Scripture Stories
Mosia na Zenivu


“Mosia na Zenivu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Omni 1; Mosia 9

Mosia na Zenivu

Kulindwa na Bwana

Picha
Mosia akiwaongoza watu

Wanefi na Walamani walikuwa na vita vingi. Siku moja, Bwana alimwambia Mnefi aliyeitwa Mosia kuondoka nchi ya Nefi pamoja na kila mmoja ambaye angemfuata Bwana.

Omni 1:10,12

Picha
Mosia akitazama jiji

Wanefi wengi walimtii Bwana na waliondoka na Mosia. Bwana aliwaongoza kwenye nchi ambayo ilikuwa na watu wakiishi ndani yake. Waliitwa watu wa Zarahemla.

Omni 1:13–14

Picha
Mosia akiongea na watu

Watu wa Zarahemla pia walikuja kutoka Yerusalemu hapo kale. Walikuwa na furaha Bwana aliwatuma Wanefi pamoja na mabamba ya shaba. Watu wa Mosia waliungana na watu wa Zarahemla. Watu wote walimchagua Mosia kama mfalme wao. Aliwafundisha kuhusu Bwana.

Omni 1:14–19

Picha
Zenivu akiwaongoza watu

Wanefi wamekuwa wakiishi Zarahemla kwa muda sasa wakati kundi kubwa la watu lilirudi kwenye nchi ya Nefi. Waliongozwa na Mnefi aliyeitwa Zenivu

Omni 1:27–29; Mosia 9:3–5

Picha
mfalme Mlamani akiongea

Walamani sasa waliishi katika nchi ya Nefi, kwa hiyo Zenivu alimwomba mfalme wao kama watu wake wangeweza pia kuishi pale. Mfalme alikubali.

Mosia 9:6–10

Picha
Walamani wakishambulia

Mfalme alimlaghai Zenivu na watu wake. Aliwaacha waishi katika nchi ya Nefi ili aweze kuchukuwa baadhi ya chakula na wanyama wao. Watu wa Zenivu waliishi pale kwa amani kwa miaka mingi. Walipanda chakula kingi na walikuwa na wanyama wengi. Kisha Walamani wakawashambulia na walijaribu kuchukua chakula chao na wanyama wao.

Mosia 9:10–14

Picha
Watu wa Zenivu wakishinda mapigano

Zenivu aliwafundisha watu wake kumtegemea Bwana. Wakati Walamani walipokuja kupigana nao, Zenivu na watu wake waliomba kwa Bwana. Bwana aliwapa nguvu na alisaidia kuwalinda. Waliweza kuwafukuzilia mbali Walamani. Bwana alimbariki Zenivu na watu wake kwa ajili ya imani yao.

Mosia 9:15–18

Chapisha