Scripture Stories
Dhoruba Baharini


“Dhoruba Baharini,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Dhoruba Baharini.” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

1 Nefi 18

Dhoruba Baharini

Kupata amani katika Bwana

Picha
familia zikileta chakula ndani ya merikebu

Bwana alimwambia Lehi kwamba ulikuwa muda muafaka kuingia kwenye merikebu. Familia zilipakia chakula kingi cha kula walipokuwa wakisafiri. Wote waliingia ndani ya merikebu na kusafiri kuelekea nchi ya ahadi.

1 Nefi 18:5–8

Picha
watu wakinywa wakiwa kwenye merikebu

Baada ya siku nyingi baharini, baadhi ya watu walianza kutokuwa na heshima na wafidhuli Walisahau kwamba Bwana aliwasaidia.

1 Nefi 18:9

Picha
Lemueli, Nefi, na Lamani kwenye merikebu na dhoruba inakuja.

Nefi alikuwa na hofu kwamba wangeweza kumuudhi Bwana. Bila msaada wa Bwana, merikebu yao haingekuwa salama. Nefi aliwaomba kaka zake kuacha.

1 Nefi 18:10

Picha
Lamani na Lemueli wanamfunga Nefi.

Lamani na Lemueli walimkasirikia mno Nefi. Walimfunga na walikuwa wakatili kwake. Hawakumtii Bwana, na Liahona ikaacha kufanya kazi. Mara dhoruba kubwa ikaja. Baada ya siku tatu katika dhoruba, wote waliingiwa na woga kwamba watazama.

1 Nefi 18:10–13

Picha
wanawake wakiwaomba Lamani na Lemueli

Familia ya Nefi iliwaomba Lamani na Lemueli wamfungue Nefi. Lakini Lamani na Lemueli bado hawakutaka mtu ye yote amfungue Nefi. Saria na Lehi walihuzunika na wakawa wagonjwa sana. Dhoruba haikwisha.

1 Nefi 18:17–19

Picha
Nefi na Liahona

Katika siku ya nne, Lamani na Lemueli walijua merikebu ilikuwa inakaribia kuzama. Walitubu na walimfungua Nefi. Nefi aliposali, dhoruba ilisha. Liahona ilifanya kazi tena. Nefi aliitumia hiyo kuongoza merikebu katika mwelekeo sahihi.

1 Nefi 18:14–15, 20–22

Picha
familia zikitoka kwenye merikebu na Lehi akiomba

Baada ya siku nyingi, familia zilifika kwenye nchi ya ahadi.

1 Nefi 18:23

Chapisha