamani jinsi ya kurudi kwenye nchi yao.

Mosia 23:25, 30, 36–37

Amuloni na walinzi wakimchunga Alma na watu wake

Walamani hawakuheshimu ahadi yao. Badala yake, waliichukua nchi na kuweka walinzi wa kuwachunga watu wa Alma. Wao pia walimfanya Mnefi aliyeitwa Amuloni kuwa mfalme wa watu wa Alma. Amuloni alikuwa kiongozi wa makuhani wa uongo. Yeye na makuhani wake walikuwa wamemuua nabii wa Mungu na kufanya mambo mengine mengi mabaya.

Mosia 17:12–13; 23:31–32, 37–39; 24:9

Amuloni amekasirika

Amuloni alimkasirikia Alma. Aliwafanya watu wa Alma kufanya kazi ngumu sana na alikuwa mkatili kwao. Ilikuwa vigumu kwa watu wa Alma.

Mosia 24:8–9

Alma anasali, na Amuloni aliyekasirika yuko nyuma

Walisali kwa Mungu kwa ajili ya msaada. Amuloni aliwaambia waache kusali. Alisema mtu yeyote atakayesali angeuawa.

Mosia 24:10–11

Alma na mwanamke wakimsaidia mwanaume mkongwe kusimama

Alma na watu wake waliacha kusali kwa sauti. Badala yake, walisali mioyoni mwao. Mungu alisikia sala zao. Yeye aliwafariji wao na aliwaahidi kuwasaidia kutoroka. Mungu alifanya kazi yao ngumu kuwa nyepesi. Watu walikuwa na subira na furaha walipokuwa wanamsikiliza Mungu. Walijua Yeye atawasaidia wao.

Mosia 24:12–15

Alma anawaongoza watu wake kutoroka usiku

Watu wa Alma walimtumainia Mungu na walikuwa na imani kubwa katika Yeye. Siku moja, Mungu aliwaambia muda wao wa kuondoka umefika. Usiku ule, Alma na watu wake wakawa tayari. Walikusanya wanyama wao wote na chakula. Asubuhi, Mungu aliwafanya Walamani walale usingizi mzito. Ndipo Alma na watu wake walitoroka na kusafiri siku nzima.

Mosia 24:16–20

Alma na watu wake wakitazama Zarahemla

Usiku ule, wote wanaume, wanawake na watoto walimshukuru Mungu. Walijua ni Mungu tu angeweza kuwasaidia wao. Waliendelea kusafiri kwa siku nyingi na kufika nchi ya Zarahemla. Wanefi waliwakaribisha, na Alma alimfundisha kila mmoja kuhusu kuwa na imani katika Yesu Kristo. Watu wengi waliamini na wakabatizwa.

Mosia 24:20–25; 25:14–24